Uchaguzi 2020 PICHA: Tundu Lissu Misungwi, maelfu ya watu wakishuhudia mkutano wake

Uchaguzi 2020 PICHA: Tundu Lissu Misungwi, maelfu ya watu wakishuhudia mkutano wake

dikteta2020

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2018
Posts
595
Reaction score
3,991
Mkutano: Maelfu ya watu Wilayani Misungwi wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Tundu Lissu

Nitaweka link ili mumfuatilie live akiwa Misungwi muda huu.

Wakuu najaribu kuweka link inagoma ila mkutano upo live ndani ya Dar mpya online tv

Lissu anasema hivi
1. Wagombea wote wa Chadema ngazi ya udiwani na Ubunge Misungwi walienguliwa kihuni na tume baada ya jaribio la kuwateka kushindikana.
2. Tume wanatulazimisha tupigane na tutapigana kwa ajili ya haki, nasema tutapigana.

3. Najua kuwa tutashinda kwa kishindo uchaguzi huu, ole wao tume watuibie ushindi wetu nasema Ole wao!

4. Tundu Lissu: Tukiingia ikulu tutaweka katiba mpya ambayo pamoja na mambo mengine itafutilia mbali hii tume ya uchaguzi iliyopo.

5. Lissu: Nikiwa Rais viongozi wa serikali za mtaa na vijiji ambao hawakupatikana kihalali wataondolewa na uchaguzi kufanyika upya chini ya tume mpya ambayo ni huru.

Lissu anaonyesha kukerwa na wagombea kuenguliwa na anasema tume inawalazimisha wapigane na wapo tayari!
Bado anaendelea, fuatilia live ndani ya Dar mpya
20200925_145612.jpg

 
Misungwi wamekataa kutumika. Sasa najua unahaha kutafuta picha za bukoba uweke hapa. Mi nimeona live na link iko youtube.

Lissu ameshachelewa kuupata urais wa nchi hii, amebakiza uongo tu.
 
Mwambie mboe aje akusaidie kurudisha wagombea, maana ni kama vile wamekutosa
 
Back
Top Bottom