Picha ya Dunia yenye high resolution kutoka space imepigwa na Artemis II!

Kwa namna hali ya hewa ilivyo kwa sasa karibia kila sehemu mawingu yametanda tena muda wote, akili yangu inawauĺza hizo kamera zao huwa zinayayeyusha mawingu kwanza ndio zinapiga picha, maana naona picha inaonyesha ardhi ya afrika ilihali afrika kwa sasa mostly imefunikwa na mawingu.

Msinishambulie nimetumia akili zangu kuwaza.
 
Walete flat earthers wakina DR Mambo Jambo
the same old story the same old myth...
unaamini kabisa hiyo picha imepigwa juzi au imepigwa na appolo? halafu ukiangalia picha hiyo inakuonyesha Duna ni dura lenye kipenyo kinachofanana ila wanasayansi hao hao wanakuambia dunia ni Yai umbo la yai..

cha ajabu taswira ya dunia inayoonekana hapo iliundwa zamani sana kabla hata ya kwenda mwezini miaka ya 1400-1700...
propaganda lazima waithibitishe kwa sababu vijana wa siku hizi haya genz na gen alpha wanataka uthibitisho so ni lazima ilikuwa wawape ili waendelee kuwatawala ki ideas

wanakuambia dunia inazunguka kwa kasi kwenye muhimili halafu ukiangalia picha waliotuma inaupande mmoja tu wa afrika means dunia iko still haizunguki na ndo maana picha ina upande mmoja....THINK
 
Nasubiri majibu ya hii comment nipo kujifunza

Yoda
 
Dunia ni oblate spheroid, Waswahili ndio walifananisha na yai.
Hakuna conspiracy inayoweza kudumishwa na kubaki siri kwa nchi zaidi ya 20 zilizowahi kuwa katika space projects na zenye satellites angani, zaidi sana hakuna conspiracy inayoweza kudumishwa kati ya US, Canada, Ulaya, Russia na China.
 
picha ya oblate ni kweli bado hatujapewa,
 
Tusubiri majibu hapa.
 
mkuu Usisahau the controller ni Mmoja tu wa anga na ardhi ni NASA ndo anajua whch information to feed us...
can you tell me kwanini mpaka leo Mercator projection ya mwaka 1569 iliyoandaliwa na Gerardus Mercator akiwa amekaa kibarazani mwake akinywa juice akaichora enzi hizo hakuna hata ndege wala rockets na hakuwahi kwenda mwezini wala angani, kwanini hakuna version mpya ya ramani na kila siku tunaenda mwezini?

ikumbukwe nasa imeanza kufanya kazi mwaka 1958 wakati huo tayari kuna ramani ya dunia na mpaka kuna umbo la dunia
 
Picha mpya ya Dunia imepigwa kutoka Artemis II. View attachment 3567044
Umejuaje kama ni ukweli kama walishatudanganya mara nyingi tu na picha zao hizo. Angalia picha ya dunia inaonyesha Afrika ni ndogo kuliko Ulaya na Asia wakati vipimo vinaonyesha Afrika ni kubwa kuliko Ulaya na Asia kwa pamoja. Wazungu hawaaminiki 100% wako kibiashara zaidi.
 
Chuoni nakumbuka Kuna kitu tulikisoma kwenye G.I.S na hydrometeorology pale MWECAU kinauhusiana na swali ulilouliza hapa
Picha za satellite za uso wa Dunia hupitia hatua nyingi za kuboreshwa kabla hazijaonekana clear. Baadhi ya hatua hizo ni:
Radiometric correction
Hurekebisha mwanga na intensity ya picha ili sehemu zisizo na mwanga mwingi zisionekane nyeusi sana au zenye mwanga mwingi zisionekane kupita kiasi.
Geometric correction
Hurekebisha distortion inayotokana na mwendo wa satellite, mzunguko wa Dunia, au angle ya kamera ili maeneo yaonekane mahali sahihi kwenye ramani.
Atmospheric correction
Huondoa athari za ukungu, mawingu , vumbi, moshi, unyevunyevu na reflection ya mwanga kwenye anga ambayo inaweza kufanya picha ionekane hafifu.

Sharpening
Huongeza ukali wa mipaka ya vitu kama barabara, mito, majengo na mashamba.
Contrast enhancement
Huongeza tofauti kati ya maeneo tofauti kama misitu, maji, jangwa na miji ili vitu vitambulike kirahisi.
Noise reduction
Huondoa dots au mistari inayoweza kusababishwa na sensor ya satellite au signal interference.
False color rendering
Wakati mwingine satellite hutumia colors zisizo za kawaida ili kuonyesha vitu vizuri zaidi. Kwa mfano mimea inaweza kuonekana nyekundu badala ya kijani ili ionekane wazi zaidi kwenye uchambuzi wa kilimo au misitu.
Image stacking and mosaicking
Satellite inaweza kupiga picha nyingi za eneo moja kisha zikachanganywa kupata picha moja yenye ubora mkubwa zaidi na mawingu machache.
Super-resolution techniques
Mbinu za kisasa za Machine Learning na Deep Learning hutumika kuongeza resolution ya picha na kufanya maelezo yaonekane zaidi kuliko picha ya awali.
Pansharpening
Hii ni mbinu muhimu sana kwenye satellite imagery ambapo picha ya black-and-white yenye detail kubwa huunganishwa na picha ya color yenye detail ndogo ili kupata picha ya color iliyo sharp zaidi.
Katika mifumo kama Google Earth au picha kutoka NASA na European Space Agency, karibu kila picha huwa imepitia hatua nyingi za processing kabla hujaiona.

NB: point zingine hapa ni kwa msaada wa Chatgpt... Ili uelewe kwa upana kiasi 📌📌📍
 
We jamaa ni mjinga...
Unabishana na science .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…