Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

wana CCM wafia chama ni waoga mno, mnaweza kupanga kupindua MEZA, siku ya tukio ukajikuta umebakia peke yako watu washakula kona kitambo.
Ila wafiachama hao ni hatari! Wanaweza mshusha mtu mshipa akajiondokea mwenyewe. Hii miaka mitano walidhani wataisoma wapinzani lakini na wao wanaisoma hata ule wimbo "wataisoma" siku hizi ukiwambaia waimbe utanuniwa tuu!
 
Hili ni dongo kwa Bashite??!!!
FB_IMG_15726070388591373.jpg
 
Huu utetezi wako unafungua milango mingi sana; kwahiyo sababu Trump anatukanwa basi na Rais wetu atukanwe. Sababu USA wanaruhusu ushoga na TZ turuhusu ushoga. Sababu USA wanaruhusu bangi na sisi turuhusu. Sababu USA Kuna vyama viwili vikubwa na sisi tubaki na vyama viwili tu. Sijui unaishia wapi na nani wakusema hiki tuige kile tusiige.

Sikubaliani na Idris kushikwa ila napingana na utetezi wako.
Kosa la Idris ni lip
 
Makonda ni sikio la kufa, ndo maana Katibu mkuu alimkemea, ila cha ajabu halijifunzi.

Nina wasiwasi na matokeo yake darasani!
 
Kiwekwe kipengere cha kuwapiga saspensheni hawa viongozi wapuuzi ili waskilizie uchungu wa kitaa!
 
Makonda ni sikio la kufa, ndo maana Katibu mkuu alimkemea, ila cha ajabu halijifunzi.

Nina wasiwasi na matokeo yake darasani!
Kuna tabia Fulani kijana yeyote rijali akiingia tuu, basi anakuwa na tabia za hovyo hovyo kama kajamaa na maumbile yana badilika. Ngoja nitafute picha nitakuonyesha, lakini nadhani umenielewa
 
Jamani, mimi naamini this is a ruse. Watu wameingizwa kwenye mjadala wa kijinga ili wapotezee vituko vya kipumbavu vinavyooendele kwenye huo uchaguzi wao.
 
Angalieee asitake ligi na king wa dar anaweza akanyimwa viza asikanyage dar

Ova
 
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwa jina la Baba_Keagan amepakia ujumbe unaosema ''Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako''
​
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mchekeshaji Idris Sultan alipakia picha mbili za Rais Magufuli ambazo zimehaririwa na kuandika maneno haya "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani''

Ikumbukwe jana ilikuwa ni siku ya kusherekea mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Rais Magufuli na watu, taasisi na mashirika mbalimbali ya walituma salamu za siku ya kuzaliwa.

Kuna wengine walienda mbali mpaka kutengeneza video za utani, mfano Mchungaji muhuni, Masanja Mkandamizaji alipakia video ikimuonesha akiimwagia maji picha rasmi ya Rais Magufuli inayotumiwa kwenye ofisi,taasisi na mashirika mbalimbali kwa mujibu wa sheria.



======

UPDATES

Baada ya mchekeshaji Idris Sultan kutakiwa ajisalimishe Polisi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema yupo Tayari kumuwekea Mwanasheria wa kumtetea na kumdhamini Msanii huyo.

Ameyasema hayo kwenye Ukurasa wake wa Twitter. "Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo". Amesema Kigwangalla.

Kazingua idrisa..
 
sioni kosa...

nadhani nishajua ni nani anachochea maugomvi na chuki za chini chini huko jijini Dar!

by the way, "belated birthday greetings Mr. President" 🙌
 
Back
Top Bottom