Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Picha ya Rais: RC Makonda amtaka Msanii Idris Sultan kujisalimisha kituo cha Polisi

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwa jina la Baba_Keagan amepakia ujumbe unaosema ''Naona mipaka ya kazi yako huijuwi. Nenda sasa hivi kituo chochote Cha polic uwambie Makonda kaniambie nije utakuta ujumbe wako''
​
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, mchekeshaji Idris Sultan alipakia picha mbili za Rais Magufuli ambazo zimehaririwa na kuandika maneno haya "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani''

Ikumbukwe jana ilikuwa ni siku ya kusherekea mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Rais Magufuli na watu, taasisi na mashirika mbalimbali ya walituma salamu za siku ya kuzaliwa.

Kuna wengine walienda mbali mpaka kutengeneza video za utani, mfano Mchungaji muhuni, Masanja Mkandamizaji alipakia video ikimuonesha akiimwagia maji picha rasmi ya Rais Magufuli inayotumiwa kwenye ofisi,taasisi na mashirika mbalimbali kwa mujibu wa sheria.


Idris.PNG

======

UPDATES

Baada ya mchekeshaji Idris Sultan kutakiwa ajisalimishe Polisi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema yupo Tayari kumuwekea Mwanasheria wa kumtetea na kumdhamini Msanii huyo.

Ameyasema hayo kwenye Ukurasa wake wa Twitter. "Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo". Amesema Kigwangalla.

1572434683721.png


26AD7384-E3DA-453C-993A-C170E39DDAC9.jpeg
 
Back
Top Bottom