PreGE2025 POTOSHI Picha ya Rais Samia akifuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu

PreGE2025 POTOSHI Picha ya Rais Samia akifuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Picha inaelezea vitu vingi.

IMG_20250701_115834.jpg
 
Tunachokijua
Tarehe 01, Julai 2025 Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu imeendelea kuunguruma huku ikirushwa mbashara kwa njia ya mtandao na vyombo mbalimbali vya habari ili kutoa nafasi kwa umma kufuatilia kinachojiri katika kesi hiyo iliyoarishwa hadi Julai 15, 2025.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na X walichapisha picha inayomuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na wasaidizi wake, wakionekana kufuatilia kesi inayomkabili Tundu Lissu, kupitia matangazo mbashara yaliyorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini kuwa picha hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika ukurasa wa Ikulu kwenye mtandao wa X tarehe 13, Juni 2024.

Rais Samia alikuwa akifuatilia Bunge la Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2024/25 kwa njia ya runinga akiwa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma. Hotuba hiyo ilikuwa ikisomwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Picha hiyo imepotoshwa kwa kubadilishiwa picha ya Televisheni, ambapo imeondolewa iliyokuwa ikonesha Televisheni ya Taifa iliyokuwa ikirusha matangaza ya bajeti kuu ya serikali 2024/25 na kuweka picha ya matangazo ya ITV inayohusu matangazo mbashara ya Kesi inayomkabili Tundu Lissu
1751363784879-png.3390216
Mhe. Rais mwachie huyo mtu! Mshirikishe kwenye serikali yako ijayo kuunda mifumo mizuri ya kisheria ya nchi. Pamoja na utukutu wake anayo mema pia hasa ya kuonesha udhaifu wa mifumo yetu ili irekebishwe twende vyema kama nchi.
Huo utukutu wewe ndo unao MTU anapambania haki na utawala bora unasema mtukutu
 
Mbona ka picha imetengenezwa kwa akili mnemba
 
Elimu
Elimu
Elimu

KAZI ni kipimo cha utu
 
Edited hiyo
Hapo walikua wanafuatilia kuwasilishwa kwa bajeti kuu ya serikali.
 
M ningekuwa samia huyu lisu nafanya mwana sheria mkuu wa serikali afu pia aendelee kuwa mwenyekiti wa chama chake afanye reforms kwenye serikal yangu
je kama wana ccm hawataki afanyaje?
 
Back
Top Bottom