PreGE2025 POTOSHI Picha ya Rais Samia akifuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu

PreGE2025 POTOSHI Picha ya Rais Samia akifuatilia kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Picha inaelezea vitu vingi.

IMG_20250701_115834.jpg
 
Tunachokijua
Tarehe 01, Julai 2025 Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu imeendelea kuunguruma huku ikirushwa mbashara kwa njia ya mtandao na vyombo mbalimbali vya habari ili kutoa nafasi kwa umma kufuatilia kinachojiri katika kesi hiyo iliyoarishwa hadi Julai 15, 2025.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Instagram na X walichapisha picha inayomuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na wasaidizi wake, wakionekana kufuatilia kesi inayomkabili Tundu Lissu, kupitia matangazo mbashara yaliyorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Je, ni upi uhalisia wa picha hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini kuwa picha hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika ukurasa wa Ikulu kwenye mtandao wa X tarehe 13, Juni 2024.

Rais Samia alikuwa akifuatilia Bunge la Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2024/25 kwa njia ya runinga akiwa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma. Hotuba hiyo ilikuwa ikisomwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Picha hiyo imepotoshwa kwa kubadilishiwa picha ya Televisheni, ambapo imeondolewa iliyokuwa ikonesha Televisheni ya Taifa iliyokuwa ikirusha matangaza ya bajeti kuu ya serikali 2024/25 na kuweka picha ya matangazo ya ITV inayohusu matangazo mbashara ya Kesi inayomkabili Tundu Lissu
1751363784879-png.3390216

Attachments

  • Screenshot_20250701_124415_Instagram.jpg
    Screenshot_20250701_124415_Instagram.jpg
    243.8 KB · Views: 20
Nadhani hata Bunge Live huwa aangaliii, TL ana kitu fulani hivi, ila kiko uncoordinated
 
Kama yalivyo mabillion ya nyota angani, ndivyo wanavyohitajika MATAGA namba kama hiyo kumatch IQ ya Lissu.
 
Back
Top Bottom