Ilishawahi kutokea kwangu hapo nyuma kidogo...!
Nilimfungulia Sister angu facebook account, simu yake Ilikua inazingua, so nikamfungulia kupitia kwangu kwa Chrome then nika log in kwake, nikamwelekexa kidogo then nikamwacha a enjoy....!
Baada ya miaka kama 3, kukatokea shida kidogo kwa facebook app, nikawa siwezi ku log in, ikasema ngoja niingie kwa kutumia Chrome then baadaye ntarekebisha kuhusu app, coz kuna mtu muhimu wa nje nilijua atakua keshatuma message...!
Ku search facebook ikafunguka, chap nikaenda messenger nikagundua hii sio facebook yangu, nikakumbuka Miaka 3 nyuma nilimfungulia Account sister angu...!
Nikaanza kusoma messages, Lah...! Haula.,...!
Nikajikuta natetemeka siamini nachokiona, sister angu ni mkubwa sana kwangu, ndo alinilea mimi, naanza Maisha yangu nikitoka kwake, ni kama Mzazi hivi kwangu, kukuta chatting zake na Wanaume wengine nje ya Shemeji yangu kulinipa Shida sana, hafu sio mwanaume mmoja...!
Kwa miaka 3 hiyo keshaliwa na 3, kuna kama 4 wanalishia, 2 kawaelewa, mmoja nadhani siku yeye tu akiamua akale mzigo, mwingine ndo wanaweka mambo sawa...!
Hawa 2 ndo Damu hazikuendana nadhani, kila wakitupa sound zinatolewa Mbavuni, anawaambia waache kumsumbua...! Nika log out kwa account yake...! Nikaanza kumtafakari...!
Hakuna anachokosa, mme wake ni aina ya mtu akinunua Gari mpya yake, ujue atanunua mpya pia kwa mkewe, ana kila kitu.... Nikasema WHY....!?
Nikasema japo ni mkubwa kwangu nitamwita....! Wakati najiandaa kumwita kuna jambo likatokea sehemu yake ya biashara, kwa nje hutaona kama lina uhusiano na mambo ya kuchepuka, ila mimi nikaenda kufanya Uchunguzi nikapata picha, nikamwambia nataka tuongee, akakataa coz alihisi nataka kuongea nae nini hasa kwa tukio la pili...!
Nikamwambia kama atakataa kuonhea na mimi means anakataa Ujumbe wa Mungu kupitia mimi... (Sio mlokole na Kanisani niliasi)
Akakubari...!
Tukaonana, nikaanzq kumpa Makavu yake mwanzo Mwisho, nikamwambia umri huo ukiachika utaenda wapi...!?
Nilimsema sana, na ukweli mpaka leo huwa ananambia kikao changu na yeye kilibadirisha Maisha yake... Huwa ananishukuru...!
Binadamu ni Wabishi tu na ujuaji mwingi usio na Maana, wale wanawake walojitunza ujanani, wakiingia kwenye Ndoa, wakikutana na changamoto kidogo tu kwenye Ndoa, huwa wanafungua Mlango, Shetani anachofanya ni kuchochea tu hisia zao, na vile wenzetu wanatumia hisia zaidi, Shetani anakazia hapo, kitakachofata ni Mke wako atafunuliwa ovyo ovyo na Wanaume tofauti huku yy akiona hakuna tatizo coz hujui, sasa Mungu ana namna ya kusaidia Watu wake.....!
Niamini mimi Mungu anataka kumsaidia Dada ako kupitia wewe, wewe mwenyewe nadhani hata issue ya kupiga picha kwa simu ya Dada ako haikua planned...!
Muite Dada ako, ni Damu yako, achana na mawazo Negatively ya members hapa, wengine ni Wanawake walishaingia mkataba na Satan.
Mkanye, mwambie aache.... Mwambie asipoacha kuna kitu kibaya kitatokea... Then Mungu atamgusa, ataacha njia yake Mbaya..!
Mwambie afunge na Kuomba, ni kwa njia hiyo tu ndo Ndoa yake itakua salama...!
Shetani anaharibu Ndoa nyingi sasa katika ulimwengu wa Roho....!
Mlio kwenye Ndoa.....Bila kufunga, bila maombi.... Hamtatoboa....! Sisemi juu ya Ulokole.... Nasema wewe mwenyewe funga na kuomba....! Ukifunga na kuomba utakua karibu na Mungu, then yeye menyewe atakupa njia.....!
Mkuu...! Mkanye Sister ako, usiogope, mimi nilifanya hivyo na ilimsaidia....!