Picha za kwanza zatolewa za mkutano wa Mkuu wa Majeshi na Rais Robert Mugabe

Picha za kwanza zatolewa za mkutano wa Mkuu wa Majeshi na Rais Robert Mugabe

Taarifa ambazo nimezipata hivi punde zinasema kwamba ombi la Rais Mugabe kuruhusiwa kwenda uhamishoni nchini Afrika ya Kusini limekataliwa na kwamba Mkewe Grace ( jina la Utani Gucci Grace kutokana na tabia yake ya kupenda kufanya manunuzi ya Vitu vya gharama katika Maduka makubwa makubwa na ya Kitajiri ) atakuwa amekimbilia kati ya Namibia, Botswana, Dubai na Malaysia ambako imegundulika Mali nyingi za Familia ya Rais Mugabe ziko huko.

Na taarifa za ndani kabisa kutoka kwa Watu wa karibu na Rais Mugabe zinasema kwamba kuna uwezekano mkubwa sana Mkewe Grace akaachana rasmi na Mumewe Mugabe na kuondoka na Watoto zake Watatu wawili wa Kiume na Binti mmoja ambao wanaishi Johannesburg Afrika ambako pia kuna Mali nyingi sana za Rais Mugabe ila kutokana na ile Kesi inayomkabili Mkewe ( Grace ) imeshindikana kwa wao kuishi huko hivyo sasa hizi Mali zote zinatarajiwa Kuuzwa.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa sana kwamba sharti pekee ambalo atapewa Rais Mugabe ili ama aachiwe akimbie huko anakotaka kwenda au aishi hapo hapo Zimbabwe bila kubughudhiwa ni kukubali Mali zake zote zitaifishwe na afilisiwe Utajiri wake wote aliojilimbikizia kwa muda wote huu aliokuwapo Madarakani. Na dalili zote za hili kuwezekana lipo wazi hasa ukizingatia kwamba Rais Mugabe kwa sasa hana tena ujanja na ukizingatia kwamba hata afya yake si nzuri na kuna taarifa za chini chini zinasema huenda hali hii ya Kisiasa iliyopo huko sasa ikaathiri hata afya yake na kupelekea Umauti wake siku si nyingi.
 
667.jpg


Hapa ndio wanafurahia kabisa.
 
Hii picha ya mwisho mbona kama Mugabe anabembeleza kwa Mkuu wa Jeshi ili aendelee kukalia kiti?
Kwasasa yule delila hayupo mzee anaweza kuachiwa muda ajifie kitini. Tatizo lilikua kwamba mke wangu atashika madaraka. Ndo hawa wahenga wakaona mzee usitutanie
 
Hakuna damu itakayomwagika huyo cdf na Mugabe ni marafiki tangu walivyokuwa na miaka 20 ,walikuwa msituni pamoja

Kauli ya cdf hawana shida na bob Bali wanaomzunguka zanu pf

Hakuna hata risasi italayomwagwa ,wana settle maslahi yao tu na hata Bob akiondolewa ,ataondolewa kwa kubembelezwa na heshima

Kosa la Bob ni kumfukuza rafiki yao wa zamani vice ,hata Bob akikataa hakuna damu itakayomwagwa ,wanajuana hao hvyo watayamaliza kwa amani
Hivi wanasiasa unawajua kweli likija suala la madaraka wanavyokuwa? Makamu Emmerson Mnangagwa alikuwa swahiba wake kabla ajampata Bi Crace. Lakini chek alivyomdhalilisha.

Acha kabisa kuamini hivyo, kuna matukio mengi yaliyotokea kuhusu hilo.
 
Huyu alikuwa wa kuuwawa tu sio kufanya naye vikao
 
Wanajeshi gani wanafanya mazungumzo [emoji23][emoji23][emoji23] upuuuz mtupu
 
Back
Top Bottom