Picha zikiwaonyesha Wazamiaji wakidandia meli kwa kukaa kwenye kizimba cha majembe ya kusozea meli kwa muda wa siku 11

Picha zikiwaonyesha Wazamiaji wakidandia meli kwa kukaa kwenye kizimba cha majembe ya kusozea meli kwa muda wa siku 11

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
Watu watatu wamekutwa wamekaa juu ya kizimba cha majembe ya kusozea meli

1669800591842.png


Mlinzi wa pwani ya Uhispania amewaokoa watu watatu waliopatikana wakiwa wamejiegesha juu ya ukingo wa majembe ya kusozea meli iliyowasili katika visiwa vya Canary kutoka Nigeria.

Wanigeria Watatu Wapatikana Wakiwa Wamekaa Kwenye Ungo wa Meli Walinusurika kwa kusafiri Safari ya Siku 11 Kutoka Nigeria.

1669800694261.png


Katika picha iliyosambazwa na walinzi wa pwani siku ya Jumatatu, wahamiaji hao wanaonyeshwa wakiwa kwenye majembe ya meli ya mafuta na kemikali ya Althini II.

Waliwasili Las Palmas huko Gran Canaria Jumatatu baada ya safari ya siku 11 kutoka Lagos nchini Nigeria.

1669800767692.png


Haya Ndio Matokeo Ya Ugumu wa maisha Nchini Nigeria
Wahamiaji hao walipelekwa bandarini na kuhudumiwa na huduma za afya,

1669800860190.png


Wanaume hao, waliopatikana wakiwa kwenye ukingo wa majembe ya kusozea meli ya mafuta ya Alithini II kwenye bandari ya Las Palmas, walionekana kuwa na dalili za upungufu wa maji mwilini na hypothermia na walihamishiwa katika hospitali za kisiwa hicho kwa matibabu.

Meli hiyo yenye bendera ya Malta iliondoka Lagos, Nigeria mnamo Novemba 17 na kufika Las Palmas Jumatatu, Novemba 28, 2022.

1669800918315.png


Ijapokuwa ni hatari sana, si mara ya kwanza kwa wazamiaji wa meli kupatikana wakisafiri kwa kudandia ukingo wa majembe ya kusozea meli za kibiashara hadi Visiwa vya Canary.

Mwaka jana mvulana wa miaka 14 wa Nigeria alihojiwa na gazeti la El País la Uhispania baada ya kunusurika kwa wiki mbili kwenye majembe ya meli, Alikuwa pia ameondoka Lagos.

Miguu yao ilikuwa ikining'inia kwa inchi chache tu juu ya maji nyuma ya kizimba hicho kikubwa. Walitibiwa kwa upungufu wa maji mwilini na hypothermia.

Meli hiyo - iliyoondoka Lagos, Nigeria, mnamo Novemba 17 - ilisafiri maili 2,000 wakati wa safari ya siku 11 hadi eneo la Uhispania Kaskazini Magharibi mwa Afrika.
1669800975507.png


Txema Santana, mshauri wa uhamiaji wa serikali ya mtaa, alisema katika tweet: "Sio wa kwanza na hautakuwa wa mwisho. Mnamo 2020, mvulana wa miaka 14 wa Nigeria alihojiwa baada ya kudumu kwa siku 15 kwenye kizimba cha meli baada ya safari kutoka Lagos.
Alinusurika kwa maji ya chumvi na kwa kulala kwa zamu kwenye shimo juu ya kizimba pamoja na watu wengine aliokuwa akisafiri nao.

“Tulikuwa dhaifu sana. Sikuwahi kufikiria inaweza kuwa ngumu hivi.” kijana alisema. Pia mwaka huo, wanaume 4 walipatikana kwenye kizimba cha meli ya mafuta ya Norway Champion Pula, ambayo pia ilisafiri kutoka Nigeria hadi Las Palmas. Walijificha kwenye chumba nyuma ya majembe wakati wa siku 10 baharini.

1669801031134.png

Maelfu ya wahamiaji na wakimbizi wa Kiafrika wamefika Visiwa vya Canary katika miaka ya hivi karibuni kwa kufanya safari hiyo hatari kwa boti zilizojaa watu baada ya kuondoka katika pwani ya Morocco, Sahara Magharibi, Mauritania na hata Senegal.

Kufikia sasa mwaka huu, zaidi ya watu 11,600 wamefika visiwa vya Uhispania kwa boti.

1669801296991.png


Chanzo: CNN

1669801101123.png
 
Ukisikia mtu fulani ni muhuni, au ana roho ngumu ndiyo Hawa sasa.halafu uwaimbie sisiem mbele kwa mbele sijui kama watakuelewa

Siyo wale panyaroad wanaokata nyavu za madirisha kutokana na njaa huku wakihatarisha maisha ya watu

Hawa wao Wana risk maisha yao bila kusumbua wengine
 
Ukisikia mtu fulani ni muhuni, au ana roho ngumu ndiyo Hawa sasa.halafu uwaimbie sisiem mbele kwa mbele sijui kama watakuelewa

Siyo wale panyaroad wanaokata nyavu za madirisha kutokana na njaa huku wakihatarisha maisha ya watu

Hawa wao Wana risk maisha yao bila kusumbua wengine
Hiyo ni kukuonyesha jinsi gani nchi ilivyo, na wanaume wako tayari kwenda extra mile kujihamisha, hawakuwa na chaguo zaidi ya kuondoka nchi ya mateso na shida
 
Duh! Hawa jamaa wana roho ngumu sana na hawakua na chakupoteza,wapewe kazi huko walipofikia maana wana moyo wa kujitoa na wapo tayari kufanya kazi yeyote ile kwa bidii na kwa kujitoa,

Good luck wapambanaji wa maisha,

Kwakumalizia,njia hiyo ya uzamiaji ni hatari sana kwa maisha yako.
 
Back
Top Bottom