Hakuna siku nili enjoy kiupenda mpira na kuipenda Yanga kama siku ile ya Yanga dhidi ya Belouizdad.
Siku hiyo nilikuwa safarini natokea Kilwa narudi zangu Dar nikapanda gari ila hesabu zangu akilini nawaza nisijekuikosa hii mechi haijalishi matokeo yatakuwaje. Ikiwa kufungwa nijue tumefungwaje kwa uzembe au kwa kuzidiwa eneo gani, basi nikawa nashauku ya kuona mechi. Gari likaanza kuzingua njiani basi mimi kazi yangu kuangalia muda tu maana nilipiga hesabu hadi saa kumi na mbili nitakuwa mbagara. Lile gari liliharibika likabidi tutembee mdogo mdogo sana hadi kufika Kimanzi Chana ndipo wakaegesha pembeni kurekebisha nacheck muda ilikuwa saa kumbi na mbili. Jamaa wakaangaika nalo nikawaza kweli nakosa hii mechi hivi hivi. Basi kufika saa kumi na mbili na dakika kama 25 hivi gari likaa sawa tukaendelea na safari huku nacheck muda tu kila mara. Tunafika Kisemvule saa moja kasoro dakika 10. Aisee nikasema msinitanie nikaomba kushushwa hapo hapo Kisemvule.
Nikashuka kisha nikaanza kutafuta sehemu ya kuangalia mpira iliyokuwa nzuri na kuna nafasi nikatembea tembea ndani ndani mara tu naona ukumbi huu hapa wa mpira. Niakazama ndani ni ukumbi mkubwa mno nafasi ya kutosha kabisa nikapata siti nikakaa. Baadae wakaja warembo pembeni yangu tukawa tunaangalia game. Lilipo ingia goli la kwanza kutoka kwa Mudathir aisee liliamka shangwe sio mchezo. Goli la tatu linaingia kuna mdada katika kushangilia kwake kajikuta kanikumbatia pasipo kutarajia hanijui nami simjui ila ule mzuka kashindwa kujizuia. Aisee baada ya akili kukaa sawa nikaingiwa na wasiwasi sana maana nipo ugenini ikabidi kidogo nisogee kidogo mbali nae nisijekutwa na hatia. Siku ile nilikuwa na furaha mno baada ya mechi nikapanda gari huku moyo ukisema sikujutia kushukia njiani ili niwe moja wa mashuhuda wa hiki kilichotokea.