Piga ua, mradi wa JKN Power Plant (Stiegler's Gorge) lazima ukamilike

Piga ua, mradi wa JKN Power Plant (Stiegler's Gorge) lazima ukamilike

Uko sahihi sana, je kipaombele kwa sasa ni umeme tu? Ingekuwa ni kwa fedha zetu wenyewe hapo sawa, lakini za mkopo sioni kama ni sawa. Kwani hizo 2,115mg hatuwezi kufanya biashara ya umeme, au kuna kiwango tunatakiwa tupeleke kwenye hilo soko la umeme hivyo tutakuwa na mzigo mdogo? Toka nje ya box unaingizwa mjini boss.
Nakuelewa vizuri sana mkuu. Ila kila serikali iliyopo madarakani ina stategy zake ( kwa lugha ingine ina vipaumbele vyake ), maana sie sio kama marekani au baadhi ya nchi zenye mifumo ya kusimamia policy flani. Sie kiongozi yoyote ane ingie madarakani anafanya kile anacho ona yeye kwa wakati huo kwamba ni bora. Katika yale anayo amin Rais wa sasa kafanya vyema. Shida inakuja katika yale yasio kipaumbele chake ndio watu wanapata ukakasi, ila hawezi fanya kila kitu, atakuja mwingine nae anaweza wekeza zaidi kwa watu. Na ndio maana maanambiwa mchawi katiba
 
Kitu cha kushangaza pamoja na fly over foleni bado zipo mandela road nilitegemea kitu hiki kingefutika kabisa au sijui ni hila au nini?
 
Kama TANESCO wana mazonge na tumeridhika, una uhakika gani hiyo SG haitakuwa na mazonge? Au ndio haya haya ya kufufua shirika la ndege lililokuwa limekufa, lakini mahesabu ya ndege hizi ni siri hayakaguliwi? Mkuu kuwa makini maana unacheza ngoma usiyoijua.
Mkuu ukiwa pessimist always, nothing will be done kwa kuogopa kupigwa.
 
Kama TANESCO wana mazonge na tumeridhika, una uhakika gani hiyo SG haitakuwa na mazonge? Au ndio haya haya ya kufufua shirika la ndege lililokuwa limekufa, lakini mahesabu ya ndege hizi ni siri hayakaguliwi? Mkuu kuwa makini maana unacheza ngoma usiyoijua.
Kama mtu mwenye busara nilitegemea uhoji ni lini Atcl itapata faida? Je kweli hili shirika lina tija kwa watanzania? Sio kubwabwaja milawama tu
 
Kama mtu mwenye busara nilitegemea uhoji ni lini Atcl itapata faida? Je kweli hili shirika lina tija kwa watanzania? Sio kubwabwaja milawama tu

Nimecheka kwa nguvu hiki ulichoongea hapa, nahoji lini ATCL itaanza kupata faida, kwani hata taarifa za mapato yake ziko wazi? Shirika linaweza kuwa na tija ama, ila kwangu naangalia kipaombele zaidi, je hizo ndege zilikuwa ni kipaombele kwa sasa? Halafu hili la ndege sio mada husika bali nilichomeka tu kwenye post yangu kama mfano halisi.
 
Sio kwa uendeshaji wa makampuni ya serikali upuuzi ni mwingi sana. Hiyo pesa tunapoteza bure maana najua tu mradi utakamilika ila utaanza ufala katika uendeshaji.

Kuna yale mazee mapigaji yatachukua siti utanambia kama kuna kitu kitaenda.

Kwani shirika la ndege ATCL si hilo hapo tazama linavyoendeshwa kiboya na watu wanaojinasibu kuwa na experience plus ma phd na masters za kitaaluma.

Wastage of our time and money plus resources.......
 
Nimecheka kwa nguvu hiki ulichoongea hapa, nahoji lini ATCL itaanza kupata faida, kwani hata taarifa za mapato yake ziko wazi? Shirika linaweza kuwa na tija ama, ila kwangu naangalia kipaombele zaidi, je hizo ndege zilikuwa ni kipaombele kwa sasa? Halafu hili la ndege sio mada husika bali nilichomeka tu kwenye post yangu kama mfano halisi.
Unasikitisha sana, yaani mapato ya Atcl yanafichwa kibindoni? Kujua kuwa Atcl ina manufaa kwa umma napo kunahitaji kitu cha ziada?
Screenshot_20210213-161434.png
 
Unasikitisha sana, yaani mapato ya Atcl yanafichwa kibindoni? Kujua kuwa Atcl ina manufaa kwa umma napo kunahitaji kitu cha ziada? View attachment 1701504

Acha tu nicheke, kwa bahati mbaya ww ndio unaamini hizo taarifa ndio maana tuko 2021 unaleta taarifa za 2019, mimi naangalia uhalisia na sio hizo taarifa za kupika. Kama watu wanaficha waziwazi taarifa za ugonjwa wa Covid ambao sio wa kuficha, unapaswa kuwa mwendawazimu kuamini taarifa za hivyo.
 
Mbona kama hamjiamini tena au ndio kutuandaa kisaikolojia pale ambapo hautakamilika.
Wewe kama ni mtanzania, usitumie neno hamjiamini! Maana na wewe ni pamoja na kila mtanzania kuhusiana na mradi huu. Uwe una uunga mkono au unaupinga, ulipofikia hapa na wewe unashiriki! Huwezi kujitenga, mpaka sasa wewe umetumia hela nyingi kwenye huu mradi. Ukihamia kenya, ubelgiji au Canada, hapo ruksa kujitenga na huu mradi - vinginevyo unausuport 100 kwa 100!
 
Acha tu nicheke, kwa bahati mbaya ww ndio unaamini hizo taarifa ndio maana tuko 2021 unaleta taarifa za 2019, mimi naangalia uhalisia na sio hizo taarifa za kupika. Kama watu wanaficha waziwazi taarifa za ugonjwa wa Covid ambao sio wa kuficha, unapaswa kuwa mwendawazimu kuamini taarifa za hivyo.
Mimi kuweka taarifa za 2019 sio kwamba nipo outdated. Nipe kupa fact kuwa taarifa hazifichwi. Kuhusu Covid hapo kuna utata. Ila mficha ugonjwa huumbuka.
 
Am not a fan of Magufuli, lakini SGR na Stieglers ni miradi mkakati ambayo itatupeleka mbali. Leo wengi hawataona lakini hizi project mbili ni critical kuelekea 2050
Ni kweli mkuu hatuwezi kujenga miundombinu ya maendeleo kwa wasiwasi wa watu.
Hii project italeta maendeleo kwa muda mrefu ujao.
 
Binadamu tuna maneno sana. Lakini kati ya vitu vyote, Magufuli atakumbukwa kwa vizazi vingi vikavyo kwa kutekeleza mradi wa Umeme wa JK Nyerere Power plant kule Stieglers Gorge.

Huu mradi kiuchumi ni game changer.

Umeme rahisi utapunguza sana gharama za uzalishaji na hata kimaisha kwa matumizi ya nyumbani.

Kwa hili, kongole kwa Prsidetz. Magufuli.
Kwa Tanzania ninayo ifahamu tunaweza kuwa na umeme wa uhakika ila siyo bei kushuka
 
Am not a fan of Magufuli, lakini SGR na Stieglers ni miradi mkakati ambayo itatupeleka mbali. Leo wengi hawataona lakini hizi project mbili ni critical kuelekea 2050

..SGR itafanikiwa ikiwa kutakuwa na MIZIGO ya kutosha. Kumbuka tunayo reli ya Tazara lakini inaendeshwa kwa hasara. Na Tazara ilijengwa kwa mkopo nafuu kuliko mikopo ya SGR.

..Stieglers itakuwa na faida kama mkopo tuliyochukua ina masharti nafuu kwetu. Kama mkopo tuliochukua kujenga Stieglers una masharti mabaya basi umeme wa Stieglers utakuwa ghali. Pia kuna suala la MAZINGIRA bado hajutui bwawa hilo litatuletea changamoto gani za mazingira.
 
Nakubaliana na wewe kuhusu SGR.... ila TAZARA tuliua wenyewe kwa tamaa zetu. Time will tell kuhusu SGR lakini kama ikisimamiwa vizuri itatuletea faida. Stieglers vivyo hivyo, kama tukiweza kuhama kutoka kwenye gesi nina uhakika hata mkopo unaweza kulipwa na makusanyo tu. Kila kitu ni jinsi tutakvyokiendesha.
 
Ukiona sehem Kuna mafanikio ujue kuna watu waliumia, tukaze buti tumsapoti Rais Magufuli faida watakuja kutumia hata wajukuu zetu.

Maendeleo hayana vyama!!!
 
Nakumbuka kipind cha JK wapiga matarumbeta Kama nyie mlituaminisha kuwa umeme wa gesi toka kusini ndio siliuhisho la umeme Tanzania

Mkaptisha mikataba bungeni fastafasta bila kuwepo na muda wakujadili kwa kina ilikuwa kila mtu aliye katka mamlaka Kama prof Muhongo na wengineo kuwa Sasa nchi inaelekea kwenye utajir lakn had leo hatujui nn kilitokea

Leo mnakuja na ngonjera zile zile kwamba umeme wa maji ndyo mkombozi wa umeme Tanzania sijui nimuamin nani

Nilichojifunza hapa hii mirad n madil ya watu ili upige pesa isiyo na makele lazma ubuni mrad ambao utapata gawio lako

Atakuja Rais mwingne atapiga chini mrad huu atanzzisha mrad wa upepo mkubwa na kujinad ndio suluhisho kwan upepo haujawah Isha Kama mvua huwa znakata kabisa wakat mwingne lakn upepo upo tu
Na hawatakosekana akina KEMIKALI ALI wa bongo. Watakao sapoti hili

Nikuulize mleta mada labda upo upande gan katka hili
 
Back
Top Bottom