Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Nimakupa like. Hawa jamaa kama wana moyo mzuri, hawajui kuzika ni ibada, mbona hawaendi kusomba miili isiyo na ndugu mochwari wakazike.
 
Sijawahi kuona waislam wanamsusia marehemu. Wana ushirikiano sana kwenye misiba, taarifa zikitolewa chaap wamefika shughuli inaanza.
Utaskia tu Inalillahi wa inailahi rajiun, Mungu amjalie mapumziko mema inshaallah yani fasta tu mtu analamba udongo.
 
Hakuwa na pesa. Kama anapesa maaskofu wangaligombea mwili kuuombea. Au nasema uongo wadau?

KANISA KATOLIKI LAGOMA KUMZIKA BILIONEA MREMA

Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha jana lilikataa kuendesha misa ya mazishi kwaajili ya marehemu Faustine Mrema, mmiliki wa hotel za Ngurdoto, Impala na Naura springs kwavile hakuwa na sakramenti ya ndoa na mke wake wala kipaimara.

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mt. Theresia, Mtoto Yesu, Jimbo Kuu la Arusha, Padri Festus Mangwingi amethibitisha hilo na kusema marehemu hakuweka heshima kwa kanisa.

"Marehemu ni mkatoliki wa kuzaliwa lakini hakuwahi kuwa na sakramenti ya ndoa na mke wake aliyezaa nae watoto wala kupata kipaimara hivyo kanisa haliwezi kabisa kumzika. Kwa kawaida, mazishi ya Kanisa Katoliki hutolewa tu kwa mkristu anayestahili. Huyu marehemu hakuwahi kufunga ndoa kanisani na alijitenga na kanisa. Hivyo kusema Kanisa limemtenga si kweli kwani yeye ndiye alilitenga kanisa, hakutaka kuonesha heshima yake kwa kanisa kama mkristu. Aidha, marehemu hakuwahi kuhudhuria misa za jumuiya ambazo ni muhimu kwa Mkristu. Jumuiya ni utaratibu wa Kanisa unaowataka waumini wawe na usharika wa karibu na kufahamiana. Marehemu alikuwa hashiriki kabisa kwenye jumuiya sasa unaanzaje kumzika mtu kama huyo kwa heshima za Kanisa Katoliki?" alihoji padri Mangwingi.

Baada ya Kanisa hilo kujivua, ilibidi Askofu Dr. Eliud Issangya wa Kanisa la Kimataifa la Kiinjili kuokoa jahazi na akaendesha ibada hiyo ya mazishi iliyofanyika hoteli ya Ngurdoto, wilaya ya Arumeru, Arusha.
 
Sijawahi kuona waislam wanamsusia marehemu. Wana ushirikiano sana kwenye misiba, taarifa zikitolewa chaap wamefika shughuli inaanza.
Mbona mochwari miili mingi tu haina ndugu hao waislam hawaendi kuibeba wakaizike kwa ibada? Unadhani kuzika ni kitu chepesi sana?
 
Ni sahihi, warudishwe kundini. Hususani viongozi.
 
Ona hii ilichoandika
 
Hapa ndio dini yangu huwa inanichosha kabisa!

Hata wakatae kumsalia, what difference does it make to a dead man?🧟‍♂️ AbsoFREAKINGlutely NONE!!!!
Dead man wangapi umeenda kuwazika, ambao hata huwafahamu? Unadhani kanisa ni tofauti?
 
Hakuna Dola na Taasisi ya Kidkteta hapa ulimwenguni kama Kanisa Katoliki na Vatican[holy see] kwa ujumla.

Hivi, taasisi inayohimiza Uhuru wa Maoni and yet inaadhibu wenye maoni tofauti nayo, is it not dictatorial in it's own form!?

Ajabu Kanisa hili hili, linataka Mashoga wabarikiwe, in spirit ya kukumbatia tofauti zetu.

Organized religions zote ni shida zinapigania zaidi maslahi ya taasis and not an expected prime role ya kulea watu kiroho.
 
Katika eneo Uislam nina usifu ni Mazishi. Yeyote mwenye elimu na ujuzi wa kusalia maiti, anazika. Hii mambo ya kuweka taratibu kuwa hadi kiongozi, ni kutumia mwanya huu kuweka mambo ambayo sio ya kiimani kabisa kwa waumini. Yaani kanisa haliziki Muumini wake, kwa sababu ya utofauti wa mitazamo ya Kisiasa. Thadei anaadhibiwa na Kanisa kwa mambo ya Kaisari na Sio Mungu.
 
Kuna msiba uliokuwa na hela kama wa Ruge Mutahaba kwa siku za hivi karibuni? Muulize ndugu yake yeyote kama alizikwa kikatoliki. Ukiishi bila ndoa umejitenga na Kanisa, utazikwa na wahuni
Ruge Mutahaba ni cha mtoto, bilionea Mrema wa Arusha, pamoja na ubilonea wake hakuzikwa na kanisa Katoliki. Usicheze na Kanisa Katoliki katika kufuata taratibu zake.
 
Mbona mochwari miili mingi tu haina ndugu hao waislam hawaendi kuibeba wakaizike kwa ibada? Unadhani kuzika ni kitu chepesi sana?
Katika uislam kuzika ni Sanda tu tena kitambaa chepesi hakizi elf 20, kumsalia bure na kumzika bure. Hao waliokuwa munchuwari waislam labda uongozi wa hospital hawajatoa tu Taarifa kwa uongozi wa msikiti uliokaribu dakika miili yote itazikwa kiislam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…