Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Kanisa Katoliki lagoma kuendesha Ibada ya misa ya mazishi ya Thadei Ole Mushi kwa sababu ALIPINGA WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.

Thadei Ole Mushi alipinga hadharani waraka wa TEC, kupitia andiko lake la tarehe 18 August 2023 lenye kichwa cha Habari "WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA"

Juzi ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangazia dunia kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yetu Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.

Lakini watu wengi ikiwemo mimi tulipofika kanisa la St. Peter's Oysterbay, tulikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.

Uamuzi wa haraka kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.

Leo familia imekwaa tena kisiki kingine Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu kugomea kuendesha mazishi na kufunga milango kiasi cha kupelekea kutafutwa kwa wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.

Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.

Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Hili ni Somo kubwa na funzo kwa wanasiasa na watu wote ambao tulikuwa hatujui uzito na maana ya waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao hutolewa na kusomwa makanisa yote ya waumini wao.

Kama na wewe ni muuumini wa kanisa katoliki na unajua uliropoka na kupinga lolote kuhusu waraka ule wa TEC fanya haraka urudishwe kundini.

VIJANA[emoji849]

Ila kuna mambo mengine yanashangaza sana kwani kuzikwa kikatoliki au kwa namna yoyote ile kutabadilisha nini?

Cha msingi mwili wake umestiliwa na kuzikwa hayo mengine hayana umuhimu wowote.

Ila hao wachungaji wa kikatoliki wana matatizo kwa hiyo wao wanataka kila mtu awaunge mkono jambo lao kwani hawajui kuwa kuna uhuru wa kuchagua?

Huo usomi wao ambao huwa mnawasifia uko wapi?

Aibu.
 
Sijawahi kuona waislam wanamsusia marehemu. Wana ushirikiano sana kwenye misiba, taarifa zikitolewa chaap wamefika shughuli inaanza.
Shetani na Malaika Gabriel waliwahi kugombania mwili wa Musa.

Hivyo fahamu Mwili wako utawekwa upande uliouchagua.

Mf. Kuna vijana wanajiita wadudu na ukiwa kundi hilo watakuzika.

Ukijiandaa kwa mazishi ya Kikristo, Ishi Kikristo.
 
Ila kuna mambo mengine yanashanga sana kwani kuzikwa kikatoliki au kwa namna yoyote ile kutabadilisha nini?

Cha msingi mwili wake umestiliwa na kuzikwa hayo mengine hayana umuhimu wowote.

Ila hao wachungaji wa kikatoliki wana matatizo kwa hiyo wao wanataka kila mtu awaunge mkono jambo lao kwani hawajui kuwa kuna uhuru wa kuchagua?

Huo usomi wao ambao huwa mnawasifia uko wapi?

Aibu.
Sasa mnalialia Nini kama Haina maana kaeni kimya mzikeni mtu wenu.

Kama unaona mafundisho ya Kanisa hayakufai acha taratibu zake Zote.
 
Haya sasa wakatoliki kazi mnayo, mwenzenu kawapinga TEC tu kakataliwa ibada ya mazishi je nyinyi mnaompinga papa kuhusu ushoga mkifa si ndio mtalaaniwa kabisa na wenzenu. Wakatoliki achieni marinda hayo mbomoane hakuna namna papa keshanogewa.
 
Shetani na Malaika Gabriel waliwahi kugombania mwili wa Musa.

Hivyo fahamu Mwili wako utawekwa upande uliouchagua.

Mf. Kuna vijana wanajiita wadudu na ukiwa kundi hilo watakuzika.

Ukijiandaa kwa mazishi ya Kikristo, Ishi Kikristo.

Kuzikwa ni kuzikwa tu hata ukitupwa.

Ukizikwa kikristo ama kiislam hakuna kitachoongeza mwili wako utaoza na kubaki mifupa na kututengenezea rutuba udongoni.
 
Rc wamejaa ubaguzi sana.
Waumini makapuku wanazikwa na Katekista ama Mwenyekiti wa jumuia.
Akiwa na uwezo kidogo ama anafahamika basi atakuja Padre,
Akipanda kidogo basi anakuja Paroko
Ukiwa maarufu sana ama tajiri mkubwa atakuja Askofu tena bila maswali maswali..hata kama ukiwa na wake wengi wanakuzika.
Hii dunia hiii mmmmh
Umeandika Uongo na unaujutia.
 
Ooh jamani mimi mkatoliki ila hapa hawajafanya vizuri.Kutokumfanyia mtu ibada kisa mtizamo wa kidunia,ingekuwa amefia kwa hawara,au kujiua au ushoga nk hapo sawa.Maaskofu jamani muogopeni Mungu!Mlitakiwa mliposikikia yupo mahututi nyie ndio muwe wa kwanza kumuungamisha dhambi zake,na sio kusubiria afe msuse maiti mtaenda kujibu nini huko mbele ya haki?
 
Japo sikuwa nakubaliana kuuzwa kwa bandari, lakini kwani mtu haruhusiwi kuwa na mawazo huru?
Wapo wengi waliounga mkono uuzwaji wa bandari na ni Wakatoliki, lakini walitoa hoja zao bila kufanya rejea kwa Waraka wa TEC, hiyo Haina shida. Unapoamua kufanya Waraka wa TEC kama reference ya kupingana nao, maana yake unapingana na Waraka wa kichungaji, wakati ungeweza tu kuuunga mkono bila kuupinga Waraka. Kupingana na mafundisho ya Kanisa ni kutokubali kuwa mtiifu wa Kanisa, na hapo hautengwi, ila unajitenga mwenyewe maana hakuna aliyekutuma
 
Sasa mnalialia Nini kama Haina maana kaeni kimya mzikeni mtu wenu.

Kama unaona mafundisho ya Kanisa hayakufai acha taratibu zake Zote.

Nani analia Kirchhoff?

Naelezea ujinga ambao kanisa lenu limekumbatia.

Nyie endeleeni kubariki ushoga maana ndo kazi mnayoiweza.

Hizo PhD za falsafa na Theology kwa hao mapadri wenu bado sioni umuhimu wake kama bado wako na akili ambazo ni primitive kama hizo..
 
Hapa ndio dini yangu huwa inanichosha kabisa!

Hata wakatae kumsalia, what difference does it make to a dead man?[emoji3446] AbsoFREAKINGlutely NONE!!!!
Na kwa nini unafikiri watu huenda kuswaliwa??
 
Ikiwa kweli TEC wamefanya uamuzi kama mtoa mada alivyowasilisha basi haikuwa haki,mmketaa kumzika mtu kisa mtizamo wake kwenye mambo ya kidunia(siasa).Na ikiwa sio kweli watoe ufafanuzi kuondoa ukakasi kati ya waumini.Nimemuonea huruma Thadei maana kila mmoja ana haki ya kuagwa kutokana na dini yake aliyoiamini wakati akiwa hai unless aliikana au kukiuka sheria za kidini zilizowekwa
 
Rc wamejaa ubaguzi sana.
Waumini makapuku wanazikwa na Katekista ama Mwenyekiti wa jumuia.
Akiwa na uwezo kidogo ama anafahamika basi atakuja Padre,
Akipanda kidogo basi anakuja Paroko
Ukiwa maarufu sana ama tajiri mkubwa atakuja Askofu tena bila maswali maswali..hata kama ukiwa na wake wengi wanakuzika.
Hii dunia hiii mmmmh
Wewe sio RC na hujui chochote kuhusu taratibu za Kanisa. Ibada yoyote iliyopewa idhini na Paroko ni ibada halali hata kama itaendeshwa na Katekista. Ibada yoyote iliyozuiwa na Paroko haiwezi kuendeshwa na mtu yeyote ndani ya Parokia, awe Katekista, Padri wa nje ya Parokia, Askofu na hata Papa
Ukiona katekista anaendesha ibada, hiyo ni halali kabisa, maana mapadri huwa ni wachache na mambo ya kuhudumia ni mengi sana hadi huwa tunawaonea huruma
 
Hapo ni kupinga maaskofu tu, bado kwa waliompinga papa. vijana turudi tu kundini tuliojitia kumpinga papa. hapa hakuna namna kwa kweli.
 
Ila kuna mambo mengine yanashangaza sana kwani kuzikwa kikatoliki au kwa namna yoyote ile kutabadilisha nini?

Cha msingi mwili wake umestiliwa na kuzikwa hayo mengine hayana umuhimu wowote.

Ila hao wachungaji wa kikatoliki wana matatizo kwa hiyo wao wanataka kila mtu awaunge mkono jambo lao kwani hawajui kuwa kuna uhuru wa kuchagua?

Huo usomi wao ambao huwa mnawasifia uko wapi?

Aibu.
Na ndo shetani anaependa haya Maneno na ushawishi wako

Soma Kitabu Cha Yakobo.
 
Ikiwa kweli TEC wamefanya uamuzi kama mtoa mada alivyowasilisha basi haikuwa haki,mmketaa kumzika mtu kisa mtizamo wake kwenye mambo ya kidunia(siasa).Na ikiwa sio kweli watoe ufafanuzi kuondoa ukakasi kati ya waumini.Nimemuonea huruma Thadei maana kila mmoja ana haki ya kuagwa kutokana na dini yake aliyoiamini wakati akiwa hai unless aliikana au kukiuka sheria za kidini zilizowekwa
TEC hawawezi kujishughulisha na ishu ndogo hivyo, acha kuishusha hadhi. Hilo ni suala la Paroko tu, inawezekana hata sio waraka, sakramenti za Ole Mushi hazizungumziwi hapa. Inawezekana alikuwa anaishi na mwanamke bila ndoa
 
DP world walituma muwakilishi au walituma japo ka ubani kwa MTU wao?
 
Hii article imeandikwa kichochezi.Wengi walipinga ule waraka lkn hii haujawahi kuwa sababu ya wao kutengwa na kabisa.Kanisa Katoliki ni tooo liberal na linaamini katika hoja ndo maana waamini wake wako huru kuchangua aina ya maisha wayatakayo.

Ni kweli Kanisa halishiriki mazishi ya mtu ambaye alikua hashiriki katika mambo ya kanisa ikiwemo kuhudhuria Ibada. Hii ni sahihi kabisa.Mtu ana Uhuru wa kuchagua aishije na akifa tutatumia aina ya maisha yake kuamua alitaka azikweje (Mode of life test). Aliamua kutoshiriki na kanisa hence sio busara kumpeleka kanisani wakati kafa mtakua mmemtemdea marehemu kinyume na matakwa yake.
 
Back
Top Bottom