Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

PIGO LA MWISHO KWA THADEI OLE MUSHI.

Kanisa Katoliki lagoma kuendesha Ibada ya misa ya mazishi ya Thadei Ole Mushi kwa sababu ALIPINGA WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.

Thadei Ole Mushi alipinga hadharani waraka wa TEC, kupitia andiko lake la tarehe 18 August 2023 lenye kichwa cha Habari "WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA"

Juzi ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangazia dunia kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yetu Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.

Lakini watu wengi ikiwemo mimi tulipofika kanisa la St. Peter's Oysterbay, tulikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.

Uamuzi wa haraka kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.

Leo familia imekwaa tena kisiki kingine Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu kugomea kuendesha mazishi na kufunga milango kiasi cha kupelekea kutafutwa kwa wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.

Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.

Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Hili ni Somo kubwa na funzo kwa wanasiasa na watu wote ambao tulikuwa hatujui uzito na maana ya waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao hutolewa na kusomwa makanisa yote ya waumini wao.

Kama na wewe ni muuumini wa kanisa katoliki na unajua uliropoka na kupinga lolote kuhusu waraka ule wa TEC fanya haraka urudishwe kundini.
 
Hii article imeandikwa kichochezi. Wengi walipinga ule waraka lkn hii haujawahi kuwa sababu ya wao kutengwa na kanisa.
Aliamua kutoshiriki na kanisa hence sio busara kumpeleka kanisani wakati kafa mtakua mmemtemdea marehemu kinyume na matakwa yake.
Natamani watu wote wanaopitia uzi huu wasome hiyo mistari ya hii post.
 
Kwani kutoendesha ibada ya mazishi ndio kuhukumu? Kuna kitu hamuelewi hapa. Kanisa Katoliki hutoa huduma za kiroho kwa Wakatoliki tu. Kwa mujibu wa taratibu za kiroho, Ole Mushi hakuwa Mkatoliki
Alikuwa Mkatoliki kamili na alishiriki kila kitu,kosa lake kubwa ni kupinga maazimio na mafundisho ya kanisa kupitia ule waraka wake.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Ibada za mazishi huwa hazibadili makao ya marehemu huko aendako, bali hukumbusha tu walio hai kujiandaa na hiyo safari.

Isitoshe, hakuna uthibitosho unaohalalisha hizi imani zetu kuwa ni za kweli au tu ni mambo yaliyobuniwa ili watu waweze kuishi wakiwa no hofu fulani kulikoni kama tungeishi bila ya hofu hiyo(maovu yangekuwa mengi sana hapa duniani).
 
Hii article imeandikwa kichochezi. Wengi walipinga ule waraka lkn hii haujawahi kuwa sababu ya wao kutengwa na kanisa.
Aliamua kutoshiriki na kanisa hence sio busara kumpeleka kanisani wakati kafa mtakua mmemtemdea marehemu kinyume na matakwa yake.
Natamani watu wote wanaopitia uzi huu wasome hiyo mistari ya hii post.
 
Mbona mochwari miili mingi tu haina ndugu hao waislam hawaendi kuibeba wakaizike kwa ibada? Unadhani kuzika ni kitu chepesi sana?
Sasa wenyewe wanajuaje kuna miili ambayo haina ndugu huko? Na wanajuaje ni wenzao katika imani?

Hawa wenzetu wakipewa taarifa tu fulani alikuwa ni mwenzetu amefariki, hawachukui muda wameshajaa na taratibu zinaanza hata kama huyo mtu haendagi msikitini.

Mtaani kwetu kuna dogo alibadili dini na kuwa muislam akiwa shuleni. Hata familia haikuwa na Idea, hata mtaani hamna aliyejua. Alivyofariki tu , kanisa likagoma wakasema huyo kijana hayupo kundini maana alikuwa ahudhurii ibada.

Kama bahati aliyesoma na huyo mtoto akachana mkeka kwamba “fulani alibadili dini tukiwa shuleni na anaitwa AbdulKarim”. Wazazi wakiwa wanaendelea kushangaa wenye AbdulKarim wao wakapata taarifa wakafika chaaap. Masaa kadhaa mbele dogo ameshazikwa shughuli imeisha.
 
Kanisa Katoliki lagoma kuendesha Ibada ya misa ya mazishi ya Thadei Ole Mushi kwa sababu ALIPINGA WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.

Thadei Ole Mushi alipinga hadharani waraka wa TEC, kupitia andiko lake la tarehe 18 August 2023 lenye kichwa cha Habari "WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA"

Juzi ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangazia dunia kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yetu Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.

Lakini watu wengi ikiwemo mimi tulipofika kanisa la St. Peter's Oysterbay, tulikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.

Uamuzi wa haraka kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.

Leo familia imekwaa tena kisiki kingine Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu kugomea kuendesha mazishi na kufunga milango kiasi cha kupelekea kutafutwa kwa wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.

Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.

Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Hili ni Somo kubwa na funzo kwa wanasiasa na watu wote ambao tulikuwa hatujui uzito na maana ya waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao hutolewa na kusomwa makanisa yote ya waumini wao.

Kama na wewe ni muuumini wa kanisa katoliki na unajua uliropoka na kupinga lolote kuhusu waraka ule wa TEC fanya haraka urudishwe kundini.

VIJANA🙄
Hawa jamaa ni wanafiki waziri wasingemzika kisa aliwapinga?
 
Najua imekugusa mkuu. Huwezi kubadilisha taratibu na sheria za kanisa. Watu wanasomea na kupata Shahada ya uzamivu kwenye sheria za kanisa (Canon law) eg Askofu Henry Mchamungu.

Ikiwa mfalme Henle wa pili wa Uingereza miaka hiyo aliliomba kanisa limruhusu kuoa mke wa pili ili apate mtoto wa kiume kwa ajili ya urithi wa kifalme, lakini kanisa Katoliki lilimkatalia na akaanzisha kanisa lake la Church of England/ Anglican na bado kanisa Katoliki halikutishika mpaka leo taratibu ni zile zile. Wewe ni nani ?
 
Ni kweli mkuu kanisa Katoliki hailimtengi mtu ila halilazimishi mtu kulifuata. Kama alijitenga akiwa hai, kwa nini kanisa limlazimishe akiwa ameshakufa na bila kujua sababu ya yeye kujitenga huko.

Suala la Waraka inaweza isiwe sababu ila maisha yake ya ukatoliki, ndoa n.k hatuyajui yanaweza kuwa ni sababu pia.

Wapo wengi mfano bilionea Mrema wa Arusha (Ngurudoto na Nauru Spring) nae hakupata ibada ya mazishi ya kanisa Katoliki. Nyie mnaosema haina umuhimu wowote kwa nini mnalalamika na kuleta uzi?

Ile ni Ibada/ Misa ya kuonesha ushindi katika kuiishi imani katoliki (Ukristo) katika maisha yako hapa duniani. Kwamba "Nimevipiga vita vilivyo vizuri mwendo nimeumaliza na Imani nimeilinda."
Na hakuna mtu aliekuwa anazihudumia kwaya za Katoliki Arusha kama Bilionea Mrema,tangu amefariki kwa karibu zote zimefifia zikiongozwa na Kwaya ya Mt Theresa Unga Limited.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Ishu sio alikuwa anawapinga maaskofu kuhusu DPW, ni kwamba jamaa hakuwa na mchango chanya kwa kanisa hasa kwenye utoaji wa pesa. Hii kitu huwezi kuisikia kwa matajiri au viongozi wakubwa wa serikali mana hao hua wanatoa pesa au kuwapa upendeleo kwenye mambo yao kikanisa.
 
Sasa wenyewe wanajuaje kuna miili ambayo haina ndugu huko? Na wanajuaje ni wenzao katika imani?

Hawa wenzetu wakipewa taarifa tu fulani alikuwa ni mwenzetu amefariki, hawachukui muda wameshajaa na taratibu zinaanza hata kama huyo mtu haendagi msikitini.

Mtaani kwetu kuna dogo alibadili dini na kuwa muislam akiwa shuleni. Hata familia haikuwa na Idea, hata mtaani hamna aliyejua. Alivyofariki tu , kanisa likagoma wakasema huyo kijana hayupo kundini maana alikuwa ahudhurii ibada.

Kama bahati aliyesoma na huyo mtoto akachana mkeka kwamba “fulani alibadili dini tukiwa shuleni na anaitwa AbdulKarim”. Wazazi wakiwa wanaendelea kushangaa wenye AbdulKarim wao wakapata taarifa wakafika chaaap. Masaa kadhaa mbele dogo ameshazikwa shughuli imeisha.
Kama huwezi ku comply na taratibu za sehemu hamia kule kwingine unapoona unaweza kufuata taratibu zao, usilazimishe Kanisa Katoliki lifuate matakwa yako.
 
Back
Top Bottom