Pindi Chana: Nimesitisha usafirishaji wa wanyamapori mpaka nitakapopata taarifa kamili

Pindi Chana: Nimesitisha usafirishaji wa wanyamapori mpaka nitakapopata taarifa kamili

Serikali kukataza hii ni kuchochea ujangili tuu. Huwezi kuwaambia watu walale njaa wakati wanyama wa kuuza wapo. Ni akili finyu.
Sawa hakuna kuwauza badala yake vutia watalii waje kuwatazama. Mchukue Christiano apige picha na Pundamilia na Twiga. Uone kama watalii hawatakuja kuwatazama hao wanyama. Mchukue Ed Sheeran naye aje hivyohivyo.
 
Hizi issue zao ndio zinafanya wananchi wanakuwa na hasira sana!
Kuna haja gani ya kuuza wanyamapori hai nje ya nchi! ni kwamba tuna shida sana ya pesa au!!!
Kwa maslahi ya nani!?
Kisha utawasikia wanasema mama anachukiwa kwa sababu ya dini ....kweli CCM NI MAVII
 
Waziri wa Maliasili na utalii Mh Pindi Chana amesema kuna tangazo limekuwa likizunguka kwenye mitandao kuhusu usafirishaji wa wanyamapori ambalo lilizua taharuki toka jana !

Hivyo kwakuwa yeye ni Waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii ametangaza kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori na Maliasili mpaka hapo atakapopata taarifa kamili na kutoa maamuzi!

Kwa maelezo yangu haya hakuna tena usafirishaji wa wanyama pori hao kama jinsi ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo taasisi" amesisitiza Balozi Pindi Chana

View attachment 2251487

Chanzo: EATV

N:B Ni wazi ndani ya serikali hakuna mawasiliano kabisa hivi inawezekanaje waziri wa maliasili na utalii asiwe na taarifa na tangazo kubwa na nyeti kama lile?

Ni kweli waziri hakuwa na taarifa la na tangazo lile? Ni kweli waziri hakuambiwa kuhusu tangazo?
Hilo ni group la kaole
 
Mbowe na lissu wanahusikaje kwenye huo ujinga.jambo lifanywe na watu wengine lawama upeleke kwingine.maccm ndio wanaofuja mali za umma wao ndio wanaopaswa kuambiwa.Ata hivyo ni jukumu la kila mwananchi kupiga kelele pale anapoona rasiliamali za nchi zinatumika isivyopasa.Sasa wewe umefanya wajibu wako kiasi gani au unasubiri mbowe na lissu waseme kila kitu.Wewe ndio uanze kuamka.
Acha zako wewe
 
Kwamba alikuwa hana taarifa ?!!!!

Ni mangapi yanafanyika / yatafanyika bila yeye kuwa na taarifa ? kwahio hili lilipita / lilijadiliwa bila yeye kufahamu lolote ? Au kosa lililofanyika ni taarifa kutolewa badala ya kufanyika kimya kimya
 
Usimlaum waziri! Rais mzigo tena wa misumari! Ujuaji mwingi na kujifanya kuelimika kumbe wizi! Jiulize Kinana na kashifa za ujangili eti makamu mwenyekiti wa CCM! Hahahahah

Waziri Mzigo Yaani Shida Sana

Umemuona huyu jangili ndo mambo yote huyu! Hata huruma hata kidogo!
 
Wewe usiwe mburula,shida sio kuuza twiga na Wala sina tatizo hata wakiuzwa..

Swala ni kwa nini ionekane tangazo halina coordination ya serikali? Huu ni ujinga na utoto..

Serikali ilisitisha hiyo biashara kwa sababu ilizotaja sasa kama kuna sababu za kuanza kuuza wanyama hai kuna tatizo Gani ikiwa wanaona inafaa kufanya hivyo?

Huwezi kuwa serikali ya kuvizia kusikia watu watasemaje.
Wewe taahira si chwa wa masa 100! Kila siku kushangilia hata kama akijamba! Kwendra zako!
 
View attachment 2251418Waziri Chana ametoa kauli hiyo kufuatia taarifa zilizokuwa zinasambaa mitandaoni kuwa baadhi ya taasisi zimeanza kusafirisha wanyama hao kwenda nje ya nchi

Akizungumza na wanahabari Jijini Arusha Waziri Chana amesema zoezi la usafirishaji wa wanyama pori nchini limesitishwa mara moja hadi hapo serikali itakapopata taarifa rasmi na serikali kuamua vinginevyo

"Kwa maelezo yangu haya hakuna tena usafirishaji wa wanyama pori hao kama jinsi ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo taasisi" amesisitiza Balozi Pindi Chana
Nchi haina rais
 
Kwanza tambua anaitwa

PINDI na serikali sidhani Kama mawasiliano hayapo Ila ndo utaratibu wake kuleta Jambo jamii ikihamaki tu. Wanalikataa
 
AtaKuwa Alilipitisha bila kujiridhisha vya kutosha. Lazima Km wake anajua, Sana Sema ameona negative reaction kaamua kusitisha
Waziri wa Maliasili na utalii Mh Pindi Chana amesema kuna tangazo limekuwa likizunguka kwenye mitandao kuhusu usafirishaji wa wanyamapori ambalo lilizua taharuki toka jana !

Hivyo kwakuwa yeye ni Waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii ametangaza kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori na Maliasili mpaka hapo atakapopata taarifa kamili na kutoa maamuzi!

Kwa maelezo yangu haya hakuna tena usafirishaji wa wanyama pori hao kama jinsi ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo taasisi" amesisitiza Balozi Pindi Chana

View attachment 2251487

Chanzo: EATV

N:B Ni wazi ndani ya serikali hakuna mawasiliano kabisa hivi inawezekanaje waziri wa maliasili na utalii asiwe na taarifa na tangazo kubwa na nyeti kama lile?

Ni kweli waziri hakuwa na taarifa la na tangazo lile? Ni kweli waziri hakuambiwa kuhusu tangazo?
 
Waziri wa maliasili Chana Pinda akiongea kwa gadhabu kuzuia wanyama kusafirishwa nje ya nchi wakati tayari wanyama kibao wamekwisha safirishwa kimyakimya kwa haraka sana wameelekea Marekani na uarabuni.
Taarifa za kiintelijinsia zimethibitisha na muda si mrefu ushahidi tutauweka hadharani hapa jukwaani
 
Naona kama kuna picha tuna chezewa hapa, mlioko huko wanako pitishwa hawa wanyama muwe macho kutujuza na sisi wa vijijini ili tujue nini kinaendelea huko
Pigeni mawe hayo magari
 
Mijizi kweli alfu watu wanasema watalihi wamepungua Bila kutaja sababu za msingi

Alfu ajabu Zaid Ni kuwa taarifa hyo inatoka baada ya hutuba ya wizara yake kupitishwa bila hicho kipengele
 
Back
Top Bottom