Uchaguzi 2020 Pinga pinga wa ndege, Zitto Kabwe aumbuliwa na ndugu zake

Zitto kupanda ndege hakufanyi mimi na wewe tufikiri kuwa katika matatizo yote ya nchi hii, ndege ni muhimu. Hiyo ndege aliyopanda Zitto, ilimpelekea mama wa kijijini maji safi ya kunywa, ilimnunulia dawati mtoto ambaye hana dawati shuleni? Msituminishe kuwa lengo la ndege ni Zitto kupanda. Zitto akipanda basi Watanzania wote tumefaidika?
 
 
Kampuni ya Airbus huijui? Si ukawaulize hizo ndege wanauza shs ngapi?

Kweli hapo ufipa hata kuingia kwenye mtandao hamuwezi mpaka msubiri Magufuli awaambie?
Kwa hiyo awaulize Airbus bei ya ndege za Boeing? Upo sawa upstair??
 
Mkuu kwa IQ ndogo waliyo nayo watanzania CCM itatawala milele.wameshindwa kabisa kutafsiri nini bwana ZZk alikuwa anamaanisha
 
Jiwe bwaana! πŸ˜…, Leo amekopy na kupaste wimbo wa hadithi tuliyokuwa tunaasimuliwa na bibi yetu mmoja wa kiha:
Manju: Mningwa hanyelee, Mningwa hanyelee, Mningwa hanyelee!
Waitikiaji: Mningwa hanyelee, Mningwa hanyelee, Mningwa hanyelee!
Manju: Alisema ha...gii!
Waitikiaji: Mningwa hanyelee!
Manju: .. na Sasa ame....aa!

Waitikiaji: Mningwa hanyelee!
.
.
. TOO LOW! πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ’₯
 
Acheni ujinga..

Hilo bango hakuna mwananchi anaweza ligharamia..

Huyo ni meko mwenyewe kaprint kwa kodi za wananchi..

Mbinu za kizamani na mawazo ya kimaskini.

Bukoba hatufanyi huo Ujinga.
 
Umemuona rwanda anapasua anga kimataifa wewe unaruka kwenda wapi
 
Usikwepeshe, walisema hawataki maendeleo ya vitu. Wakataja ndege,madaraja si mabarabara, majengo ya hospitali na sgr.


Huo ni uongo mkubwa sana unaowazulia akina zitto, wao wanataka "KWANZA" maendeleo ya WATU halafu ndipo maendeleo ya vitu.

Wao na hata mimi na hata baba wa taifa tunataka kwanza maendeleo ya watu ndipo maendeleo ya vitu, maendeleo ya watu ni kama:- Uhuru na haki zao, Afya (huduma za afya bora, madaktari, vifaa tiba, madawa nk ), maji safi ya kunywya nk, lishe bora, watu waweze kujijengea makazi bora nk, mzunguko mzuri wa pesa, mazingira bora ya kufanya biashara, kilimo ufugaji nk, (kuondoa kodi gandamizi), wafanyakazi wa serikali wapewe haki zao zilizopo kisheria nk, uhuru wa watu kupata habari na kutoa habari kuhusu nchi yao, usalama wa watu na mali zao, wananchi wapewe nafasi kuchangia katika uchumi wa nchi na kuepukana na uchumi dola nk,--- hiyo ni baadhi ya maendeleo ya watu kwanza baadaye ndipo maendeleo ya vitu yaje.
 
Jibu trilioni 1.5 ziko wapi
 
Onesha malori yaliyowasomba hao watu
Na fiesta ya wasanii
 
Tanzania ndo nchi pekee duniani ambayo bado baadhi ya wananchi wake wanaamini mali za umma ni za raisi wao na ndiye mwenye mamlaka ya kuwapangia matumizi πŸ˜› πŸ˜› πŸ˜›
 
Kampuni ya Airbus huijui? Si ukawaulize hizo ndege wanauza shs ngapi?

Kweli hapo ufipa hata kuingia kwenye mtandao hamuwezi mpaka msubiri Magufuli awaambie?


Nyie watu wa Lumumba ni shida sana, mtu anafuja pesa yetu kununua vitu tusivyohitaji tunapo muuliza kulikoni mnatujibu; "nendeni dukani kuulliza bei ya hivyo vitu".

Hiyo ni sawa mtu atumie pesa yako kununulia pombe na ukimuuliza bei ya pombe aliyonunua anakuambia nenda kaulize bei kilabuni !! πŸ™‰--- nyie mmelewa madaraka kiasi kwamba mnadhani mnayo haki ya umiliki wa milele wa nchi hii, ipo siku mtajua tu kwamba watu tumechoka.
 
Hivi kwa akili yako ya kuvukia barabara,kuna mnyonge wa Tanzania mwenye uwezo wa kutengeneza Bango la aina hiyo?kumbuka;wastani wa kipato cha mtanzania kwa sasa ni USD 1080.00 kwa mwaka
 
Mmenunua ndege kinyume na sheria na ndege zenyewe zinalitia taifa hasara.
Kisha mkaua mashirika FAST JET na PRESICIONS AIR kwa hiyo mlitegemea Zitto asafiri na punda kwenda Kigoma? Magufuli hakika kaishiwa hoja, mnatengeneza bango Dar na kwenda nalo Kigoma ili mseme watu wa Kigoma wanamsuta Zitto? Utoto mtupu!
Subirini muondoje kisha mtashuhudia ya Kagera. Magufuli kuondoka tuu, mbunge kaitisha mkutano wa kutisha huku watu wakimkejeli magu na wasanii wake kuwa wamecheza muziki wa bure aende nao tena.
CCM mnakwama wapi kutumia akili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…