LGE2024 Pius Msekwa aeleza kutofurahia ushindi wa 99% wa CCM, asema anafurahia tu pale uchaguzi unapomalizika na pande zote zinaridhika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Wenye akili wote wanaona wazi njia tunayoelekea siyo nzuri na tusipokuwa makini tutaiingiza nchi kwenye majanga lakini cha ajabu kuna wapumbavu wachache hawalioni hilo!
 
Magufuli ndio muasisi wa hizi siasa chsfu za kutaka ccm ishinde kwa kishindo kitu kisichoendana na ukweli. Wamaccm wanaojitambua wanajua ukweli kuwa ccm iko madarkani kwa shuruti na sio kwa ridhaa ya walio wengi.
Hakika.
 
Naunga mkono hoja. Bora ushinde kihalali asilimia 51 kuliko kufanya ujambazi wa kura.
 
Katiba haina tatizo,tatizo lipo kwenye Tume ya Uchaguzi,Rais,Makamu wa Rais,Waziri Mkuu,Spika na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
 
Ukimsikiliza kwenye hii clip, mzee Msekwa ni muoga.

Kaulizwa swali kwamba "Jana waziri mkuu mstaafu, jaji Joseph Since Warioba amelaani tabia ya kuvitumia vyombo vya dola kwenye chaguzi. Kwann ccm mnatumia vyombo vya adola kwenye chaguzi?"

Majibu ya mzee Msekwa anasema yeye hajawahi kuviona vyombo vya dola vikitumika ktk chaguzi. Majibu haya yamejaa marashi ya uwoga.
 
Naunga mkono hoja. Bora ushinde kihalali asilimia 51 kuliko kufanya ujambazi wa kura.
Huwezi kuwapumbaza watu wote muda wote, Vile vile ujinga ni kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile halafu ukitegemea matokeo chanya ama kulazimisha watu wafikiri unavyotaka wewe hata kama una uwezo mdogo wa kufikiri
 
Safi sana mzee Msekwa! Wazee hawapaswi kukaa kimya huku mambo yakienda kombo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…