Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Pius Msekwa amesema hafurahii ushindi wa 99% wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika kwani kuna mapungufu mengi. Pia amesema mtu mwenye akili timamu hawezi kufurahia ushindi huo.
Spika mstaafu ameyasema hayo leo alipohojiwa na Sauti ya Kiswahili ya Ujerumani. Spika amevitaka vyombo vya uchaguzi kuondokana na kasoro ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu na kuwaengua wapinzani ambapo amesema hilo halikuwahi kutokea hapo zamani kwanini linatokea sana siku hizi? Amehoji Spika Mstaafu.
Absolutely, he's right...
CCM kuanzia waziri wao wa TAMISEMI (sijui nani yule vile, ooh yes, anaitwa Mchengerwa) akajitoa ufahamu, akatoka kwenye ujinga akaingia kwenye level ya upumbavu na bila soni wala aibu usoni mwake huku akijua kabisa kuwa anachokisema/kukitangaza ni uongo kwa 1000% akaamua kujitosa mwenyewe kwenye laana ya dhambi ya uongo utakaotafuna kizazi chake chote...
Pius Msekwa ingalau wewe umeamua kutokuwa mjinga katikati ya wana CCM wenzako na kuchukua uamuzi wa busara wa kukaa mbali na uovu na dhambi hiyo ya kupora/kudhulumu haki za watu ambayo mpende msipende itawatafuna ndugu zako, wana CCM wenzako, watoto wao na wajukuu zao wote hadi kizazi cha nne....
Hakika CCM wote si tu wajinga bali ujinga wao umefikia level ya upumbavu...!!
CCM furahini sasa, kuleni fedha hizo sasa lakini siku ya kulia na kusaga meno ipo inakuja upesi kwa kuwa mmeamua ku - invest kwenye uharibifu na uangamivu wenu wenyewe pamoja na Mungu wa mbinguni awapendae sana kutumia watu wengi na njia nyingi kuwaonyeni ili kuacha njia zenu mbaya na za uovu ili mtende na kuwatendea wengine kwa haki...
Lakini hamkusikia wala kujali. Kiburi cha uzima na madaraka ya kidunia kiliwapumbaza mkawa wajinga....
Kwa hiyo, nyie wenyewe kwa hiari zenu mmechagua kukimbilia mateso na uharibifu juu yenu wenyewe, watoto na wajukuu zenu pamoja na vyenu vyote....
Bado muda wa kurekebisha makosa yenu kwa TOBA YA KWELI upo. Mkipenda mnaweza kufanya sasa yaliyo sahihi before it's too late....
Lakini msipofanya hivyo sasa, Mungu atawapa sawasawa na mlichokitaka wenyewe na ndipo mtakapotambua kuwa, huyu Mungu - Yehova aliyetuumba ni Mungu wa HAKI na anachukia na kuadhibu dhuluma sawia....
Na ndiposa mtakapotambua kuwa kumbe yeye Mungu Jehovah ndiye atawalaye juu ya serikali za wanadamu wote duniani...!
Mkumbukeni mfalme Nebukadneza, Ahabu, Farao na wengine waliowahi kutawala falme zenye nguvu sana duniani lakini zilichonajisi HAKI na kutenda yaliyo maovu Mungu aliwafanya nini....
Bado tunasubiri kauli ya "Malkia" wenu, mwenyekiti wenu taifa wa CCM Bi Samia Suluhu Hassan...
Je, naye atajiunga kwenye ujinga na laana hii..??