LGE2024 Pius Msekwa aeleza kutofurahia ushindi wa 99% wa CCM, asema anafurahia tu pale uchaguzi unapomalizika na pande zote zinaridhika

LGE2024 Pius Msekwa aeleza kutofurahia ushindi wa 99% wa CCM, asema anafurahia tu pale uchaguzi unapomalizika na pande zote zinaridhika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Kipindi cha hawa wazee, CCM ilikuwa kwaajili ya maendeleo ya watanzania, lakini CCM ya sasa ni CCM ya mashetani, ambayo ipo kwaajili ya kuwaangamiza Watanzania.
Huyu akiwa spika si ndo Loliondo iliuzwa? Si ndo mikataba ya kifisadi kwenye umeme ilisainiwa? Wazee bora wangekaa kimya.
 
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Pius Msekwa amesema hafurahii ushindi wa 99% wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika kwani kuna mapungufu mengi. Pia amesema mtu mwenye akili timamu hawezi kufurahia ushindi huo.

Spika mstaafu ameyasema hayo leo alipohojiwa na Sauti ya Kiswahili ya Ujerumani. Spika amevitaka vyombo vya uchaguzi kuondokana na kasoro ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu na kuwaengua wapinzani ambapo amesema hilo halikuwahi kutokea hapo zamani kwanini linatokea sana siku hizi? Amehoji Spika Mstaafu.
Absolutely, he's right...

CCM kuanzia waziri wao wa TAMISEMI (sijui nani yule vile, ooh yes, anaitwa Mchengerwa) akajitoa ufahamu, akatoka kwenye ujinga akaingia kwenye level ya upumbavu na bila soni wala aibu usoni mwake huku akijua kabisa kuwa anachokisema/kukitangaza ni uongo kwa 1000% akaamua kujitosa mwenyewe kwenye laana ya dhambi ya uongo utakaotafuna kizazi chake chote...

Pius Msekwa ingalau wewe umeamua kutokuwa mjinga katikati ya wana CCM wenzako na kuchukua uamuzi wa busara wa kukaa mbali na uovu na dhambi hiyo ya kupora/kudhulumu haki za watu ambayo mpende msipende itawatafuna ndugu zako, wana CCM wenzako, watoto wao na wajukuu zao wote hadi kizazi cha nne....

Hakika CCM wote si tu wajinga bali ujinga wao umefikia level ya upumbavu...!!

CCM furahini sasa, kuleni fedha hizo sasa lakini siku ya kulia na kusaga meno ipo inakuja upesi kwa kuwa mmeamua ku - invest kwenye uharibifu na uangamivu wenu wenyewe pamoja na Mungu wa mbinguni awapendae sana kutumia watu wengi na njia nyingi kuwaonyeni ili kuacha njia zenu mbaya na za uovu ili mtende na kuwatendea wengine kwa haki...

Lakini hamkusikia wala kujali. Kiburi cha uzima na madaraka ya kidunia kiliwapumbaza mkawa wajinga....

Kwa hiyo, nyie wenyewe kwa hiari zenu mmechagua kukimbilia mateso na uharibifu juu yenu wenyewe, watoto na wajukuu zenu pamoja na vyenu vyote....

Bado muda wa kurekebisha makosa yenu kwa TOBA YA KWELI upo. Mkipenda mnaweza kufanya sasa yaliyo sahihi before it's too late....

Lakini msipofanya hivyo sasa, Mungu atawapa sawasawa na mlichokitaka wenyewe na ndipo mtakapotambua kuwa, huyu Mungu - Yehova aliyetuumba ni Mungu wa HAKI na anachukia na kuadhibu dhuluma sawia....

Na ndiposa mtakapotambua kuwa kumbe yeye Mungu Jehovah ndiye atawalaye juu ya serikali za wanadamu wote duniani...!

Mkumbukeni mfalme Nebukadneza, Ahabu, Farao na wengine waliowahi kutawala falme zenye nguvu sana duniani lakini zilichonajisi HAKI na kutenda yaliyo maovu Mungu aliwafanya nini....

Bado tunasubiri kauli ya "Malkia" wenu, mwenyekiti wenu taifa wa CCM Bi Samia Suluhu Hassan...

Je, naye atajiunga kwenye ujinga na laana hii..??
 
CCM walivyo watamtukana Msekwa hadi aingie upepo. Maana haya majitu ni ya hovyo sana hayana hata aibu kwa maovu wanayofanya
Kwani Msekwa anasema hii Katiba iliyopo imevunjwa wapi !
Kwani Katiba inasemaje kuhusu mambo ya Uchaguzi ??!!
Mimi naamini Mzee Msekwa anaijua vizuri hii Katiba na anajua kila kitu kilikwenda kwa mujibu wa Katiba !
Au nasema uongo ndugu zanguni ???!!!
😳🙄😳 !
 
Wasiishie kuchukizwa na. ushindi wa asilimia 99 wachukizwe na mbinu zilizotumika kuupata ushindi huo kwa kutumi kura fake.
 
Huyu akiwa spika si ndo Loliondo iliuzwa? Si ndo mikataba ya kifisadi kwenye umeme ilisainiwa? Wazee bora wangekaa kimya.
Kwani Katiba ilivunjwa ???!!
Kila kitu kinakwenda kwa mujibu wa Katiba ambayo ndio sheria Mama !
Hata wenyewe wakati ule hawakuwa wakivunja Katiba kusaini ile mikataba !
 
CCM mmeyavagaa kwa kitendo chenu hiki cha aibu - sasa mmewaibua hadi wazee wetu wa heshima kisa tamaa yenu ya madaraka.
 
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Pius Msekwa amesema hafurahii ushindi wa 99% wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika kwani kuna mapungufu mengi. Pia amesema mtu mwenye akili timamu hawezi kufurahia ushindi huo.

Spika mstaafu ameyasema hayo leo alipohojiwa na Sauti ya Kiswahili ya Ujerumani. Spika amevitaka vyombo vya uchaguzi kuondokana na kasoro ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu na kuwaengua wapinzani ambapo amesema hilo halikuwahi kutokea hapo zamani kwanini linatokea sana siku hizi? Amehoji Spika Mstaafu.

---------

View attachment 3170482
Ajiandae kuambiwa na bwana chiembe kuwa hajawai kuwa spika wa bunge bali kajipachika.
 
Kaongea point,hawa CCM sijui wanajiona ni nani

..huyu Mzee sio mkweli.

..hamkumsikia alivyojizima data eti hafahamu jinsi POLISI wanavyoingilia michakato ya uchaguzi?

..pia Mzee Msekwa anadai walioonewa waende MAHAKAMANI!!

..Mzee Msekwa anapaswa kujiuliza kwanini wanaolalamika hawaendi mahakamani, na sababu yake ni kwamba mahakama imepoteza heshima yake.

..Mzee Msekwa amefuatilia hukumu zilizotolewa hivi karibuni ktk mashauri kama lile la Bob Chacha Wangwe, na wenzake? Kwa hukumu za hovyohovyo zinazotolewa na mahakama zetu nani ana moyo wa kupeleka shauri linalohusu uchaguzi huko?

..Na katika mazingira ambapo kuna maelfu ya wananchi waliodhulumiwa hivi mahakama zetu zina uwezo wa kubeba mashauri mengi kiasi hicho?

..Binafsi naona kuna dalili za ulaghai ktk kauli za Mzee Msekwa.
 
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Pius Msekwa amesema hafurahii ushindi wa 99% wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika kwani kuna mapungufu mengi. Pia amesema mtu mwenye akili timamu hawezi kufurahia ushindi huo.

Spika mstaafu ameyasema hayo leo alipohojiwa na Sauti ya Kiswahili ya Ujerumani. Spika amevitaka vyombo vya uchaguzi kuondokana na kasoro ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu na kuwaengua wapinzani ambapo amesema hilo halikuwahi kutokea hapo zamani kwanini linatokea sana siku hizi? Amehoji Spika Mstaafu.

---------

View attachment 3170482

Ila Msekwa afahamu kuwa CCM hawataki kutafuta majawabu. Haya wanayoyafanya na yanayoendelea ndiyo mipango yao. Hata Kinana kaondolewa kwa kuwa alikuwa anataka kuhakikisha ya 2019 hayaendelei 2024.

MWENYE KIFUA KIPANA taratibu anapata influence. Msije shangaa 2025 anapigwa Post la kufa MTU!!
 
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Pius Msekwa amesema hafurahii ushindi wa 99% wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika kwani kuna mapungufu mengi. Pia amesema mtu mwenye akili timamu hawezi kufurahia ushindi huo.

Spika mstaafu ameyasema hayo leo alipohojiwa na Sauti ya Kiswahili ya Ujerumani. Spika amevitaka vyombo vya uchaguzi kuondokana na kasoro ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu na kuwaengua wapinzani ambapo amesema hilo halikuwahi kutokea hapo zamani kwanini linatokea sana siku hizi? Amehoji Spika Mstaafu.

---------

View attachment 3170482
Hawa wazee wangemwitisha kitako Bi mkubwa
 
Angewashauri CCM waache kukiambisha Chama walichokiasisi, sasa hakiaminiki kwa lolote kutokana na viongozi wake kunuka rushwa, ufisadi na tamaa ya madaraka.
 
Back
Top Bottom