Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

#HABARI Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa @halimamdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.#EastAfricanRadio
================
Mambo yameanza kuwa sio mambo.
================


Ni kweli
But wataenda mahakamani kupinga then Mahakama inapiga tarehe
 
Lengo la kufukuzwa ni kuwa wasiende kwa tiketi ya Chadema basi, hata wakipelekwa kwa tiketi ya mahakama sidhani kama Chadema itawasumbua.
Hata mimi najua na nakubaliana na maamuzi. Najua kabisa sasa hivi kwa sababu kina Magufuli and co wako kwenye madaraka na nchi yenyewe ni Tanzania inayokaliwa na watanzania wapole kupita kiasi, wana uwezo wa kufanya chochote. Lakini hii itakuwa historia yenye mafunzo mazuri sana kwa vizazi vijavyo kuona jinsi utawala ulivyokuwa mbovu. Hili nalo linazidi kuwaamsha watu na hata wana CCM wengi wanazidi kuchoka uhuni unaofanywa.
 
CCM wanatega mitego chadema wananasa,hii ya kuvua uanachama inaweza fanya CCM wakaendelea kuifitinisha chadema ili iendelee kuvuana uanachama Mbowe atazame kwa jicho la mbali sana
 
Unaboa na visredi mbuzi. Subiri maana yajayo yanafurahisha. Hao ni wabunge hadi 2025. Anayeweza kuwaondolea ubunge ni Mwenyezi Mungu tu.
Ni kweli. Hili halina shaka. Lakini uhuni unaofanywa utabaki kwenye historia na utazidi kuwafunua watanzania, hasa wana CCM umuhimu wa kuchuja viongozi wa ngazi za juu kwa umakini. Juzi ´nilikuwa nazungumza na kiongozi mmoja aliyewahi kuwa kigogo nadani ya serikali na CCM na alikuwa na majuto kweli kweli hapa tulipofikia.
 
#HABARI Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa @halimamdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao. https://t.co/76GGpFgMnt
 
Mzee Halima kiongozi wa Covid19 hawana chao tena.

Wametumiwa kama toilet paper. Kilichobaki ni kutupwa chooni.

Kwa hili CCM wamefanikiwa kuisumbua CDM. Usumbufu wa muda mfupi.

Haijalishi tena kama Mnyika alipeleka barua NEC au la, sio wana CDM na si wabunge tena.
 
Wamesahau hao wale Ni wabunge ukweli wote utajulikana kadiri sinavyosogea Kama Chadema ilifanya hivyo kuwakomoa imejikomoa yenyewe.Kwisha habari yao , Chadema wivu unawasumbua
Nani anamuonea nani wivu—-wewe lazima utakuwa mzanzibari.
 
Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
Huyo la professori ubongo wake ulishatolewa wote amebaki na kamasi tu
 
Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
Yule Kitila Mkumbo taaluma yake imeingia nzi, ukishakuwa ccm ata uwe na elimu gani ukweli kwako inakuwa ni mwiko
 
Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge

Kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

====

Mambo yameanza kuwa sio mambo.
Huyu mzee naona fahamu zimeanza kumrudia sasa maana naye huwaga kwa kutoa utumbo hajambo!!
 
Back
Top Bottom