Plata O Plomo: Ulimwengu wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja[ Pablo Escobar]

Toka Nikufaham sijawahi kuijutia JF,
Ila mkuu nina suali kuhusu familia yake je ipo mpka leo? Na vip kuhusu mijihela aliyokuwa anaificha ni nani akawa mrith wake?
 
The bold ni kama nilikuwa naangalia movie vile lugha nyepesi Na nilikuwa namsimulia dingi katulia kinoma...next time naomba unitag kaka.....Thanks kwa jiwe hili limenipata gizani.....THE BOLD
 
Toka Nikufaham sijawahi kuijutia JF,
Ila mkuu nina suali kuhusu familia yake je ipo mpka leo? Na vip kuhusu mijihela aliyokuwa anaificha ni nani akawa mrith wake?

Mkuu makilo

KUHUSU NDUGU ZAKE

Pablo ana ndugu wengi ambao bado wako hai mpaka sasa lakini labda nielezee kidogo kuhusu wale ndugu zake wa karibu zaidi (familia yake - mke na watoto)
Baada ya kifo cha Pablo familia yake kwa msaada wa serikali ya Colombia ilibidi wahame nchi kwa kuhofia usalama wao. Nchi nyingi zilikataa kuwapa ukimbizi (asylum) na ikawabidi watumie passport ya utalii kukimbilia nchini Msumbiji.
Baadae serikali ya Colombia ilibidi wafanye makubaliano maalumu na serikali ya Argentina ili kuwapatia ukimbizi familia ya Pablo. Makubaliano haya yalifanikiwa na familia ya Pablo ikahamia Argentina wakitumia majina ya bandia.

i)Mkewe - Maria Henao Vellejo
Mke wa Pablo bado yungali hai mpaka sasa. Maria alianza uhusiano na Pablo kipindi ana miaka 13 na Pablo akiwa na miaka 24 na miaka michache baadae wakafunga ndoa.
Baada ya kifo cha Pablo na kufanikiwa kupata ukimbizi nchini Argentina Maria alibadilisha jina na kujiita Isabel Santos Caballero

ii)Mtoto wake wa Kiume - Juan Pablo Escobar Henao
Pengine huyu ndiye mwanafamilia maarufu zaidi katika ndugu wa Pablo walio hai. Alizaliwa mwaka 1977, na Juan anafahamika kuwa alikuwa karibu mno na baba yake kiasi cha kuwa kama marafiki na wanafanana mno kwa sura. Pia alikuwa ndio moja ya watu walioaminiwa kwa asilimia 100 na Pablo. Ingawa toka kipindi Pablo mwenyewe yuko hai Juan alikuwa hakubalini na biashara za baba yake.

Baada ya kupata ukimbizi nchini Argentina Juan alibadilisha jina na kwasasa anaitwa Juan Sebastian Marroquín.
Mwaka 2009 alichapisha kitabibu kilichoitwa 'Pecados de mi Padre' (Sins of my Father) kwa lengo la kuwaomba msamaha wahanga wote waliokutwa na madhira kwasababu ya baba yake.

Hivi karibuni amechapa kitabu kinaitwa 'Pablo Escobar - My Father' ambacho kinaelezea maisha ya baba yake na genge lake la Medellín Cartel. Pia Juan ni muhandisi na msanifu wa majengo na pia anamiliki kampuni ya mavazi yenye kutumia jina na picha za Pablo Escobar.

iii) Mtoto wake wa kike - Manuella Escobar Henao
Huyu binti alizaliwa mwaka 1984. Huyu ndiye alikuwa roho ya Pablo. Alikuwa anampenda kupitiliza kiasi kwamba alimdekeza katika viwango visivyo mithirika. Huyu ndiye mtoto wake ambaye ilimbidi Pablo achome moto dola milioni mbili ili kumkinga na joto.

Kuna kisa kinaeleza kuwa Manuella alipo kuwa mtoto alimwambia baba yake kuwa anataka Unicorn (kiumbe cha kufikirika kama farasi mwenye mbawa na uwezo wa kupaa). Inasemekana kwamba Pablo alinunua farasi akafanyiwa upasuaji kuwekwa pembe mbele ya kichwa chake, pia akawekewa mabawa ubavuni pande zote mbili ili afanane na Unicorn. Farasi huyu alikufa baada ya siku chache tu.
Pia ni Manuella aliyesababisha Pablo atoe sharti la kuwekewa Telescope gerezani ili awe anamwangalia kila siku jioni akiwa anaongea nae kutoka nyumbani.
Kwa kifupi Manuella alikwa roho ya Pablo.

Baada ya kupata ukimbizi nchini Argentina Manuella alibadilisha jina na kujiita Juana Manuella Marroquín Santos.
Pia Manuella ndiye ndugu pekee wa karibu wa Pablo ambaye anaishi kwa usiri mkubwa mpaka sasa. Hajawahi kufanya mahojiano na vyombo vya habari na hataki, hajawahi kuchapisha andiko lolote na hataki watu wamfahamu.

iv) Roberto Escobar - Kaka wa Pablo Escobar
Huyu alikuwa ni kaka wa damu wa Pablo Escobar na alikuwa ndiye muhasibu Mkuu wa Medellín Cartel. Baadavya kifo cha Pablo, Roberto alikamatwa na alifungwa miaka 10 gerezani kutokana na uhusika wake katika genge la Medellí Cartel. Baada ya kutoka alichapisha kitabu kilichoitwa 'The Accountant's Story' kinachoeleza maisha ya Pablo na Medellín Cartel.

Kuhusu Mali zilizoachwa na Pablo..

Kwanza kabisa tufahamu kuwa wahalifu wote wakubwa hasa wa biashara ya mihadarati mali zao zinakuwa katika aina tatu. Nitaeleza aina hizo na zilienda wapi baada ya kifo cha Pablo..

Aina ya kwanza: vitu vinavyotunza thamani mfano majumba, mashamba, mahoteli na magari adimu ya kifahari (limited editions). Pablo alikuwa navyo vyote hivi na baada ya kifo chake baraza la wawakilishi lilipisha muswada maalumu ambao baadae ulikuja kusaidia kupatikana Sheria ya kuzuia watu kujitajirisha kiharamu (Unjust Enrichment laws). Hii iliwapa mamlaka serikali kuchukua mali zote zisizohamishika zilizomilikiwa na Pablo.
Moja ya mali muhimu za Pablo ilikuwa ni 'pepo' yake ya Hancienda Nápoles (rejea kwenye makala) Familia yake iliwahi kufungua kesi mahakama kuu ya Colombia kuzuia serikalini isichukue makazi hayo kwani si kitega uchumi bali ni makazi wanayoishi kama familia. Kesi hii iliunguruma kwa miaka mingi lakini hatimae mwaka 2006 mahakama ikawaruhusu serikali kuchukua Hacienda Nápoles.

Aina ya pili: wafanyabiashara wengi wa mihadarati (hasa America ya kusini) wana kitu kinaitwa Guacas/Caletas. Hizi huwa ni nyumba za siri zilizoko milimani ambako malundo ya fedha tasilimu huwa yanatunzwa. Yani unaweza ukaingia kwenye nyumba ukaikuta imejaa pesa tasilimu.
Pablo pia alikuwa na hizi Caletas. Na inasemekana kuwa kipindi yuko hai alikuwa anatupa au kuchoma moto kila mwaka karibia dola bilioni mbili (zaidi ya trilioni nne fedha ya kitanzania) kutokana na kuliwa na panya au kuharibika (kuoza kwa mfano) katika Caletas hizi za kuhifadhi pesa pasilimu.
Kutokana na mtoto wake wa kiume Juan kutoshiriki kwenye biashara za haramu za baba yake Caletas zote za Pablo zilikuwa zinafahamika na wapambe wake wa karibu pekee. Hivyo baada ya kifo cha Pablo wakatumia mwanya huo kuchukua fedha zote kwenye Caletas kama mali yao.

Aina ya tatu: fedha zinazo takatishwa
Mabilioni mengi ya Pablo yalikuwa yanainginzwa katika mamia ya akauti za siri kwenye nchi maarufu zinazojulikana kwa utakatishaji fedha ambazo huitwa 'tax havens' (mfano Uswisi, Canyon Islands, Mauritius n.k).
Marekani imeingia mkataba maalumu na Colombia ambapo kuna kikosi kazi maalumu cha kupeleleza na kuzigundua hizi akaunti za siri za Pablo na huwa zikigundulika fedha inatolewa na inagawanywa kwa serikali ya Colombia na Marekani.

Nadhani nitakuwa nimejibu swali lako mkuu. Nifah na wakuu wengine ambao mlipenda niendelee kutiririka naomba msome hapa na tuende kwa mtindo huu. Kama kuna swali au mahali kwenye makala panahitaji ufafanuzi zaidi, you ask a question alafu mimi natiririka na maelezo in details like this.
 
Asante sana the bold,
mkuu kuna vitu unavyo inabidi ufanye kitu zaidi ya hiki we ni noma.
 
Watu wengi wanapenda story zako ni vigumu kuwatag wote mm ninachofanya nikishaona the bold bila kusoma kichwa cha habari nafungua hongera bro
 
Mi bado inanichanganya inamaana kipindi vita imechacha kisawasawa jamaa bado alikuwa anaingiza madafu tu?
 
Back
Top Bottom