Plata O Plomo: Ulimwengu wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja[ Pablo Escobar]

Mmh ndefu sana
 
mkuu blod nasikia pablo aliwahi kuangusha au kilipua ndege ya abiria. je ni kweli? vipi kuhusu mama yake bado yu hai?
 
Ahsante mkuu story nzuri.Nina swali Pablo hakujihusisha kimapenzi na wanawake wengine tofaut na mke wake.
 
Ahsante mkuu story nzuri.Nina swali Pablo hakujihusisha kimapenzi na wanawake wengine tofaut na mke wake.
Afadhali umeuliza hili swali,ktk movie yake anaonekana kujihusisha na mwanamke mwingine (kama kumbukumbu zangu ziko sawa alikuwa muandishi wa habari...Monica sijui)
Alimpenda sana Pablo, ila Pablo hakuwa akimpenda zaidi ya mke wake.

Siku moja wakiwa katikati ya 'game' bibie akamuuliza Pablo... "Mkeo hukufanyia hivi?"
Pablo alikasirika sana hadi akampiga kibao.
Na game ikaishia palepale...

Anyways,tumsubiri The bold kwa maelezo zaidi.
 
mkuu blod nasikia pablo aliwahi kuangusha au kilipua ndege ya abiria. je ni kweli? vipi kuhusu mama yake bado yu hai?
Mkuu lolypop,

Mama mzazi wa Pablo Escobar alifariki mwaka 2006 nchini Colombia jina lake aliitwa Hermilda de los Gaviria.
Mpaka kipindi anafariki alikuwa haivi chungu kimoja na mke na watoto wa Pablo kwasababu walikuwa wanamshutumu yeye (mama mzazi wa Pablo) pamoja na kaka yake Pablo aliyeitwa Roberto Escobar kuwa waliifanya makubaliano na kikundi cha Los Pepes ili waendelee kuishi Colombia. Mke na watoto wa Pablo wanaona kitendo hiki ni kama usaliti kwa Pablo kwani kikundi cha Los Pepes kinahusika kwa asilimia kubwa na kifo cha Pablo pamoja na zaidi ya watu 300 waliokuwa marafiki, washirika na ndugu wa Pablo Escobar.

Pia wanamshutumu kuwa alishirikiana na dada yake Pablo aliyeitwa Alba Marina kuwa baada ya kifo cha Pablo walijinufaisha kinyemela na sehemu ya fedha za zilifichwa kwenye moja ya Caletas.


Nikijibu swali lako kuhusu Pablo kulipua ndege; ni kweli Pablo aliwahi kufanya hili tukio siku ya tarehe 27 Novemba 1989 na ndege hii ilikuwa ni ya abiria ya kampuni ya Avianca Airlines (Flight 203) ambapo siku hii ya tukio ilikuwa inaruka kutoka mji wa Bogota kuelekea mji wa Cali.

Sababu kubwa ya Pablo kuilipua ni kwamba alipewa taarifa kuwa ndege hiyo imembeba mgombea urais aliyeitwa César Gaviria Trujjilo ambaye alikuwa na mafungamano na mahasimu wake wa Cali Cartel. Kwa bahati mbaya taarifa hii haikuwa ya kweli kwani César hakuwepo katika ndege hiyo.

Abiria wote 107 walikuwepo kwenye ndege pamoja na marubani na wahudumu walipoteza maisha katika ajali hii pamoja na watu watatu waliokuwa ardhini ambao waliangukiwa na mabaki ya mlipuko huo.

Hili lilikuwa ni moja kati ya matukio ambayo yalichochea zaidi hasira za Marekani dhidi ya Pablo kwani katika ndege hiyo pia walikuwepo Wamarekani watatu.
Miezi michache baadae muuji mkuu (chief assassin) wa Medellín Cartel aliyeitwa Dandeny Muñoz Mosquera alikamatwa na kufunguliwa mashtaka kumi likiwemo la ulipuaji wa ndege hii. Muñoz alikutwa na hatia katika mashtaka yote na akahukumiwa kifungo cha maisha jela.
 
Mkuu hongera sana kwa stori nzuri iliyoshiba haswaaa.

Ukipata muda tuandikie pia stori ya mwanamama Giselda Blanco au Black Widow, na yeye pia nasikia kuwa alikuwa nguli kwenye biashara hii ya mihadarati,niliangalia kwa ufupi sana stori yake kwenye chanel ya novela 1,nilikuwa impresed sana na ukamanda wake,hebu tafuta hii kitu mkuu
 
Ahsante mkuu story nzuri.Nina swali Pablo hakujihusisha kimapenzi na wanawake wengine tofaut na mke wake.

Mambo ya Series ya Narcos, naipenda ile part Monica anamwambia Pablo "f.... me in a....."
 
Ahsante mkuu story nzuri.Nina swali Pablo hakujihusisha kimapenzi na wanawake wengine tofaut na mke wake.
Mkuu ngaboru,

Pablo alikuwa na michepuko mingi kiasi kwamba hata inashangaza ni kwanini mkewe Maria Gavaria aliendelea kuishi nae. Ni kwasababu alimpenda kwa dhati na alikuwa tayari kumvumilia udhaifu wake??? Au Maria alikubaliana na yote ili aendelee kuishi maisha ya anasa na utajiri??? Labda..
Hata kipindi ambacho Pablo alikuwa gerezani La Catedral, bado kulikuwa na 'oda' maalumu ya kumpelekea wanawake wa kumburudisha.. Kwa kifupi Pablo alikuwa 'mzee wa totoz'..

Lakini mchepuko wake wa muhimu zaidi alikuwa ni Virginia Vallejo. Huyu ndiye ambaye Nifah umemuongelea hapo juu..
Mwanamama huyu licha ya kuwa mchepuko lakini alimpenda kwa dhati Pablo. Huyu ndiye aliyesema msemo ambao nimeunukuu pale mwishoni mwa makala, "Amando a Pablo, Odiando a Escobar" (Nampenda Pablo, Namchukia Escobar).

Mapenzi yao yalikuwa moto moto kiasi kwamba Virginia alikuwa ni moja ya wa wasiri walioaminika na Pablo.
Kuna kisa kinasema kuwa Virginia aliwahi kunasa mimba kwa makusudi ili amzalie mtoto Pablo kutokana na kumpenda sana. Hicho kisa kinaeleza kuwa Pablo kutokana na kumpenda mwanae Manuella kupitiliza alishajiapiza kuwa hatozaa tena mtoto mwingine na mwanamke yeyeto yule.
Baada ya Pablo kugundua Virginia ana mimba akmwambia atoe lakini Virginia akakataa. Pablo akatuma walinzi wake wakamkamta wakaenda kumtoa kwa lazima.

Baada ya kifo cha Pablo Virginia alitumika sana na serikali ya Marekani na Colombia ili kuvujisha siri nyingi zilizohusu maisha ya Pablo hasa hasa vibaraka aliokuwa amewapandikiza serikalini.
Virginia Vallejo ndiye alikuwa shahidi Mkuu katika kesi ambayo Seneta Alberto Santofimio alishtakiwa akituhumiwa kutumiwa na kushirikiana na Pablo Escobar kumuua mgombea urais wa Colombia Carlos Gálan.

Mwaka 2006 Virginia Vallejo alitoa chapisho lake la kwamza (makala) iliyoitwa 'Polla Bianca' (White Dick) ambayo alieleza kwa ufupi mahusiano yake ya kimapenzi na Pablo. Mwaka uliofuata, yaani 2007 akatoa kitabu cha 'Amando a Pablo, Odiando a Escobar' ambapo ameelezea kwa kina uhusiano wake na Pablo, jinsi Pablo alivyowatumia viongozi na watendaji wakuu wa serikali na ugomvi wake na Cali Cartel.
 
The bold , Kwanza ahsante kwa hizi story, maombi yangu kwako,
  1. Hizi short pieces unazowajibu watu, tunaomba uwe unaziweka kwenye uzi wa juu kabisa.
  2. Ni lini utaanza kutoa vitabu/majarida na namna ya kuyapata hasa kwa sisi tulioasi mkoa wa Dar, niko tayari hata leo kutoa advance.
  3. Kwa tunaopenda kukupatia japo kifuta jasho kwa hii burudani tunayoipata tunawezaje kukufikishia hicho kidogo?
 
naomba nipate jibu,
Hiv raw materials za hayo macoccaine na maheroine ni nini? nadhan huko ndo kwa kudeal nako ili kueradicate hii tamu ya chid benz na ray c
 

Mkuu kijana wa leo,

1. Sawa Mkuu ntazipandisha hizi short pieces zote kwenda post #1

2. Mkuu bado niko kwenye mchakato wa kufanya hivyo.. Kuchapisha kitabu chenye ubora inahitaji rasilimali za kutosha! Sijawahi kusema ila naomba niseme leo kuwa I need patners wa kushirikiana nao katika hili. I can' t do this myself, nahitaji mtu/watu wa kufanya nao pamoja hii project.. Kwa ambao wako interested tuwasiliane tafadhali.

3. Mkuu nakuPM namba yangu haraka sana [emoji12] [emoji12] [emoji3] kwa ajili ya hicho kifuta jasho..

Ubarikiwe.
 
Huyu jamaa alikuwa mpambanaji sana maishani.. nimejifunza kuwa hakuna maisha rahisi, daima ni kupambana.. pia hakuna kuridhika hata kama umefanikiwa kwa kiasi gani.. Ubarikiwe sana mleta mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…