Interesting!
Maisha ya Pablo yalijaa ukatili na ubabe sana.
Kuna kisa kimoja kinachekesha lakini hakipendezi.
Wakati Pablo yuko kijana anasoma, walisoma na kijana mmoja jirani yao ambae baba yake alikuwa na ukwasi. Huyu tajiri alikuwa akimpeleka kijana wake shule na Gari. Kilichomkwaza Pablo ni kuwa, tajiri huyo alikuwa akiwapita pasi na kuwapa lifti, na alikuwa jirani na wakisoma darasa moja na kijana. Pablo alijenga chuki kubwa juu yake.
Miaka kadhaa baadae,akiwa tajiri tayari, Pablo aliamua kumshughulikia. Alijipa apizo kuwa, yule mzee hatoendesha gari kamwe maisha yake yote.
'Mwehu' huyu aliajiri mtu akimlipa mshahara, akampa gari na Posho ya mafuta na Posho ya ziada kila atekelezapo kazi aliyopewa.
Kazi yenyewe ilikuwa ni kuteketeza magari yote ya huyo tajiri. Kisha kila gari atakalo nunua liteketezwe kwa moto au kuliiba.
Dunia hii ina wababe.