SoC01 Platform ya Siasa Afrika sio chaguo sahihi la maendeleo kwa vijana

SoC01 Platform ya Siasa Afrika sio chaguo sahihi la maendeleo kwa vijana

Stories of Change - 2021 Competition

odaafrica

New Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
2
Reaction score
12
Afrika tumekuwa tukitafsiri siasa tofauti , miaka ya nyuma kidogo hususani miaka ya 2000 vijana wengi tulijua siasa ni uongo mtupu , na jamii nyingi za vijana ziliamini kwamba hupaswi kumuamini kabisa mwanasiasa , lakini miaka ya 2015 na kuendelea, siasa ilianza kuonekana ni ajira nzuri na inayolipa sana , hii ni baada ya vijana wengi wasomi kuingia mtaani kwa kutegemea watapata ajira kutoka serikalini , jambo ambalo liliwaamuza na linaendelea kuwaumiza vijana wengi wasomi barani Afrika , wachache sana wanaingia kwenye siasa kwakua kuna mambo wangependa kuyabadiri katika jamii zinazowazunguka na wachache hao mala zote hubadirika na kumezwa na mifumo ya serikali iliyokuwepo na kujikuta wakianza kufanya maamuzi kwaajili ya pesa na mafanikio ,

Tuna mifano mingi sana ya wanasiasa vijana waliaminiwa na vyama vya siasa pamoja wananchi wakakaa bungeni na katika nafasi nyingine za serikali baada ya kuondoka kwenye mfumo hawachukui muda wanapoteza mali waliyochuma na kuanza kuhangaika kwa kutumia gharama kubwa tena wakitamani kurudi katika mfumo wa Serikali.

Kuna mbunge yupo Morogoro na amekaa bungeni miaka 10 lakini kwa sasa yupo anachoma chips , sasa Je, ni platform gani ambayo ndiyo nguzo kubwa ya maendeleo kwa vijana , BIASHARA NA UJASILIAMALI , kwanini ?

Mataifa yote yaliyoendelea duniani , asilimia kubwa yamejengwa kwa jasho ,akili na muda wa vijana wajasiliamali , sisi kama vijana wa kiafrika tukiwekeza nguvu kubwa katika sekta ya biashara na ujasiliamali tuko na nafasi kubwa sana ya kufanikiwa na kulisogeza taifa na bara Afrika mbele zaidi , ni vigumu sana siasa kukuunganisha wewe kama vijana na vijana wa matiafa mengine , lakini ni rahisi sana wewe kama kijana wa kitanzania ukiwa kwenye ulimwengu biashara na ujasiliamali kuungana na vijana wenzio wa mataifa mengine na mkafanya jambo kubwa la maendeleo ,

Kuna vijana wengi na wana biashara kubwa kutoka mataifa mengine kama vile China , America , uk , Canada hata nchi za barani Afrika wanatafuta sana vijana wa matifa mengine kuungana kibiashara (partnerships ) , kitu ambacho kinaweza kutufanya kuwa na maendeleo binafsi , kutangaza taifa letu na hata kulifanya liendee kwa kulipa kodi , lakini hakuna vijana wa taifa fulani wako tayari kuungana na taifa fulani kwa sababu za kisiasa ,

Na siku ukiamua kuingia kwenye ulimwengu wa biashara na ujasiliamali kumbuka sana kutochanganya kati ya siasa na biashara , ama maisha yako binafsi na biashara, tujifunze kuacha biashara kuwa na maisha yake binafsi , ni suala gumu sana lakini kila kitu nikujifunza , vjiana wa africa tujifunze lugha ya biashara na maisha ya biashara pia.

5dd14ffba310cf3e97a6b9aa.jpeg
 
Upvote 6
Ndio shughuri au career inayolipa vizuri zaidi.
Ndio shughuri yenye uhakika wa kulipwa pesa yako mkimaliza tu kipindi.
Ndio career itakayo Fanya usiguswe ukiwa na mipango yako isiyo faa.
Ndio career itakayo onekana una akili kuliko mtu yoyote.
Ndio career yenye hadhi kubwa kabisa.
Ndio career pekee ushauri wako angalau inaweza kusikika.
Ndio career itakayo kupa dili nyingi mno
 
Back
Top Bottom