Wanabodi heshima kwenu!
Taarifa zilizonifikia kutoka chanzo ninachokiamini ni kwamba ziara za Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mikoani pamoja na mambo mengine anazitumia kujiweka sawa kwa ajili ya kumrithi Rais Magufuli.
Duru za siasa mikoani zinaeleza kwamba, sehemu kubwa ya Wabunge waliopitishwa na CCM na hatimaye kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ni mipango mahsusi iliyopangwa na PM Kassim na kuratibiwa na Katibu Mkuu Dk. Bashiru Ally kama hatua ya kwanza ya kujiweka sawa kwa 2025.
Hatua ya pili kupitia wabunge hao ni kupanga safu katika Uchaguzi Mkuu wa ndani ya Chama 2022 ambapo "wabunge wa PM" wamepewa jukumu la kushawishi wajumbe mikoani na wilayani kuunga mkono harakati hizo butu.
Taarifa zinaeleza kwamba, harakati hizo zinam-keep busy Waziri Mkuu kiasi kwamba utendaji wake kuwa shakani au dhaifu.
Hata hivyo, taarifa kutoka kwenye korido za Lumumba zinaeleza kuwa mamlaka za juu zimepata taarifa na hivyo hatua kadhaa zimeanza kuchukuliwa dhidi ya SG na PM likiwemo uteuzi wa Polepole Ubunge kufuatilia nyendo za PM bungeni.
My Take! Kutamani Urais si dhambi. Lakini tamaa hiyo inapokuondoa katika utendaji kazi basi ni kheri kujiuzulu ili kuwa huru kusaka Urais. Lakini pia ikumbukwe Waziri Mkuu naye ni Mkulu kiprotokali. Anaishi Ikulu. Kuutamani Urais ni kutaka kuishi Ikulu kwa miaka 20 tofauti na Rais aliyeishi 10 years. Hawezi kuruhusu ajali hiyo kutokea. Huu ni muda wa kujenga nchi si kusaka madaraka.
Ni ushauri tu!