PM Majaliwa: Bwawa la umeme kukamilika Juni 2022

PM Majaliwa: Bwawa la umeme kukamilika Juni 2022

Tuombe Mungu iwe hivyo maana msimu huu maneno yamekuwa mengimengi.

Vv
Sospeter Muhongo nasikia kaibuka huko, kwa wasiomkumbuka huyu mwamba waziri wa nishati na madini wa awamu ya Jk ambaye akiwahi kusema watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye miradi ya gesi na mafuta bali wanaweza kuanzisha miradi ya viwanda vya juisi ya matunda!
Leo kaibuka na kudai miradi ya Umeme inayotegemea vyanzo vya maji haina faida kwa ulimwengu wa sasa!
Wanajamvi tuombe uzima, makambare yameanza kutoka kwenye hibernation!
 
wewe ndo humuamini ila mimi namuamin
Huyo mzee tapeli alisema SGR kipande cha Dar-Moro kinaanza kazi Nov 2019 haikuwa kweli. Akajitokeza hapo katikati akasema hicho kipande kitakuwa tayari Aprili 2021, sasa amebadilika tena ni mpaka August 2021! Je huko kwenye umeme ataaminika na nani? Huyo mzee namfananisha na ile mamlaka ya utapeli ya hali ya hewa, ambao huwa wanatabiri mvua kunyesha, na kuwa kinyume chake kila mara.
 
Ni kama vile mkaa unaonekana ni nafuu kuliko gesi kwa sababu gharama za deforestation haziingizwi kwenye bei.
Nilidhani hata gesi inasababisha environmental pollution. If I am right, what is the cost and how do you mitigate that!
 
Sisi wa hanga wa mgao wa umeme wa kipind kile tukisia haya maneno ya PM twa farijika sana. Pengine hapatatokea tena kakika nchi hii wahanga wa mgao wa umeme.

Lakini kwa nini haikuoneshwa bei ya umeme wa gas? Mnataka kumpa huyu Prof upper hand ya kuongea ugoro wake tena Bungeni?

Je huu mradi unaenda sambamba na ujenzi wa njia za kuufikisha kwa walaji au zinasubiri miaka mingine ya mbele?

PM na wengine mnaowindwa na genge la mijizi na mafisadi wanao jipendekeza kwa bidii na maariafa. Msikose kuwa na planB likitokea la kutokea muwe tayari kwa hali zote kuitekeleza. La muhimu muwe pamoja na mshirikiane ie team work.
Mkuu kwa ufupi njia za kufikisha umeme kwa walaji zipo zinaendelea kujengwa. kwa mfano mimi nimeshiriki kuchukua taarifa(detail survey) za njia(route) ya 400KV kutoka Bwawani rufiji hadi chalinze sub station. Hapo hapo route kutoka Chalinze hadi dar, chalinze-Dodoma , Chalinze-Tanga kote huko kazi inaendelea ku peek detail pamoja na watu wa udogo wapo kazini kusoma udongo kwahajiri ya kujenga tower [emoji556]. Kwa ufupi naomba hii kazi ukamilike maana imechukua pesa nyingi za walipa kodi na ni mrad mkubwa kweli.
 
Duh!
Ukamilike tu huu mradi umekuwa na maneno mengi
 
Hivi unafikiri transformer, Generators na control system zote zitafungwa za mwaka 70 kwa akili yako!!?..😀😀Labda CAG yeye mwenyewe au team yake hawako compitent juu ya feasibility study ya mradi wowote wa umeme, wanaposema imetumika feasibility ya miaka ya 70 sijui wameisoma vyema hiyo feasibility ilichokuwa inakihitaji kitimie na ingetumika kwa miaka mingapi kutoka wakati huo na je! Hizo MW2100 zitakazozalishwa na mradi huo hazitaleta ongezeko chanya la umeme kwenye mfumo wetu wa sasa wa umeme!?.
CAG sio kuwa yeye anajua kila utaalam. Anachojua ni uhasibu na auditing; hayo ya taaluma zingine anaelezwa ingawa baadhi ni waajiliwa ktk ofisi yake.

Mambo ya efficiency ya mradi kiufundi hawezi kuwa competent kama watu waliosomea hizo fanii na kuzipractise.

Mradi wa stigler ni viable na rahisi hata waziri mkuu ameeleza unit moja ya umeme bei yake ni sh 36 lakini kwa gesi ya kusini unit moja ni sh 150 ( taarifa ya habari saa 2.00 usiku UTV).
 
Ikikamilika kabla ya 2025 nitatembea uchi kutoka Dar mpaka Morogoro!
 
Kumbe umeme utokanao na maji Ni wa Bei ya chini kiasibhicho?
Ina maana professor hakuwahi kulifahamu hilo?

Swali la msingi Ni kweli huo mradi ndio utakakua suluhisho la tatizo la umeme kama tulivyokua aminishwa?
Maana inatakiwa umakini Sana unapoaminishwa na mwanasisa!

Sisi kwetu Ni kuwatakia heri na wepesi katika kutekeleza hayo.
 
Shida ya majaliwa ni muongo muongo hivi
 
Waziri mkuu wa Tanzania Bwana Majaliwa leo ametembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na kuangalia maendeleo ya ujenzi.

Majaliwa ameridhika na kasi ya ujenzi wa mradi huo na amesisitiza utakamilika kwa wakati mwaka 2022 mwezi wa 6 kama majubaliano yalivyo.

PM amesema mradi utakamilika kama ilivyopangwa kwani pesa zipo hakuna sababu ya kuchelewesha mradi.

PM amasema mradi huo utatoa faida kubwa kwa uchumi wa nchi yetu kwani mradi utaleta umeme wa bei nafuu sana kwa watanzania.

Kwa wasiojua.
Kuzalisha Unit moja ya umeme wa maji hua ni TZS 36, Nuclear TZS 66, Jua TZS 105, Joto Ardhi TZS 114.5, Gas 150 na Mafuta mazito 460.

Kwa kuangalia hizo unit price unaona wazi kabisa kua hakuna source yoyote ya nishati yenye gharama ndogo kama maji.

Tuseme kuwa PM bado hajapangwa? Maana hawa tayari:
Mama yetu, Ndugai na Wabunge wanafiki na vilaza washasetiwa tayari ili team Msoga iingize vitu vyake.
Ukimuangalia PM ni kama vile ule mtandao wakumchafua Magu ashaushitukia, na ndiyo kiongozi mwandamizi pekee ninayemuona hajatoka kwenye line, swali linabaki moja, atauweza huu mtandao uliomua Magufuli?
Wewe tangu Magu atutoke, sisikii tena TANZIA. Washenzi hawa walizitumia ili kumflustrute our hero.

R.I.P mwamba
 
Huyo mzee tapeli alisema SGR kipande cha Dar-Moro kinaanza kazi Nov 2019 haikuwa kweli. Akajitokeza hapo katikati akasema hicho kipande kitakuwa tayari Aprili 2021, sasa amebadilika tena ni mpaka August 2021! Je huko kwenye umeme ataaminika na nani? Huyo mzee namfananisha na ile mamlaka ya utapeli ya hali ya hewa, ambao huwa wanatabiri mvua kunyesha, na kuwa kinyume chake kila mara.
project can delay due to reasons beyond the control..lkin cha muhimu kazi inaonekana na inaridhisha tunachohitaji ni faith..
 
Tuseme kuwa PM bado hajapangwa? Maana hawa tayari:
Mama yetu, Ndugai na Wabunge wanafiki na vilaza washasetiwa tayari ili team Msoga iingize vitu vyake.
Ukimuangalia PM ni kama vile ule mtandao wakumchafua Magu ashaushitukia, na ndiyo kiongozi mwandamizi pekee ninayemuona hajatoka kwenye line, swali linabaki moja, atauweza huu mtandao uliomua Magufuli?
Wewe tangu Magu atutoke, sisikii tena TANZIA. Washenzi hawa walizitumia ili kumflustrute our hero.

R.I.P mwamba

Wakati Magu anachafua wenzake mbona uliona sawa kwa kusema anasafisha nchi, iweje wengine wakisema ukweli sasa useme anachafuliwa? Kiongozi anayenajisi chaguzi za nchi , na kuendesha makundi ya kihalifu dhidi ya wote wanamkosoa ana usafi gani?
 
Back
Top Bottom