Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
Sina tatizo na hii project kabisa ila sina imani kabisa na wanasiasa wa ccm, hizi calculations tulishapigiwa sana lakini hakuna tulichoambulia.
Lakini pia tukipiga hesabu hizo lazima tujue kuwa Hydro inaonekana ina bei nafuu kwa sababu gharama za uharibifu wa mazingira haziingizwi kwenye hizo hesabu. Ni kama vile mkaa unaonekana ni nafuu kuliko gesi kwa sababu gharama za deforestation haziingizwi kwenye bei. Tungekuwa tunajumuisha na gharama ya kupanda upya miti na athari katika tabia nchi, bei ya mkaa isingeshikika.
Ni hapo sasa tuchakate akili zetu ili tusiwaachie hawa wanasiasa pekee watujie na hizo cheap statistics na sisi tuzimeze tu, tujue ikiwa gas, hydro nk kwenye enviromental impacts inakuwa covered or not, kwenye miutambo ya songas, na hata Dowans tulikuwa tinalipa mpaka capacity chargies.
Hawa wanasiasa ni watu wa kupita na session zao end of the day atataka kugain porpularity ameke lakini sisi walaji ndiyo tutaumia zaidi.
Ikiwa report ya cag inaenda kwa rais then bungeni baada ya hapo inakuwa ni public docs basi na hii mikataba na plan project ipitie mfumo huo huo ili end of the day iwe ni miradi ya public na si ya mtu mmoja. Hapo hata kama ikitokea la kutokea tunawajibika wote