PM Majaliwa: Bwawa la umeme kukamilika Juni 2022

Tuombe Mungu iwe hivyo maana msimu huu maneno yamekuwa mengimengi.

Vv
Sospeter Muhongo nasikia kaibuka huko, kwa wasiomkumbuka huyu mwamba waziri wa nishati na madini wa awamu ya Jk ambaye akiwahi kusema watanzania hawana uwezo wa kuwekeza kwenye miradi ya gesi na mafuta bali wanaweza kuanzisha miradi ya viwanda vya juisi ya matunda!
Leo kaibuka na kudai miradi ya Umeme inayotegemea vyanzo vya maji haina faida kwa ulimwengu wa sasa!
Wanajamvi tuombe uzima, makambare yameanza kutoka kwenye hibernation!
 
wewe ndo humuamini ila mimi namuamin
Huyo mzee tapeli alisema SGR kipande cha Dar-Moro kinaanza kazi Nov 2019 haikuwa kweli. Akajitokeza hapo katikati akasema hicho kipande kitakuwa tayari Aprili 2021, sasa amebadilika tena ni mpaka August 2021! Je huko kwenye umeme ataaminika na nani? Huyo mzee namfananisha na ile mamlaka ya utapeli ya hali ya hewa, ambao huwa wanatabiri mvua kunyesha, na kuwa kinyume chake kila mara.
 
Ni kama vile mkaa unaonekana ni nafuu kuliko gesi kwa sababu gharama za deforestation haziingizwi kwenye bei.
Nilidhani hata gesi inasababisha environmental pollution. If I am right, what is the cost and how do you mitigate that!
 
Mkuu kwa ufupi njia za kufikisha umeme kwa walaji zipo zinaendelea kujengwa. kwa mfano mimi nimeshiriki kuchukua taarifa(detail survey) za njia(route) ya 400KV kutoka Bwawani rufiji hadi chalinze sub station. Hapo hapo route kutoka Chalinze hadi dar, chalinze-Dodoma , Chalinze-Tanga kote huko kazi inaendelea ku peek detail pamoja na watu wa udogo wapo kazini kusoma udongo kwahajiri ya kujenga tower [emoji556]. Kwa ufupi naomba hii kazi ukamilike maana imechukua pesa nyingi za walipa kodi na ni mrad mkubwa kweli.
 
Duh!
Ukamilike tu huu mradi umekuwa na maneno mengi
 
CAG sio kuwa yeye anajua kila utaalam. Anachojua ni uhasibu na auditing; hayo ya taaluma zingine anaelezwa ingawa baadhi ni waajiliwa ktk ofisi yake.

Mambo ya efficiency ya mradi kiufundi hawezi kuwa competent kama watu waliosomea hizo fanii na kuzipractise.

Mradi wa stigler ni viable na rahisi hata waziri mkuu ameeleza unit moja ya umeme bei yake ni sh 36 lakini kwa gesi ya kusini unit moja ni sh 150 ( taarifa ya habari saa 2.00 usiku UTV).
 
Ikikamilika kabla ya 2025 nitatembea uchi kutoka Dar mpaka Morogoro!
 
Kumbe umeme utokanao na maji Ni wa Bei ya chini kiasibhicho?
Ina maana professor hakuwahi kulifahamu hilo?

Swali la msingi Ni kweli huo mradi ndio utakakua suluhisho la tatizo la umeme kama tulivyokua aminishwa?
Maana inatakiwa umakini Sana unapoaminishwa na mwanasisa!

Sisi kwetu Ni kuwatakia heri na wepesi katika kutekeleza hayo.
 
Shida ya majaliwa ni muongo muongo hivi
 
Tuseme kuwa PM bado hajapangwa? Maana hawa tayari:
Mama yetu, Ndugai na Wabunge wanafiki na vilaza washasetiwa tayari ili team Msoga iingize vitu vyake.
Ukimuangalia PM ni kama vile ule mtandao wakumchafua Magu ashaushitukia, na ndiyo kiongozi mwandamizi pekee ninayemuona hajatoka kwenye line, swali linabaki moja, atauweza huu mtandao uliomua Magufuli?
Wewe tangu Magu atutoke, sisikii tena TANZIA. Washenzi hawa walizitumia ili kumflustrute our hero.

R.I.P mwamba
 
project can delay due to reasons beyond the control..lkin cha muhimu kazi inaonekana na inaridhisha tunachohitaji ni faith..
 
Nimependa anavyosisitiza pesa ipo, sasa sio wanyonge tena, wasisogeze muda mbele kama kweli pesa ipo.
hiyo kusisitiza "pesa ipo"mmi ndo kumenipa wasiwasi.
 

Wakati Magu anachafua wenzake mbona uliona sawa kwa kusema anasafisha nchi, iweje wengine wakisema ukweli sasa useme anachafuliwa? Kiongozi anayenajisi chaguzi za nchi , na kuendesha makundi ya kihalifu dhidi ya wote wanamkosoa ana usafi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…