Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Waziri Mkuu ameomba Watanzania waiamini Serikali kwenye uwekezaji unaotaka kufanyika Bandari, akidai kuwa sio uwekezaji wa kwanza wala sio jambo jipya bali kulikuwa na mwekezaji ambaye walimpa vipindi vya kumfanyia tathmini hadi akafika miaka 22 na ameondoka Novemba mwaka 2022; hivyo DP World nao watampa vipindi kama aliyekuwepo.
Waziri Mkuu Majaliwa anasema Mwekezaji huyu mpya hajauziwa bandari, ila atapewa kuwekeza.
Kuhusu ukomo wa muda, amesema wanaodai DP World kapewa miaka 100 au milele sio kweli kwani hapajaandikwa popote juu ya ukomo ila akija ndio watakubaliana juu ya suala hilo.
Ameongeza kuwa Mwekezaji hajauziwa ardhi kwani hata sheria za nchi haziruhusu ila mwekezaji atapewa kibali cha kukaa juu ya ardhi na atalipa kodi, pia mkataba utazingatia maslahi ya nchi kama wengi wanavyodai.
Pia soma: Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World