Tetesi: PM, Philips, Foreign na February wamekalia kuti kavu?

Sote tunajua katika wote hao hakuna mwenyewe tatizo, tatizo ni boss mwenyewe. Lakini katika nchi zenye mifumo ya kusadikika, mabosi huwa ni miungu watu, huwa hawapaswi kuonekana wamekosea, na hilo ili litokee inabidi tambiko la kafara lifanyike. Sasa hao wote ni kafara tu ili kuondoa nuksi za mizimu.

Lini tambiko litafanyika, sote tunasubiri, huku tukijua mbuzi wa kafara wapo tayari.
 
Wa fedha sitashangaa sana ili abaki inabidi apige kazi kweli maana elimu ya kodi kwa wananchi bado hajatoa vya kutosha, kunakipindi walijitahidi sana ila sasa kimya.

Ni kiri wazi mimi sio mtaalumu wa maswala ya kodi ila ninakauelewa kadogo kuhusu umuhimu wa kodi., Sasa inapofikia mahali makusanyo ya kodi yanapungua wakati ukinunua bidhaa baadhi ya maduka makubwa na baadhi ya min supermakert ukidai risiti za EFD hawana, kidogo hii linashangaza kama kweli taifa kimedhamiria kukusanya kodi na kutekekeza miradi mikubwa kama ya ujenzi wa SGR.

Mheshimiwa raisi anania nzuri sana na nchi hii ila atakwamishwa na baadhi ya watendaji
wake aidha kwa kujua au kuto kujua.
 
PM siyo rahisi hivyo ww kumtoa pale, hao wengine wanaweza kutupwa chini anytime...


Wizara ya viwanda ni ngumu sana, yule waziri atapata angalau mda wa kupumzika...

Makyembe nae akapumzike sasa, anataka kufia serikalini au
 
Juz ndo nilijua PM anasukumwa tu..hili la wafanya biashara kumbe alipigiwa awape siku 4
 
Jiwe anaogopa kumtumbua maana Mange alishasema kwamba Marope atatumbuliwa na MAGU kwahiyo anataka kumprove wrong.
 
Tatizo sio mkurupukaji na hana ngebe na maneno ya kashfa,kwahyo anakuwa haendani na modus operandi ya Awamu ya tano.
 
Madaraka yalikabidhiwa kwa mshamba, bas tabu tuupu!!
 
Hii tabia ya kutumbuana natamani ingeshuka hadi vyeo vya chini. Nadhani hii itasaidia Wafanyakazi wa umma kutambua zile nafasi siyo permanent wala guaranteed hadi ustaafu kupitia hiyo mentality labda wataanza kushawishi na kutunga sera na sheria zilizo rafiki kwa watu sekta binafsi na zile ambazo hazitambuliki wakitambua na wao siku yeyote wanaweza kuhamia kwenye hizi sekta kabla hawajastafu na wakiwa na watoto ambao hawajamaliza shule. Tukifanikiwa hivyo natarajia kodi na ukiritimba zitapungua na serikali Itakuwa inahusisha wadau kwenye sekta uhusika kabla hawajafanya maamuzi. Naamini ukitaka kuona mtu anachapa kazi mtoe kwenye comfortable zone yake.
 
Tatizo ni jamaa mwenyewe dish linaonekana kuyumba sana
 
Bosi ukiwa mkali sana utawachanganya walio chini yako mpaka kazi ulizowatuma wataziharibu kwa hofu
 
Nimesoma uzi wako kwa umakini. Nakubaliana na wewe kwa PM hapo, huyu bwana anaonekana majukumu yamemzidi uwezo na kutemwa ni suala la muda tu,

Filipo bado yuko salama kwa sasa kama hatatoa kauli tata kama alizotoa Bungeni juzi hivi majuzi,

Mwisho ni bwana Februari, Huyu nadhani yuko salama kabisa kwa sababu wizara yake haina relevance kiivo ktk nchi, (sio wizara nyeti) kwahyo hakuna sababu yoyote ya kumwondoa.
 
Kampuni na biashara nyingi zinakufa makusanyo ya kodi yatapandaje unafikili? Kweli ukipewa ukuu kwenye hii awamu ni sawa umebebeshwa gunia la misumali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…