Magige si wa kupewa pole. Kwanza, inashangaza mbunge mzima anafanya mambo ambayo hata mtu asiyeitwa mheshimiwa hawezi kufanya kana kwamba hakwenda shule. Kama alikuwa akimpenda si angemuoa? Je kwanini marehemu na Magige hawakumaliza sakata moja na kuoana badala ya kuanza kufanya uhuni? Kutengana si kuvunja ndoa. Walipaswa wavunje ndoa kwanza ili wawe na uhuru wa kuoa na kuolewa. Huyu ni mhuni wa kawaida ambaye huenda amekuwa chanzo cha wawili waliokuwa mke na mme kukosana. Huyu anaweza kuonekana kama ni gold digger tu ambaye ameamua kuvuruga ndoa ya wenzake ili apate yeye. Sitaki nimhukumu kwani sijui stori nzima ila hili haliepukiki kwa vile walivyojiamini bila kuvunja ndoa ya kwanza.