Pole Catherine Magige, hii iwe fundisho kwa wadada maarufu nchini

Pole Catherine Magige, hii iwe fundisho kwa wadada maarufu nchini

Ni mchumba wake na Pete kavishwa...na kakaa nae 2 yrs toka 2018

Sema Cat alizubaa sana ilitakiwa hiyo divorce iwe imeshatoka mapema sana, ndo imekula kwake, na kama alikuwa anafanya nae investments zozote sijui mwanaume anaandika majina yake.....hiyo ndo nitolee wife analamba vyotee maninaaa[emoji134]

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app

Dooh unafanyaje investment na mchumba [emoji848][emoji848] ambaye anatarajia talaka [emoji848][emoji848] wanawake ifike wakati tujitambue
 
Ila ukweli kabisa...Cat alikuwa na muhaho wa ndoa[emoji848]

Huyu jamaa kafa kwa mambo mengi asee

Kama maiti inagombaniwa hivi je wakati yuko hai si alikuwa anarushiwa vipapai mpaka vya India?...asingeweza kuchomoka huyo, ukute mandumbaa yamemuua[emoji849]



Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app

Funzo kwa wanaume, wanawake usipokua makini watakuumiza sana tu mpaka upate presha zisizokua na kichwa wala miguu
 
Nakwambia Mchepuko alichemsha mwenyewe akasepa,kila akijaribu kujipendekeza kwa Mama anakuta Mama yuko busy anasali na Kikundi chake cha Moyo Mtakatifu wa Yesu kumwombea mtoto wake arudi kwenye Ndoa yake,Mchepuko kwangu hakuwahi thubutu hata kuandika msg. Kajipendekeza kwa Cousins wetu wakawa wanamlia vipesa vyake,wadogo zangu wa kiume wawili walikuwa na misimamo pia kumtetea Mke wa Ndoa, familia nzima tulisimama,Kaka akachoka akamwambia nimechoka kutengwa na familia na ndugu zangu,akarudi zake kwa Mkewe wa Ndoa na ndiyo tukarudisha mahusiano nae kifamilia.
Sasa ndo ukute familia inakukubali,ukikuta familia kama ya huyo Madoda wanafiki tu wanamsapoti kaka yao na ufedhuli wake unafanyaje sasa maana Huyo wifi mwanzo alikua best yake kamchenjia tu mwishoni ukute waligombana..!!!yaani inauma sana baasi tu bora hata km wifi unajua lakini usijiingize kwenye mgogoro usokuhusu
 
Kumbe ni mkurya...basi ndo maana

Fita ni fita muraa

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Mkurya huyo Magige hyo ni muraaa....!!!!yaanni ni wabishi sana hao na huyo anafia ndoa kwa sababu jamii za kikurya zinamdharau sana na hivi hajaolewa ndo kabisaa yaani anahangaika kuolewa hata afanyeje
 
Hiyo pete ilikuwa pete ya u-mchepuko au ya kitu gani? Mtu hawajapeana talaka na mke wake, anakuvishaje pete, na hiyo pete angeivaa hadi lini bila ndoa? Wanawake wanaokutana na cases kama hizi wajifunze kwa Shaa; kasubiri mpaka talaka ya Master Jay na mkewe imetoka ndiyo na yeye kaamua hata na kuzaa sasa.

Wanaume wetu hawa asikudanganye sijui hamtaki mke wake, sijui wanaishi tu kwa ajili ya watoto wala vya talaka ipo kwenye process; akuoneshe kabisa hiyo talaka ndiyo mengine yaendeleee. Sio una kazi ya kudanganywa na pete sijui kubeba mimba, huku mtu anapatwa na matatizo yet anataka aitiwe mkewe. Mh atakuwa ameshajua alikuwa na nafasi gani kwa marehemu.

Kwanza haitakiwi kuolewa na mtalaka [emoji2356][emoji2356] kama alishindwa kuishi na mkewe atakuja tu kukusumbua na wewe huko mbele ya safari [emoji4].
 
Nafikiri Yule unae mpenda na kumheshimu anapo fariki kuna vitu vya kuzingatia kama kweli tulimpenda na kumheshimu...

Kwanza ni kutowazuia wanao mpenda wengine kuombeleza...

La pili ni kuhakikisha humletei aibu marehem wakati wa mazishi..

La tatu ni kuhakikisha Siri za marehem zinabaki kuwa siri..sio wakati wa kumvua nguo marehem..

Kama hayo yote yatazingatiwa basi sioni
Ni vipi Mke na mchepuko wanaweza anzisha vurugu wakati wa msiba..


Hivi ni ngumu Sana watu mnaochukiana kuzuia chuki zenu Kwa siku mbili mkamzika mnae claim 'mnampenda na kumheshimu'..halafu vurugu zenu zikaja
Kuendelea baada ya mazishi?
 
Hahaa ungefight? Mm nisingefight niwe mkweli!..ila sina hakika sana!
Hahaaa,mi natakaga ujinga sasa! Kwanza ye na hicho kikundi chake wangeishia nje na wangelala selo, pumbavu kabisa!

Huwa nawashauri tu wadada ukimkuta mtu na mkewe wapo kwenye sintofahamu usiingie hapo utaishia kuaibika tu,ndo haya sasa!

Sent from my TECNO P701 using JamiiForums mobile app
 
Sasa ndo ukute familia inakukubali,ukikuta familia kama ya huyo Madoda wanafiki tu wanamsapoti kaka yao na ufedhuli wake unafanyaje sasa maana Huyo wifi mwanzo alikua best yake kamchenjia tu mwishoni ukute waligombana..!!!yaani inauma sana baasi tu bora hata km wifi unajua lakini usijiingize kwenye mgogoro usokuhusu

Hapo ndipo kwenye mtihani ukikuta familia ni ndumilakuwili. Kwa Wifi yetu sisi sote tulisimama kidete kutetea Ndoa yake,na Mwaka huu wanatimiza miaka 20 ya Ndoa yao.Wifi yetu anampenda sana Mumewe utakuta hata akipuyanga wakati mwingine anamfichia makosa wanayamaliza kimya kimya na Ndoa yao ina Amani sana.
 
Kwanza haitakiwi kuolewa na mtalaka [emoji2356][emoji2356] kama alishindwa kuishi na mkewe atakuja tu kukusumbua na wewe huko mbele ya safari [emoji4].

Shida yetu Wanawake ni kujiona wewe ni bora kuliko aliyekuwepo. Ukianza kupigwa matukio ndiyo unajiona kumbe na wewe ulikuwa boya tu uliuvaa mkenge kama uliyekuwa unamdharau
 
Back
Top Bottom