Pole Freeman Mbowe! Umedhalilishwa sana ila Mungu atakulipia

Kwangu nimefurahi Kwa sababu huu mtindo wa kupakana matope Kwa uzushi umeasisiwa na machadomo ambao huwazushia hivyo watu wasio waunga mkono ikiwemo Kuitwa chawa.

Sasa Kwa kuwa imeanza kuwakuta wenyewe nimefurahi kweli,na hata hao wengine watakuja kumalizana Kwa utaratibu huu huu maana ndio mbinu inayowalipa.

Hukumbuki nyie Machado Huwa mnasema Samia ameuza Mali za Tanganyika bila ushahidi kisa kuita wawekezaji,Huwa mna mbagua Kwa Jinsia yake na eneo anakotokea nk nk.

Ila Kila mtu atapata majibu Kwa wakati wake,hayo ya Mbowe ni Mwanzo tuu,tutasikia mengi mda utaleta majibu.
 
Uchaguzi umeisha ila Mbowe matusi na uchafu aliopakwa utaishi milele.

Nyinyi mmepata madaraka, yeye mmemuachia maumivu.

Alichowakosea nini Chadema, ni huo uenyekiti tu?
Malipo ni hapa hapa duniani. Yeye hakuwavunjia heshima, lkn wao walifanya hivyo. Karma haikoseagi njia...inakujaga kama dhoruba
 

View: https://youtube.com/shorts/zG_n6kzkVHk?si=fVQ1042Z8ex7G3cw
 
Malipo ni hapa hapa duniani. Yeye hakuwavunjia heshima, lkn wao walifanya hivyo. Karma haikoseagi njia...inakujaga kama dhoruba
Ni kweli Lissu, Lema na Heche watapokea anguko lao.
 
Hakuna hoja ya kimantiki ya kuthibitisha Mungu yupo.

Habari za "Mungu atakulipia" ni kujifariji tu.
 
Mkuu, Mbowe katukanwa sana kapakaziwa hadi kupotea kwa Soka.

Muacheni apumzike hastaili huu usaliti.
Hata mipango ya kuuawa kwa Chacha Wangwe tunahisi niyeye kwa kushirikiana na Deus Mallya.
 
Hawatafika mbali
 
Mtafute sasa akuajiri kwenye biashara zake,Kama Mke wake tu Doctor Lilian alipiga simu nakumpongeza Lissu wewe mpango wakando kwanini hukubali halihalisi?
 
Mtafute sasa akuajiri kwenye biashara zake,Kama Mke wake tu Doctor Lilian alipiga simu nakumpongeza Lissu wewe mpango wakando kwanini hukubali halihalisi?
Haya matusi mmeyatumia kupata madaraka, kwa hiyo ndio mtaendelea kutukana watu namna yani ndio utamaduni wenu?
 
Acha kulia lia wewe,yaliyopitasondwele tugange yajayo tukijenhe chama chetu imara na chenye nguvu kuwa imara zaidi.
 
Mbowe ataumia kwa namna kundi la usaliti lilivyofanya kazi haramu (fitna) kumuondoa, mbaya zaidi ni wale wale watu wake wa karibu kabisa ndiyo wamemfanyia huo uhuni.
Cha msingi wameshapewa chama - wapambane kuijenga CDM imara ili wasije chekwa mambo yakienda mrama na nahodha kujitosa baharini - hatuombei.

Mziki wa kuongoza chama cha upinzani tena Kikuu si wa kitoto, usipojipanga vizuri unaweza kukikimbia chama.
 
What is democracy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…