Kama mimi ningekuwa ni mzee mwenyewe ningeiuza ile nyumba ya Sea View kuondoa hilo wingu la vita vya kifamilia. fedha zinopatikana kutokana na mauzo ningewagawia watoto kila mtu aaanzie na "deposit" ya nyumba zao maana wamesoma na wana kazi.
Ila Baharia alipokuwa majuu nae alikosea mahala lakini bado (kutokana na nafasi ya familia kwenye jamii) alikuwa na nafasi ya kurekebisha mambo hapa na pale khasa watoto wake.
Hivyo nae angejenga nyumba kubwa tu kwa ajili ya wanae ili wapate pa kuanzia maisha, Nyumba kubwa yenye vyumba vya kujitosheleza vinojitegemea. Hata kama kuna matatizo na wanae lakini angeonekana bado alikuwa na mawazo nao.
Nae mama Anne nae akiwa mbunge alipaswa kuwa na nyumba hadi nne za uhakika za kuwaachia wanae.
Mbona mama Anne Makinda amejipanga uzuri na moja ya nyumba alizonazo ya familia ipo pale Kijitonyama na wametulia tu? Hivyo akiwa Dar kuna nyumba na watoto wake na wajukuu hawana shida ya pa kufikia kwa muda.
Lazima ukiwa kichwa cha familia ujipange na upange la sivyo ukifa waacha taabu, laana na visasi nyuma yako.