Mimi ushauri wangu:
Wazazi, iwe baba au mama au nyote msipungukiwe upendo kwa watoto wenu. Sijui katika uislam, lakini katika ukristo, soma vitabu vyote na kitabu kikuu cha biblia, hakuna hata sehemu moja ilipoandikwa kuwa mimba ni dhambi au kupata mimba ni dhambi au mtoto wa aina fulani ni dhambi. Dhambi ni uzinzi, mimba siyo dhambi, mtoto siyo dhambi. Bali tunaambiwa wapendeni watoto wenu wasije wakakata tamaa. Tubu uzinzi wako, kisha katimizi wajibu wako kwa mwanao.
Na kwa watoto waliofanywa wa hadhi ya chini kwa sababu ya historia ya kupatikana kwao, msihuzunike na kujilaani, mmekuja Duniani kwa mapenzi ya Mungu. Jibidisheni, pambaneni, msikose kutimiza wajibu wenu wa kuwaheshimu wazazi wenu.
Kumbukeni Mungu amewashusha wenye enzi katika viti, akawakuza wanyenyekevu. Mungu wetu huwabariki zaidi wanyenyekevu waliodharaulika ili kuwafedhehesha wenye nguvu waliojawa kiburi.
Jiulizeni, mfalme Sulemani alizaliwa kwa mama yupi? Obedi baba yake Yese, Yese aliyekuwa Baba yaje Daud, alikuwa wa mama Yupi? Maadam umezaliwa, ni binadamu kama wengine, mengine yatategemea juhudi zako na baraka za Mungu.