GE2025 Pole sana Mrisho Gambo, nadhani umeona mwenyewe unachopanda ndicho utakachovuna. Karibu mtaani

GE2025 Pole sana Mrisho Gambo, nadhani umeona mwenyewe unachopanda ndicho utakachovuna. Karibu mtaani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Huyo Katambi ana kitu gani hadi Rais atake awe mbunge.?

Au ni mwenzetu?
Hana kitu Ila kipindi yupo Chadema alikuwa anajenga hoja vizuri Sana

Kama unavyojua magufuli alikuwa anaangalia brain popote zilipo anazichukua ndo ukaona watu Kama Bashiru , Katambi , n.k

Ila shida ya Ccm ni mfumo ikiwa mfumo upo weak hakuna anayeweza kuleta mabadiliko chanya.
 
Hivi hata picha huoni ndugu mbona ni rahisi sana kuelewa hii mambo! 😁

makonda ndo anatakiwa na system ya chama
Gambo hatakiwi kachokwa hasa na chama kwa tabia zake ambazo hazieleweki kwa wenzake wa chama na chama chenyewe kwa ujumla
Makonda anatakiwa na system ya chama nani akakwambia ungejua ungekaa kimya
 
Nikifikiria maneno ya Mchengerwa dakika za mwisho ni kama hii Ngoma inachezewa juu simuoni Gambo akitoboa na huenda siasa zake zikaishia hapo.

Upo mpasuko nauona Arusha ila ndo CHADEMA hatashiriki ILIKUA sehemu sahihi ya kuonesha Dunia udhalimu na umuhimu mabadiliko. Kuna maeneo YALIKUA open sana Kwa upinzani BASI TU🫥
Mchengerwa alisemaje kuhusu Gambo na kwanin maneno yake yawe na uzito kiasi cha kuhitimisha safari yake ya kisiasa hasa katika angle ambayo imetawaliwa na maamuzi ya kidemokrasia?
 
Kwani kilimo hakimfai Gambo habari imeisha hiyo Mkuu
Jina la Gambo litarudi miongoni mwa majina matatu, atapigiwa kura na wajumbe, atashika nafasi ya pili nyuma ya Makonda. Mwenyekiti taifa atampitisha Gambo kama mgombea wa jimbo. Makonda atakaa benchi tena kusubiri teuzi zingine
 
Gambo umejionea mwenyewe .

Lema yupo na Access ya Canada
Familia yake inaishi na watoto wanasoma ulaya .

Ulimfanyia Figisu
Akakosa ubunge
Ukaharibu reputation yake


But now it is ur time to reap ur karmic debt .

Pole Sana , What you sow you shall reap.

Hii ndo universe utamfanyia MTU ubaya Ila lazima you will pay that debt .

Na wanakutoa Bungeni kipindi ambacho unataka Sana huo ubunge .

Ila Makonda jinsi ulivyomfanyia Gambo utalipia that karma na wewe ni swala la Muda .
Ningepewa nafasi ya ushauri, Makonda si mwanasiasa, alitakiwa kubaki kwenye kazi Za kiutawala. Kusimamia utendaji. Huu ubunge utampwaya
 
Gambo umejionea mwenyewe .

Lema yupo na Access ya Canada
Familia yake inaishi na watoto wanasoma ulaya .

Ulimfanyia Figisu
Akakosa ubunge
Ukaharibu reputation yake


But now it is ur time to reap ur karmic debt .

Pole Sana , What you sow you shall reap.

Hii ndo universe utamfanyia MTU ubaya Ila lazima you will pay that debt .

Na wanakutoa Bungeni kipindi ambacho unataka Sana huo ubunge .

Ila Makonda jinsi ulivyomfanyia Gambo utalipia that karma na wewe ni swala la Muda .

Nakumbuka vizuri gambo alivyomkashifu Marehemu.
Lilikuwa ni suala la muda tu maana alijiona mwamba sana.

Yako wapi majigambo yako Gambo????
 
Hizi ni jitihada tu za propaganda mfu (kujipa umuhimu ambao watu hawana) ili kuwashawishi wajumbe ionekane kama vile Makonda ana backup ya Samia ili wamuone kama vile ni pendekezo la chama.

Bi-Tozo kaweka msimamo wake wazi na adharani ajatuma mtu jimbo lolote au kwa njia nyingine yeyote ya kupewa ubunge.

Mbona raisi kaweka wazi yeye ana nafasi zake 10 za kuteua wabunge, anaemtaka atamuweka huko ndio maana Chalamila hakuchukua form.

Vinginevyo huko mtaani ni gombania goli, hakuna alietumwa na Samia wala CCM.

Hakuna mtu alietumwa na Samia, if anything vigogo wa sasa CCM wamezichoka tabia za Makonda.
Kwahiyo ulitegemea rais aseme hadharani kuna aliyemtuma? Huyo Makonda muda wote watu walikuwa wanasema anafanya kick ili awe mbunge wa Arusha, yeye akawa anakana kuwa hajasema atagombea. Leo yako wapi? Kusoma hujui, hata picha huoni?
 
Nyerere, Mwinyi na Kikwete walimhujumu nini Mengi?
Soma vizuri nilichoandika.

Mengi nimemtolea mfano katika awamu ya JK ,liko wazi kama unakumbuka alifukia mahali akaamua kuwataja Mafisadi Papa.
Mafisdi Papa ulitegemea walikua wako nyuma nani na tenda zote za serikali walishika wao mpaka kuagiza vifaa muhimu sana kwa usalama wa nchi .Yaani serikali inajenga mfumo wa Kibepari kwa kutumia wageni badala ya wenyeji wanaoumizwa na kodi na ushuru .
Nyerere alitaifisha Mali nyingi sana za watu wa kaskazini japo ilikuwa nia njema kwa ajili ya umoja wa kitaifa . Lakini. Mwinyi alipoileta Azimio la Zanzibar alitelekeza viwanda na vyama vya ushirika imara sana na wakulima wa kanda ya Kaskazini ikiwemo wakulima wa kahawa ,Ngano ,shayiri , wafugaji waliokua wanauza maziwa kwenye viwanda vya maziwa pale Arusha , wakulima wa mahindi na maharage n.k . Wananchi wakakoseshwa soko kwa makusudi na hayo mazao yakaokekana hayana soko kokote ndani na nje ya nchi .

Mkapa akauza mpaka nyumba za NHC .Eti sinaendeshwa kwa hasara . Akauza viwanda vyote vya Arusha na Moshi vilivyokuwa vinatoa ajira kwa maelfu ya vijana na akina mama wa Tanzania hasa wa ukanda huo . Wakabaki vijana wakabaji ,wavuta bangi wanaotembea na visu na bisibis mfukoni .
Mkapa aliwafulisi wafanyabiashara wengi pale Arusha akiwemo Verani Tango kwa kisingizio kuwa alikua anakwepa kodi .
Palikua na mtu anaitwa askofu alifilisiwa kwa tuhuma kuwa alimuunga mkono Mrema .Chuki za kisiasa .
Mkapa akawafukiza wazawa kwenye machimbo ya mererani kwa sababu tu walimzomea wakati wa Kampeni mwaka 1995 na kusukuma gari la Mrema.
Vijana wa mirereani wakageuka kuwa vibaka na wavuta bangi wasio na hela uchumi wa wenyeji wa Arusha ukayumba sana.

Mkoa wa Arusha ukageuka kuwa eneo la uhakifu na ujambazi wa kuuana kwa sababu uchumi wao ulivurugwa sana.

Akaja JK , alipomtoa Lowasa kwa sababu ya fitina za kisiasa na maslahi binafsi ndipo alipowapa Nguvu Hawa wahuni na wavamizi wa rasilimali xa umma wakiwemo waarabu wa Loliondo na wamisri waliokua wanamchukia Lowasa kwa sababu alifanya maamuzi magumu kutumia maji ya Ziwa Victoria kuwanufaisha watanganyika . Vita ikaanza chini chini kuhakikisha Lowasa hatoboi maana walijua akitoboa Nchi ya Loliondo itatarudi katika utawala wa Tanzania .
Mengi akawa ni mtu jasiri na msema kweli akapigwa vita sana . Walijaribu kumfanya awe chawa akakataa kuwa chawa wa wanasiasa.

Akaja JPM , huyo alifunga mpaka Mirerani eneo ambalo wenyeji walilivumbua wenyewe na kuchimba madini kwa juhudi zao wenyewe bila msàada wowote wa serikali zaidi ya aerikali kushindwa kuweka mfumo wa kukusanya kodi kwa haki bila hila na rushwa kwa maafisa wa Kodi.
Huyu pamoja na nia yake nzuri kwa Taifa lakni alikosea kutumia mguvu kubwa kuua upinzani ma uhuru wa watu wa Arusha kuchagua Mtu wa kusemea kero zao kwa wazi bila unafiki ambaye alikua ni Mtoto wao anayejua shida zao yaani Godbless Lema .
Matajiri wengi wakafa vifo vya utata kwa sababu ya mali zao kuhujumiwa . Hata Ndesamburo hatujajua nini kilitokea na Regnald Mengi pia mchezo gani ulichezwa ; Anyway Kifo ni kifo tu tuachane na hayo .

Awamu ya Sita inatumia nguvu kubwa kuwaziba wananchi midomo,kuwatisha watu,kuwapoteza na hata kuwaweka ndani na kuwajaza hofu lakni kwa drama ya hali ya juu sana ili ionekane kuwa wananchi wanafurahia uhuni huo .
Awamu ya Sita imepora ardhi kunwa sana ya wamasai na kuwapa Waarabu na wazungu .
Hatujawahi kusikia makonda akisema chochote kuhusu Ardhi ya Loliondo zaidi ya kwenda kula Bata kwenye nchi jirani ya falme za Kiarabu iliyoko Loliondo . Makonda akishinda ubunge na Samia akarudi tena kwa kishindo bila kuwa na bunge lenye wapinzani halisi ni wazi kuwa Mpango wa kuwahamisha wamasaidi utarudi kwa kasi na wataongezeka na Wahazabe kuondolewa kwenye ardhi yao yenye rutuba na mazingira ya asili yenye neema kubwa ili wapewe Waarabu na Wazungu .
Hakuna mtu mwenye akili timamamu anayependa kuona watu wanauawa au kupotezwa wakati kuna sheria .
Usanii wa awamu hii ni mkubwa sana na unafanyika Kwa kutumia mbinu nyingi ikiwemo ile ya kumpeleka Makonda pale Arusha ili aonyeshe kuwa anapambana na ufisadi wakati ananufaika na mafisadi na mabilionea wakubwa huku akijifanya kusikizliza shida ambazo kimsingi zinasababishwa na mifumo mibovu waliyoiasisi wao wenyewe ili kuwafanya wananchi kuwa watu wasiojua haki zao.

Kama wapinzani hasa Chadema hawana mpango wa kugombea basi ni bora kumchagua Mbunge wa ACT kuliko kuacha jimbo hilo kikaenda kwa Makonda wa CCM . Wanaarusha mtalia na kusaga meno hasa huyo mtu kwa bahati mbaya sana akawa waziri . Atawaumiza sana wale wanayoipinga serikali na pia atatumia kila mbinu kuwamaliza wapinzani wake kisiasa kwa namna yoyote ile . Ni kati ya watu hatari sana kwa uhai wa binadam. Binadamu Ukiingia kwenye anga za Makonda ni bora uingie kwenye mto wenye mamba maana anaweza akatokea kiboko akakuokoa.

Wana wa Arusha na Wapenda Haki na umoja, upendo na mshkamano msipokuwa makini Mtakuja kukumbuka shuka asubuhi kukiwa kumepambazuka
 
Gambo umejionea mwenyewe .

Lema yupo na Access ya Canada
Familia yake inaishi na watoto wanasoma ulaya .

Ulimfanyia Figisu
Akakosa ubunge
Ukaharibu reputation yake


But now it is ur time to reap ur karmic debt .

Pole Sana , What you sow you shall reap.

Hii ndo universe utamfanyia MTU ubaya Ila lazima you will pay that debt .

Na wanakutoa Bungeni kipindi ambacho unataka Sana huo ubunge .

Ila Makonda jinsi ulivyomfanyia Gambo utalipia that karma na wewe ni swala la Muda .

Gambo ni mzalendo.
Alikua mkuu wa mkoa asiyejilimbikizia Mali kwa hila na kuwatusha Matajiri .
Alikuajirahidi maana Lema alikua mtata sana . Makonda asingeweza kumvumilia Lema hata sekunde Moja kwa siasa za wakati ule .Lema angekua a,eshasahaulika kabisa duniani .

Kudhani kuwa Makonda yupo kwa ajili ya kumkomoa Gambo ni kujidanganya sana.
Lazima ujiulize ni kwa nini Makonda anamkomoa Gambo wakati wote ni chama kimoja ? Ingakuaje kama Gambo angekua ni wa Chama cha upinzani? Ukipata jibu ndio utajua Makonda amatumika namna gani kuzuia haki katika taifa hili na kuipoteza kabisa mizizi ya haki.

Kumbuka Makonda alitumika kumpiga Jaji Warioba na kuzuia mchakato wa kuelimisha jamii juu ya Katiba mpya . Wakati huo huo Dr. Mvungi akalazwa kwenye ardhi milele. Makonda huyo akaibukia kwenye Bunge maalumu la Katiba na kushawishi Makamu wa Rais awe Samia . Wakati huo Samia alikua ndiye Naibu spika wa Bunge la katiba na spika akiwa ni Samweli Sita ambapo Sita alitegemewa sana kuwa Rais kwa maana kwamba makamu wake angekua pia ni Samia ambao walishadhoofisha kabisa bunge la Katiba na kuvuruga mchakato wa katiba bora ya Warioba .

Lakni pia kuna tetesi zilzokuwa zinavuma kwamba hata yule Mbu aliyemdondosha Deo Filikunjombe makonda alimshtua Yule Mwamba asipande . Kwa maana kuwa huyo jamaa alikua anajua huo mchongo na alishiriki kuuandaa.
Huyo mtu mnamchaguaje kuwakilisha wananchi katika ardhi hii yenye bado vidonda vibichi vya utekaji na ukatili na mauaji ya kisiasa ?
 
Mchengerwa alisemaje kuhusu Gambo na kwanin maneno yake yawe na uzito kiasi cha kuhitimisha safari yake ya kisiasa hasa katika angle ambayo imetawaliwa na maamuzi ya kidemokrasia?
Na bado unaamini katika siasa za demokrasia kwenye hii Dunia hasa kwenye michakato ya ndani ya vyama???
 
Gambo umejionea mwenyewe .

Lema yupo na Access ya Canada
Familia yake inaishi na watoto wanasoma ulaya .

Ulimfanyia Figisu
Akakosa ubunge
Ukaharibu reputation yake


But now it is ur time to reap ur karmic debt .

Pole Sana , What you sow you shall reap.

Hii ndo universe utamfanyia MTU ubaya Ila lazima you will pay that debt .

Na wanakutoa Bungeni kipindi ambacho unataka Sana huo ubunge .

Ila Makonda jinsi ulivyomfanyia Gambo utalipia that karma na wewe ni swala la Muda .
What comes around,goes around.
 
Gambo umejionea mwenyewe .

Lema yupo na Access ya Canada
Familia yake inaishi na watoto wanasoma ulaya .

Ulimfanyia Figisu
Akakosa ubunge
Ukaharibu reputation yake


But now it is ur time to reap ur karmic debt .

Pole Sana , What you sow you shall reap.

Hii ndo universe utamfanyia MTU ubaya Ila lazima you will pay that debt .

Na wanakutoa Bungeni kipindi ambacho unataka Sana huo ubunge .

Ila Makonda jinsi ulivyomfanyia Gambo utalipia that karma na wewe ni swala la Muda .
Enzi za Kina Gambo, Muro, Mnyeti, Sabaya, Makonda, Hapi......safi sana.

Lakini Gambo ni Mtu wao. Atapewa u RC
 
nafikiri makonda yupo overrated Sana .

Na unafikiri wapinzani hawayajui yote hayo Mkuu

Tatizo mfumo uliopo haumruhusu mpinzani kugombea na kushinda .

Ikiwa yatapatikana mabadiliko basi uchaguzi utaleta maana.

Wapinzani walikua wanasalitiana wenyewe kwa wenyewe.
Kama hakuna usaliti na kura nyingi zikapigwa hakuna mtu wa kushindana na nguvu ya umma.

Lakini ukitegemea kuwa eti akina Makonda waende Bungeni kuleta katiba na sheria nzuri za kuwatoa wao wenyewe madarakani au kuwaondolea umaarufu wanaoupata kwa kutumia vyombo vya dola basi siku hiyo Shetani naye atajitokeza na kubatizwa na kumwamini Yesu na kukiri kuwa Yesu ndiye Mwokozi wa dunia .
 
Back
Top Bottom