Poleni sana wamachinga, hiyo ndiyo CCM haijawahi kubadilika

Tena Koma kama u

Tena koma kabisa kumtaja JPM hiyo ni habari nyingine nyie endeeni na mambo yenu wakati sisi tukiomboleza!
 
Kwa hili la wamachinga na namna wanavyoendesha shughuli zao ni mtu mjinga pekee ama machinga mwenyewe anayeweza kulitetea. Ni kweli kila mmoja anatakiwa kuwezeshwa kupata riziki yake lakini iwe kwa utaratibu. Mji umekuwa kama vijiji vya ujamaa?
Anayepashwa kulaumiwa ni marehemu Magufuli kwa kuwadanganya kuwa hawawezi kuguswa na mtu yeyote kisa walimchagua.
 
Nchi zetu hizi za Afrika zinaendeshwa kwa upepo yaani, upepo ukivuma hivi kwa kiongozi twende, mwingine upepo ukivuma hivi tena twende. kazi kweli kweli
 
NILIWAHI KUAMBIWA NA MZEE MMJA WA KIMAKONDE HUKO MSUMBIJI LONG TIME

"UKIONA MLANGO UKO WAZI TIA AKILI IKO SIKU MOJA MLANGO UTAFUNGWA"

OVA
Hilo wana ccm hawalijuhi maana wanajiona Tanzania ni mali yao
 
"Serikali ya CCM ni serikali ya wanyonge" in Mwendazake voice...

Kazi iendelee..
 
Saa nane usiku ndio wanakuja kuvunja ili waibe vizuri. CCM, Mgambo wa jiji na PGO ni wezi zaidi ya mafisi.
 
wamachinga walitumika sana kumtuka Lisu na upinzani kwa ujumla....walimuona mwendazake na makonda kama masihi wao.
Leo hii wanalia na kusaga meno kudadadeeki zao
 
Nimeshangazwa kupitia UTV channel mkuu wa Wilaya anahojiwa asubuhi kwa kile kikichotokea usiku wa manane anadai haielewi na hana taarifa.Huyo ndo mkuu wa Wilaya ambaye tukio limefanyika ndani ya wilaya yake huku yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ukinzi na usalama wa wilaya ! angekuwa Magu angeshakula kichwa mara tu alipotoka kwenye camera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…