Poleni sana wamachinga, hiyo ndiyo CCM haijawahi kubadilika

Poleni sana wamachinga, hiyo ndiyo CCM haijawahi kubadilika

Siku zote kitambaa cha kaniki kitabakia kuwa kaniki tu.

Wamachinga walidanganywa sana na mwendazake kuwa ccm inawajali sana hivyo wakaingia mkenge na kuisapoti mwaka 2015.

Leo hii yule bwana hayupo tayari wameanza kilio cha samaki .
Nawashauri wajue kuwa ccm haijawahi kuwa na huruma .

View attachment 1949458
Mkuu, mie nina maoni tafauti. Ni zaidi ya wiki sasa tokea serikali imewatahadharisha wafanyabiashara ndogondogo kuhusu maeneo ya kufanyia biashara zao. Kumbuka reli ya kati ilijengwa kwa mjeledi na Mjerumani vinginevo.............
 
Nakubaliana na wewe bila shaka yoyote.
Lkn hao walizoeshwa na kupewa uhakika kuwa hakuna atakaye wagusa kisa waliichagua ccm.

Leo hii ccm hiyo hiyo inawageuka na kuwaachia simanzi
 
CCM ni cancer, usishangae 2025 wakawaambia warudi
Sawa sawa na kwa ujinga wao watarudi na kusahau machungu wanayo yapata leo kwa kuhangaika na mabox kichwani
 
Mtanikumbuka..........

Humu JF kuna watu wanafiki, kipindi kule Mwendazake alipowaruhusu wamachinga,walimponda humu sana, halafu leo wanamsema Mwendazake mbaya.

Leo ukizisoma comments zao unahisi labda watu wawili tofauti.

Erythrocyte kaka naona yale maombi yako ya machinga watolee mijini kipindi cha Mwendazake akiwa rais yamesika, ila navyo kujua leo utakuwa upande wa wamachinga (threads na comments zako ninazo).
 
Hizi mbinu Za Kuvunja Usiku wa Manane aliwahi kuzitumia Mzee Kandoro Enzi hizo....Zilizalisha Chuki Ya Ajabu zidi Ya C.C.M ilifika mahala Ukionekana Umevaa Sare Zao Unazomewa mji Mzima....!
Sasa Mzee Makalla ndo kaja na ubunifu huu,
Ama Kweli Wavunja chama ni Wale wale Wenyewe....!
 
Nimeshangazwa kupitia UTV channel mkuu wa Wilaya anahojiwa asubuhi kwa kile kikichotokea usiku wa manane anadai haielewi na hana taarifa.Huyo ndo mkuu wa Wilaya ambaye tukio limefanyika ndani ya wilaya yake huku yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ukinzi na usalama wa wilaya ! angekuwa Magu angeshakula kichwa mara tu alipotoka kwenye camera
aibu kwa kweli! kama serikali ilikuwa inachukua 20 za vitambulisho na bado wanalipiaga ushuru kwa kweli wamewafanyia kitendo cha kikatili sana! ni aibu!
Mkuu wa mkoa awajibike haiwezekan watu wabomolewe usku wa manane ina maana Serikali imekuwa na maharamia hivi
 
Mtu anayetetea machungu hajielewi imagine hawalipi Kodi, wanaziba barabara na mitaro wanachafua mji na wako kila corner halafu waachwe in the name of wanyonge, pia hao machinga walikuwa wanapata faida kubwa vile hawalipi Kodi, mambo ya OSHA na Kodi kibao. Mimi natamani jiji zima lisafishwe barabara ziwe clean na waende sehemu zilizotengwa kihalali
 
Makala anajua analofanya

Muda utasema

SIo mjinga yule mtoto wa mjini...

Lazima kapata ruhusa ya kimyakimya...

Mji ulichafuliwa na wamachinga...

Wafanye biashara kwa kufuata utaratibu.... Sasa mtu anaweka kibanda juu ya mtaro wa maji unategemea nini? Mwingine anatundika bidhaa kwenye transformer... ,wingie anapanga bidhaa mbele ya duka la mtu... Mwingine anachoma mahindi barabarani....
 
Siku zote kitambaa cha kaniki kitabakia kuwa kaniki tu.

Wamachinga walidanganywa sana na mwendazake kuwa ccm inawajali sana hivyo wakaingia mkenge na kuisapoti mwaka 2015.

Leo hii yule bwana hayupo tayari wameanza kilio cha samaki .
Nawashauri wajue kuwa ccm haijawahi kuwa na huruma .

View attachment 1949458

Nimeona kikundi kidogo alichokuwa anaongea nacho samia huko marekani nadhani tuweni wawazi kuwa hao sio wafanyabiashara ila ni wadau wachache sana. Sijaona tija kwenye hilo

Pia nimeona picha ya samia imewekwa huko marekani kama bango kuna umuhimu gani kwani wa marekani hiyo picha inawaletea nini??
Hii billboard inatusaidia nini kama nchi na bajeti yake inatokea wapi BUNGE LINAJUA HIVI SHIDA TUNAZOPATA HUKU ZIMETATULIWA!?

AKINA DIAMONDI HUWA WANAWEKA HIZO BILLBOARD ILI WAUZE NYIMBO ZAO

JE? KUWEKWA HUKO PICHA YA RAISI WETU INAMUSAADA GANI
KWANINI WASIWEKE PICHA ZA VIVUTIO VYA UTALII KWANI PICHA YAKE RAISI INAMUSAADA GANI KUWEKWA KAMA PICHA YA BILLBOARD HUKO MAREKANI
 
Mtu anayetetea machungu hajielewi imagine hawalipi Kodi, wanaziba barabara na mitaro wanachafua mji na wako kila corner halafu waachwe in the name of wanyonge, pia hao machinga walikuwa wanapata faida kubwa vile hawalipi Kodi, mambo ya OSHA na Kodi kibao. Mimi natamani jiji zima lisafishwe barabara ziwe clean na waende sehemu zilizotengwa kihalali
Naunga mkono hoja...
 
Screenshot_20210923-145450.png

Screenshot_20210923-145442.png

Screenshot_20210923-145328.png
 
Tatizo wamachinga wanajiweka kwenye kundi la vulnerable kama wasiojiweza wazee na watoto. Wanataka serikali iwapatie sehemu za biashara, iwape mitaji, wasifuate sheria zozote, wasilipe kodi , hata akiwa na uwezo wa kukodi fremu hataki
Wanataka kupata faida huku wakikwepa gharama zingine imagine kariakoo wao hawalipi Kodi ya jengo, na gharama zingine wao ni kupanga tu popote pale na wanapata faida ila Kodi hawaki kulipa pili wanachafua mazingira jiji zima linaonekana chafu vibanda vya hovyo kila corner
 
Back
Top Bottom