GE2025 Polepole acharuka: CCM yavunja Misingi, Haki yazimwa, Katiba ilichakachuliwa na Utekaji wazidi kutisha

GE2025 Polepole acharuka: CCM yavunja Misingi, Haki yazimwa, Katiba ilichakachuliwa na Utekaji wazidi kutisha

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu!

Ule Mkutano na Vyombo vya Habari wa Humphrey Polepole ndio leo – Julai 18, 2025 saa 5:00 asubuhi.

Awali, mkutano huu ulikuwa umepangwa kufanyika Julai 17, lakini Polepole alitangaza kuusogeza mbele hadi leo Ijumaa, tarehe 18 Julai 2025.

Unategemea kusikia nini kutoka kwake?

1752816882078.png

View: https://www.facebook.com/602529134/videos/1035169325065298
​

"Leo nazungumza nikiwa na Moyo mzito sana, imenichukua muda kidogo kutafakari mambo haya, kwa moyo mzito kabisa nimelazimika kuchukua uamuzi niliouchukua"

"Kwangu mimi na wenzetu Watanzania kuahirishwa kwa Kura za Maoni ilikuwa jambo kubwa na la msingi kabisa kwasababu, Katiba inayopendekezwa ilikuwa mbaya"

"Naamini Katiba inayopendekezwa na Watu. Wahuni ndio wameshiriki kuchakachua maoni na Katiba"

"January imefika, February mkutano Mkuu. Mkutano Mkuu wa kuchagua Makamu M’kiti. Tunaangalia LIVE, Mimi kutoka Cuba. Yule anatoa hoja kama vipi tumalize yote hapa hapa. Kikwete akachukua mic, akasema kama vipi tumalize yote hapa hapa. Nikasema NOOOO!"

"Amani ni tunda la haki, haipendezi chama changu cha CCM kutokuzingatia haki za watu, badala yake kinazungumzia amani pekee. Nawaasa turejee kwenye misingi ya chama chetu, tuthamini na kuzingatia haki za watu, kwani viongozi wasiozingatia haki watapata laana."

"Kuhusu mambo ya utekaji, siyaungi mkono. Dada yangu ametekwa jana. Mimi napost post ya kwanza, wamesharuka ukuta. Wamemtia pingu dada yangu. Wamempiga vibao"

"Hata wakati tunaelekea kwenye Uchaguzi wa 2020 kuna watu huko kwenye majimbo yao walianza kutaka baadhi ya majimbo fomu iwe moja lakini tulikataa kwasababu ni utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi hauruhusu fomu moja"

"Kwenye Chama cha mapinduzi kuna desturi hazijaandikwa lakini hazijawahi kuvunjwa ila Rais Samia kazivunja"

"Rais Samia alimteua hadharani na kila mmoja akaona, kwanini yeye asijibu hadharani."

Kuhusu Kesi ya Tundu Lissu

"Sheria zinanibana, siwezi kuzungumzia kesi ya Lissu kwa kuwa ipo mahakamani." – Humphrey Polepole

"Mwaka 2015 nilikemea kauli mbili na nikasema si za kiuongozi."

"Kauli ya kwanza ilikuwa ya Nape kuhusu goli la mkono. Nikasema haiakisi misingi ya CCM, aache mambo hayo na ayatenganishe na CCM."

"Ya pili ilikuwa kauli ya Tundu Lissu pale Kawe. Alisema: 'Uchaguzi ukiwa huru na haki..., na kama isipoachia tutakwenda Ikulu kuichukua kwa nguvu ya umma.' Nikasema hii si kauli ya kiuongozi. Kuna Katiba, pambana kuiboresha na mustakabali wa vyama vya siasa."

"Hatuwezi kuvunja taratibu ili kutatua changamoto. Lakini serikali ya wakati ule ilimpuuza pamoja na kutoa kauli hiyo. Na mtu ukimpuuza na jambo linaendelea kupotea – ndiyo maana hamlijui."

"Mwaka 2020 alitoa kauli ya pili nayo mkaibinua-binua. Alisema CCM wametumia vitambulisho vya wamachinga kununua magari yale. Mimi nikiwa msemaji wa chama, nikajua anataka tuchukue hatua ya kisheria. Nikasema hatumfungulii kesi ng’oo, tukampuuza."

"Nadhani hii ni historia yake. Ila yale ya msingi tuyafanyie kazi, lakini anayoyazungumza sasa hayana msingi – yapuuzieni."

Kuhusu Waziri Mkuu kughairi kugombea Ubunge

"Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kughairi kugomea ubunge ilikuwa baada ya wewe kumfumbua macho'?, amejibu kuwa yeye hajaongea na waziri mkuu, wala Makamu wa Rais, labda wao wamejiongea kujua desturi kwasababu mimi nilipoonaga anasema anagombea, nikasema ni haki yake kisheria, lakini kwenye CCM kuna desturi na ndio uimara wa chama"

==============For English Audience=============
​
Humprey Polepole Speaks Out "CCM must Return to its founding Principles"

The saga continues as Polepole speaks out on July 18, 2025, via Facebook live addressed the nation voicing concerns about the state of democracy, internal party affairs within CCM and growing injustices he believes are being ignored.

“For me and fellow Tanzanians, the postponement of the constitutional refeorms was a major and necessary step because the proposed constitution was fundamentally flawed. It wasn’t a people’s constitution. Thugs manipulated public views and tampered with the draft." he said

He further condemned violations of personal freedom and called accountability in cases of political and human rights abuses. He accused the current President of breaking long standing but unwritten party traditions and pointed questions regarding transparency in leadership decisions.

Humphrey Polepole’s address wasn’t just a political statement it was a public airing of long-held grievances from within the system. His emotional tone, personal revelations, and bold criticism of the ruling party mark a turning point in his political journey. Whether this signals a resignation, a defection, or a larger movement remains to be seen. What is clear, however, is that he has positioned himself as a vocal advocate for justice, transparency, and a people-centered democracy.
 
Ana drama nyingi kama anataka fanyiwa send off, Hakuna press wala Nini, watamshika sio mda mrefu, au watatoa cable za internet baharini kuizima internet Tanzania nzima.

Mtu anaangaika utazani anaenda kulipiwa mahari bwana????!!?
 
Leo tutajua mbivu na mbichi, nimemsikiliza ktk ile video yake anayo elezea kuvamia kwa dada yake huko bahari beach. anaonekana ni mtu ambaye amejitoa muhanga kwa lolote lile ngoja tusubiri huo muda ufuke tuone yapi atakayoyazungumza.
 
Umeona alivyotoa kicheko cha kebehi kwa watekaji? Yule inaonekana ni zaidi ya tumjuavyo
 
Wakuu!

Ule Mkutano na Vyombo vya Habari wa Humphrey Polepole ndio leo – Julai 18, 2025 saa 5:00 asubuhi.

Awali, mkutano huu ulikuwa umepangwa kufanyika Julai 17, lakini Polepole alitangaza kuusogeza mbele hadi leo Ijumaa, tarehe 18 Julai 2025.

Unategemea kusikia nini kutoka kwake?
NAUZA NYUMBA INA APARTMENT MBILI DAR

Ninauza nyumba yangu hapa vikindu nyuma ya mtaa wa polisi mwenye uhitaji unipigie 0625784681. Au wasap 0673294681. Ni nyumba ina apartments 2 na vyoo ndani.

Bei tsh. 23,000,000.00

Nitapunguza kidogo.
Nicheki wasap kama unahitaji picha na detailed information. Kataa mawinga
 
Ana drama nyingi kama anataka fanyiwa send off, Hakuna press wala Nini, watamshika sio mda mrefu, au watatoa cable za internet baharini kuizima internet Tanzania nzima.

Mtu anaangaika utazani anaenda kulipiwa mahari bwana????!!?
Haya ndo mambo mnaweza kufanya kwa weledi Ila mkiambiwa maendeleo mnakuwa na mwendo wa Kobe.
 
Ana drama nyingi kama anataka fanyiwa send off, Hakuna press wala Nini, watamshika sio mda mrefu, au watatoa cable za internet baharini kuizima internet Tanzania nzima.

Mtu anaangaika utazani anaenda kulipiwa mahari bwana????!!?
Hili limenigusa
 
alafu anakua kunavitu anahitaji kuviongea lakini anapatwa na kigugumizi labda hiyo saa 5 atafunguka kila kitu japo amesema atafunguka kwa 25%
Mjinga nini si bora akae kimya akaongee na familia yake hizo 25% tunataka 100 zote ndio maana nikasema huyu anatafuta kupigwa mawe
 
Wakuu!

Ule Mkutano na Vyombo vya Habari wa Humphrey Polepole ndio leo – Julai 18, 2025 saa 5:00 asubuhi.

Awali, mkutano huu ulikuwa umepangwa kufanyika Julai 17, lakini Polepole alitangaza kuusogeza mbele hadi leo Ijumaa, tarehe 18 Julai 2025.

Unategemea kusikia nini kutoka kwake?
yuko wapi? takataka tupu ile mavi uharo mtupu
 
Attachments

  • polepole enzi zake.mp4
    8.7 MB
Back
Top Bottom