Wakuu!
Ule Mkutano na Vyombo vya Habari wa Humphrey Polepole ndio leo – Julai 18, 2025 saa 5:00 asubuhi.
Awali, mkutano huu ulikuwa umepangwa kufanyika Julai 17, lakini Polepole alitangaza kuusogeza mbele hadi leo Ijumaa, tarehe 18 Julai 2025.
Unategemea kusikia nini kutoka kwake?
"Leo nazungumza nikiwa na Moyo mzito sana, imenichukua muda kidogo kutafakari mambo haya, kwa moyo mzito kabisa nimelazimika kuchukua uamuzi niliouchukua"
"Kwangu mimi na wenzetu Watanzania kuahirishwa kwa Kura za Maoni ilikuwa jambo kubwa na la msingi kabisa kwasababu, Katiba inayopendekezwa ilikuwa mbaya"
"Naamini Katiba inayopendekezwa na Watu. Wahuni ndio wameshiriki kuchakachua maoni na Katiba"
"January imefika, February mkutano Mkuu. Mkutano Mkuu wa kuchagua Makamu M’kiti. Tunaangalia LIVE, Mimi kutoka Cuba. Yule anatoa hoja kama vipi tumalize yote hapa hapa. Kikwete akachukua mic, akasema kama vipi tumalize yote hapa hapa. Nikasema NOOOO!"
"Amani ni tunda la haki, haipendezi chama changu cha CCM kutokuzingatia haki za watu, badala yake kinazungumzia amani pekee. Nawaasa turejee kwenye misingi ya chama chetu, tuthamini na kuzingatia haki za watu, kwani viongozi wasiozingatia haki watapata laana."
"Kuhusu mambo ya utekaji, siyaungi mkono. Dada yangu ametekwa jana. Mimi napost post ya kwanza, wamesharuka ukuta. Wamemtia pingu dada yangu. Wamempiga vibao"
"Hata wakati tunaelekea kwenye Uchaguzi wa 2020 kuna watu huko kwenye majimbo yao walianza kutaka baadhi ya majimbo fomu iwe moja lakini tulikataa kwasababu ni utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi hauruhusu fomu moja"
"Kwenye Chama cha mapinduzi kuna desturi hazijaandikwa lakini hazijawahi kuvunjwa ila Rais Samia kazivunja"
"Rais Samia alimteua hadharani na kila mmoja akaona, kwanini yeye asijibu hadharani."
Kuhusu Kesi ya Tundu Lissu
"Sheria zinanibana, siwezi kuzungumzia kesi ya Lissu kwa kuwa ipo mahakamani." – Humphrey Polepole
"Mwaka 2015 nilikemea kauli mbili na nikasema si za kiuongozi."
"Kauli ya kwanza ilikuwa ya Nape kuhusu goli la mkono. Nikasema haiakisi misingi ya CCM, aache mambo hayo na ayatenganishe na CCM."
"Ya pili ilikuwa kauli ya Tundu Lissu pale Kawe. Alisema: 'Uchaguzi ukiwa huru na haki..., na kama isipoachia tutakwenda Ikulu kuichukua kwa nguvu ya umma.' Nikasema hii si kauli ya kiuongozi. Kuna Katiba, pambana kuiboresha na mustakabali wa vyama vya siasa."
"Hatuwezi kuvunja taratibu ili kutatua changamoto. Lakini serikali ya wakati ule ilimpuuza pamoja na kutoa kauli hiyo. Na mtu ukimpuuza na jambo linaendelea kupotea – ndiyo maana hamlijui."
"Mwaka 2020 alitoa kauli ya pili nayo mkaibinua-binua. Alisema CCM wametumia vitambulisho vya wamachinga kununua magari yale. Mimi nikiwa msemaji wa chama, nikajua anataka tuchukue hatua ya kisheria. Nikasema hatumfungulii kesi ng’oo, tukampuuza."
"Nadhani hii ni historia yake. Ila yale ya msingi tuyafanyie kazi, lakini anayoyazungumza sasa hayana msingi – yapuuzieni."
Kuhusu Waziri Mkuu kughairi kugombea Ubunge
"Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa kughairi kugomea ubunge ilikuwa baada ya wewe kumfumbua macho'?, amejibu kuwa yeye hajaongea na waziri mkuu, wala Makamu wa Rais, labda wao wamejiongea kujua desturi kwasababu mimi nilipoonaga anasema anagombea, nikasema ni haki yake kisheria, lakini kwenye CCM kuna desturi na ndio uimara wa chama"