Polepole alifanya kosa kubwa kutowafichua waliomteka dada yake. Sasa na yeye ametekwa

Polepole alifanya kosa kubwa kutowafichua waliomteka dada yake. Sasa na yeye ametekwa

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
38,298
Reaction score
72,863
..alidai waliomteka dada yake amewaona.

..na akadai anawajua waliowatuma.

..badala ya kuwaweka wazi yeye akaendelea na mambo yake.

..watekaji wakajipanga upya na sasa wamemteka.

..hili ni fundisho kwa sisi wengine tuliobaki.

..Si busara kutowafichua wahuni, na watekaji.
 
Yule Augustino alisema,Polepole ana pitchi mwilini. Ndo maana watekaji wanamtafuta. Sijui kwa nini alisema hivyo wazi wazi ? Maana kwa kusema hivyo watekaji lazima wamtafute kwa udi na uvumba.Pole pole nae kafa ni siri nyingi mno
 
..alidai waliomteka dada yake amewaona.

..na akadai anawajua waliowatuma.

..badala ya kuwaweka wazi yeye akaendelea na mambo yake.

..watekaji wakajipanga upya na sasa wamemteka.

..hili ni fundisho wa sisi wengine tuliobaki.

..Si busara kutowafichua wahuni, na watekaji.
Kwenye series za Polepole na Gwajima kila wakija na epsode zao kwenye social media walikuwa wanamalizia kwa kusema, "...siku nyingine nikirudi nchi itasimama...., nitakuja na vitu vizito..." kana kwamba anaowasema wao hawana mipango ya kumdhibiti

Binafsi nilikuwa najiuliza na siku zote nimekuwa nikisema; ilikuwa inashindikana nini kuja moja kwa moja? Yaani kama ni mabomu unayalipua hapo hapo na biashara inaisha.

Sasa mpaka hapa hatujui Polepole hajasema nini na umuhimu wa hivyo ambavyo hajasema

Hili liwe fundisho na kwa wengine wote wanaotaka kutetea maslahi ya nchi yatu. Ukija kuwabagaza wahuni sema yote unayoyafahamu ili kazi ibaki kwa wananchi
 
Yule Augustino alisema,Polepole ana pitchi mwilini. Ndo maana watekaji wanamtafuta. Sijui kwa nini alisema hivyo wazi wazi ? Maana kwa kusema hivyo watekaji lazima wamtafute kwa udi na uvumba.Pole pole nae kafa ni siri nyingi mno
Alikosea sana kusema vile, watekaji wana resources wanaweza kumpeleka kwenye X ray machine ili kujua chip iko implanted sehemu gani ya mwili wake.
 
..alidai waliomteka dada yake amewaona.

..na akadai anawajua waliowatuma.

..badala ya kuwaweka wazi yeye akaendelea na mambo yake.

..watekaji wakajipanga upya na sasa wamemteka.

..hili ni fundisho wa sisi wengine tuliobaki.

..Si busara kutowafichua wahuni, na watekaji.
Ndio maanaa kaka yake amesema anawajua hivi huoni anavyoongea kwamba anawajua au unafikiri Mwafwele amemtaja kwa bahati mbaya?
 
Biashara ishaisha ,polepole ndiyo ntolee hautomsikia tena kama Mdude,Soka etc
Hujajibu swali. Huo uhakika uhakika umeutoa wapi?

Watu wamewekeza juhudi wanapambana kumtafuta hadi pale itapojulikana rasmi vinginevyo.

Haisaidii chochote kwa wakati huu watu wanapambana kumtafuta, wewe kuleta uzushi kwamba amekwisha kufa unless una ushahidi usio na shaka.
 
Ndio maanaa kaka yake amesema anawajua hivi huoni anavyoongea kwamba anawajua au unafikiri Mwafwele amemtaja kwa bahati mbaya?
Siyo tu ana taarifa inaonekana anaambiwa kila wanachofanya na watu walio ndani ya genge la Abdul na Mafwele.

Kuna uwezekano anapata live information kutoka kwa wazalendo pamoja na ushahidi wa mawasiliano yao, mipango yao mpaka video zao wakiwa kazini.

Nafikiri wanataka wamkamate wamuulize nani anampa taarifa na kumfunga mdomo.

Itakuwa risk kubwa kwao watekaji kumuua Polepole wakati kuna ushahidi wao ndio waliomteka, pamoja na dada yake huko nyuma.
 
Hujajibu swali. Huo uhakika uhakika umeutoa wapi?

Watu wamewekeza juhudi wanapambana kumtafuta hadi pale itapojulikana rasmi vinginevyo.

Haisaidii chochote kwa wakati huu watu wanapambana kumtafuta, wewe kuleta uzushi kwamba amekwisha kufa unless una ushahidi usio na shaka.
Wewe elewa biashara ishaisha ,washamalizana naye,mambo ya kusema sijui yupo kigamboni sijui yupo underground ni uzushi tu......Jamaa wakiteka ndani ya siku 2 kama hawana nia na wewe wanakuDAMPU ila zikizidi siku 2 means wanakupoteza mazima hata mfupa hauonekani.
 
Huu ni uzushi au ushahidi? Unasaidiaje jitihada za kupiga kelele kumtafuta Polepole na kuiwajibisha serikali na kukomesha haya matendo ya utekaji, utesaji?

Kungangia kwamba ameuwawa wakati huna ushahidi wowote ni jambo ambalo watekaji wanafurahia sana. Na unasaidia kufanya kazi yao ya propaganda.
 
Back
Top Bottom