Polepole alifanya kosa kubwa kutowafichua waliomteka dada yake. Sasa na yeye ametekwa

Polepole alifanya kosa kubwa kutowafichua waliomteka dada yake. Sasa na yeye ametekwa

Hata polepole alishawataja. Ndio nami nimemuuliza JokaKuu , alitaka watajwe kwa style ipi zaidi ya wanavyootaja kila Mara? Katajwa mafwele mara zote, katajwa Abdul.
Huyu joka kuu anataka watajwe kwa style ipi?
Tukubali hatuna Cha kufanya. Uamuzi wa kuacha au kuendelea wanao wao wenyewe Wala tusitafute kichaka cha kujifichia
Ni kweli mkuu. Wabongo ndivyo tulivyo. Tuna-treat kila jambo kama tunaangalia movie. Hata wakitajwa watu wanakuwa kimya
 
..nadhani Polepole angeuonyesha umma waliomteka dada yake tungekuwa tumepiga hatua nyingine nzuri.
Joka kuu umekumbwa na nini? Polepole alishasema kikosi cha utekaji kilipo na kinaongozwa na nani

Lakini pia unataka kuchukua hatua gani baada ya kuwajua?
 
Tukio la dada yake alishaeleza, ndio nimekuuliza ilibuidi aeleze kwa namna ipi?
Mmetajiwa kuwa kikosi kipo chini ya abdul? Mmetajiwa mafwele. Umeshawajua je umefanya jitu gani?

Taarifa muhimu ndio hizo,mmetajiwa sana. Ni taarifa zipi zaidi ya hiuzo ulitaka kuzisikia?

..ni kweli wametajwa.

..lakini wangeonyeshwa wakajulikana kwa sura, au maumbile, ingesaidia zaidi.
 
..watu waliokuwa kwenye tukio.

..abduli na mafwele hujificha nyuma ya vijana wao.
Humkusikia vizuri polepole? Leo kaka yake karudia hilo tukio na kaeleza tena kuwa mafwele alikuwepo wakati dada yake alipoenda kukamatwa

Pili, kuhusu hao vijana unaosema. Wao Wala hawana issue, wao wanapokea order

Kuna mtu aliwahi kusema sirro aondolewe kwenye IGP, hakujua kuwa sirro hata yeye anapokea tu order, alikuja IGP mwingine bado yanaendelea yaleyale.
Kuna kipindi watu walikua wanamlaumu masauni, wakataka aondolewe, akaondolewa akaletwa bashungwa. Je yameisha au ndio yamezidi?

Bado hujagundua hapo tatizo lipo wapi?
 
Polepole akija kuonekana akiwa hai kwangu utakuwa moja ya maajabu ya dunia.
Kwa jinsi alivyowabananga hao wahuni halafu wamuache bila kumpoteza.
 
Siyo tu ana taarifa inaonekana anaambiwa kila wanachofanya na watu walio ndani ya genge la Abdul na Mafwele.

Kuna uwezekano anapata live information kutoka kwa wazalendo pamoja na ushahidi wa mawasiliano yao, mipango yao mpaka video zao wakiwa kazini.

Nafikiri wanataka wamkamate wamuulize nani anampa taarifa na kumfunga mdomo.

Itakuwa risk kubwa kwao watekaji kumuua Polepole wakati kuna ushahidi wao ndio waliomteka, pamoja na dada yake huko nyuma.

..yeyote anayewajua watekaji kwa, majina, na sura, anapaswa kuwa na ujasiri wa kumwaga ushahidi huo hadharani, vinginevyo watekaji wataendelea kutamba.
 
Kaka ake asingesema tu yakuwa polepole ana chip mwilin.
Wangewinda kimyakimya
 
Ile ilikuwa geresha ya kutisha watekaji tu.

..nilitegemea Mama atajiepusha na mambo ya utekaji, na mauaji.

..angepiga kazi wakosoaji wake wangekosa hoja za kumshambulia.

..kwa maoni yangu utekaji na mauaji yanawapa wakosoaji wake hoja za kudumu za kumshambulia na kumdhoofisha.

..mbele ya safari, Mama akisema anataka maridhiano, suala la waliotekwa, kutekwa, na kupotezwa, litachukua nafasi kubwa, na kuleta ugumu kufikia maridhiano.
 
..alidai waliomteka dada yake amewaona.

..na akadai anawajua waliowatuma.

..badala ya kuwaweka wazi yeye akaendelea na mambo yake.

..watekaji wakajipanga upya na sasa wamemteka.

..hili ni fundisho kwa sisi wengine tuliobaki.

..Si busara kutowafichua wahuni, na watekaji.
Dada yake na kaka yake si wapo alishawaambia na akina nani waliomteka dada yake na record za CCtV si zipo au zimefutwa?
 
..nilitegemea Mama atajiepusha na mambo ya utekaji, na mauaji.

..angepiga kazi wakosoaji wake wangekosa hoja za kumshambulia.

..kwa maoni yangu utekaji na mauaji yanawapa wakosoaji wake hoja za kudumu za kumshambulia na kumdhoofisha.

..mbele ya safari, Mama akisema anataka maridhiano, suala la waliotekwa, kutekwa, na kupotezwa, litachukua nafasi kubwa, na kuleta ugumu kufikia maridhiano.
Watu wana uwezo wa kuiba mpaka uchaguzi, wanateka na kuua watu ili iweje sasa?
 
Yule Augustino alisema,Polepole ana pitchi mwilini. Ndo maana watekaji wanamtafuta. Sijui kwa nini alisema hivyo wazi wazi ? Maana kwa kusema hivyo watekaji lazima wamtafute kwa udi na uvumba.Pole pole nae kafa ni siri nyingi mno
Wenda kaumizwa ila hajafa, maneno ya Kaka yake tusiyachukulie poa , anasema atatoa up to date kaumia wapi na wapi alipo ,na ole wake atakae mzulu , aya sio maneno ya kitoto.

Kaka yake kwa sasa ndo mtu wa kudhibitisha kama amekufa au la ,tusubili mda mwalim.

CV yake kwanza hatuijui , his plan not known, so huwezi kuwa na conclusion juu ya hii mkuu
 
Dada yake si Yupo ?

Na hata ukiwataja kitakachofaa ni kwenye Court of Public Opinion ila sio Mahakamani kunapohitajika evidences na ni kauli yako baina ya yao....

Hapa kama nilivyosema TATIZO kuu kushinda yote tumepoteza Imani na kutokuaminiana na vyombo vyetu vya Ulinzi ; Kwahio ni vema tuka-press a reset button na ili tuanze vizuri na kuendelea waje hata Scotland Yard au Yoyote yule atakayeaminika katika macho ya watu ili wapatikane wa kupatikana na wafikishwe kwa Pirato na kupata chao kwa mujibu wa Sheria tulizojiwekea....

Na baada ya hapo tuseme tume-turn another page kwa kuishi kama wastaarabu in a Just Society (which is not biased or political motivated)

 
Back
Top Bottom