Polepole alifanya kosa kubwa kutowafichua waliomteka dada yake. Sasa na yeye ametekwa

Tujilinde tusitekwe ila jamaa wakifanikiwa kukuteka kurudi ni ngumu ,hakuna kujipa moyo.

Mimi ni mfuasi mkubwa wa KATAA WAHUNI ,leo ni day 4 tunaendelea kucount.
 
Tujilinde tusitekwe ila jamaa wakifanikiwa kukuteka kurudi ni ngumu ,hakuna kujipa moyo.

Mimi ni mfuasi mkubwa wa KATAA WAHUNI ,leo ni day 4 tunaendelea kucount.
Tusubiri taarifa rasmi kutoka kwa familia, wakili wake. Kaka, wakili wake wanasema wamuachie, watu wake wa karibu wanaamini bado yupo hai.

Kuna uwezekano mkubwa Familia yake, wakili wake na connections walizonazo ndani ya vyombo vya dola wanajua hali halisi, nini kinaendelea.

Nina uhakika watatupa umma taarifa, updates na status ya Polepole from time to time.
 
Sawa Mkuu.
 
Mbona Mo alipatikana baada ya zaidi ya hizo siku ulizozitaja?
 
Ila huyu mwamba ametekwa kindezi sana yaani kama kuku kizembe sana
ukishakuwa adui wa state yoyote unatakiwa uishi kwa machale na mawenge mda wote!
 
Hawa wazalendo unaowazungumzia hapa hebu wabadili modus operandi yao. Honestly wanatuchosha na hawatusaidii kitu. Kama ni wazalendo kweli watake sheria ziwape “meno” zaidi. Kama kufanya rescue au vinginevyo.

Nasema hivi kwanini, Kwa mnaojua mnajua, Viongozi wengi “wawindwaji” wamekuwa wakipenyezewa taarifa kadha wa kadha miaka na miaka, Mfano Tundu Lissu kufuatiliwa, ZZK kukamatwa airport kipindi fulani, vitisho dhidi ya Mbowe, Wanaharakati kadhaa wa mitandaoni hata mpaka sasa wanaambiwa leo muwe makini, nani na nani wako mitaa fulani wanamtafuta fulani. Sasa unajiuliza mimi kama mwananchi wa kawaida ukiniambia jilinde na ongeza umakini zaidi, najilindaje na kuongeza umakini zaidi dhidi ya genge lenye resources zote? Hawaoni ni suala la muda tu lazima wanipate? Kama wao ni wazalendo kweli kwanini wasiombe waboreshewe sheria waweze kuwalinda hawa watu? NB: Sijabagaza power ya information wanayowapatia wahusika, nachosema in the long run, zaidi ya kunijaza info ambazo zitaniongezea paranoia hamna kingine wanachowasaidia……….

Mfano tujadili bila hisia, Wao kuwapa info familia ya mhusika, ndio familia ya mhusika ifanye nini? Familia haina jeshi wala resources zozote kwaajili ya chochote zaidi ya kufanya pushback kupitia midomo ya watz-mtandaoni.

Ndio maana hii kazi ya “wazalendo” kwa miaka mingi watu tumeichukulia kama kazi ya umbea tu, Sorry not sorry!
 
Wazalendo kwenye mifumo inayofanya kazi inavyotakiwa kazi yao ingekuwa kuwaongezea ulinzi wahusika na kuwakamata wahalifu wanaopanga njama za kuwaumiza watu wasio na hatia. Ila hao wahalifu ndio viongozi wa hiyo mifumo na Taasisi.

Inaonekana wanafanya kazi kwa kujifichaficha, sababu kwa sasa wamezidiwa nguvu na wahuni kwenye mifumo yote. Kwa sasa systems karibu zote zipo corrupted chini ya wahuni. Kimsingi tunahitaji katiba mpya, kuibadilisha kabisa mifumo yote ya ulinzi na usalama wa raia na mifumo ya kutenda haki.
 
Ndio maanaa kaka yake amesema anawajua hivi huoni anavyoongea kwamba anawajua au unafikiri Mwafwele amemtaja kwa bahati mbaya?

..kuna msemo wa Kiswahili, "linalowezekana leo, lisingoje kesho."

..tangu dada yake Polepole atekwe na kurudishwa, kuna watu wametekwa, wameteswa, na wameuwawa.

..Na zaidi kwa kukaa na taarifa hizo Polepole naye ametekwa, na hatuna uhakika kama yuko hai.

..Watekaji wafichuliwe bila kuchelewa, ili wasilete madhara zaidi.
 
Mkuu JokaKuu ulitaka awataje hao watu kwa namna ipi? Alishawataja zaidi ya mara moja. Alisema kikosi cha utekaji kipo chini ya Abdul

Ukiacha kutaja watekaji, ametaja mambo mengine mengi. Je yamesaidia nini hadi sasa? Maana jnatoa lawama kuwa angetaja sijui ingepunguza nini
Kawatajia mambo mengi yaliyotokea na yanayotokea
 
Wabongo mnajua kulaumu na kukosoa tu. Tuseme kwa yote aliyozungumza polepole ulitaka aseme kipi cha ziada kwa alokwisha yasema? Wewe binafsi umefanya jitihada zipi? Mungu amlinde Polepole popote alipo.
 

..alipaswa kuliweka wazi tukio la utekaji wa dada yake.

..kama Polepole aliwaona watekaji, basi na sisi tunaomuunga mkono tulipaswa kuwaona.

..binafsi simlaumu lakini natoa tahadhari ya jinsi ya kuenenda kwa wanaharakati na wananchi kwa ujumla.

..tusikalie taarifa muhimu zinazoweza kuwaokoa wengine.
 
Tukio la dada yake alishaeleza, ndio nimekuuliza ilibuidi aeleze kwa namna ipi?
Mmetajiwa kuwa kikosi kipo chini ya abdul? Mmetajiwa mafwele. Umeshawajua je umefanya jitu gani?

Taarifa muhimu ndio hizo,mmetajiwa sana. Ni taarifa zipi zaidi ya hiuzo ulitaka kuzisikia?
 
Mkuu wewe ni mkongwe hapa lakini thread ya leo mh... Kwani watekaji hawajulikani? Kwani watekaji wanaogopa kutajwa? Deus Soka mbona alipigiwa simu na polisi kabisa na inajukana? Mdude naye kuna polisi alitajwa alikuwa anaulizia anapokaa. Hii serikali iliyojitoa akili na ina-operate kimafia unadhani wanaogopa kutajwa?
 
Hata polepole alishawataja. Ndio nami nimemuuliza JokaKuu , alitaka watajwe kwa style ipi zaidi ya wanavyootaja kila Mara? Katajwa mafwele mara zote, katajwa Abdul.
Huyu joka kuu anataka watajwe kwa style ipi?
Tukubali hatuna Cha kufanya. Uamuzi wa kuacha au kuendelea wanao wao wenyewe Wala tusitafute kichaka cha kujifichia
 

..nadhani Polepole angeuonyesha umma waliomteka dada yake tungekuwa tumepiga hatua nyingine nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…