PolePole alipaswa kuisoma na kuielewa Katiba ya CCM IBARA YA 99 (2 na 3)

PolePole alipaswa kuisoma na kuielewa Katiba ya CCM IBARA YA 99 (2 na 3)

Katika Ibara hii ndio unapata ni nini haswa nguvu na mamlaka ya Mkutano mkuu.
Tusipotoshe umma kwa kutokusoma vyema katiba ya CCM.
Haya tupe na za msajili wa vyama au tume utaratibu wa kupata wagombea ni kuchukua form au kikundi fulani kikiamua na iwe hvyo watampokea kama mgombea?
 
funaku wengine wanasema kuwa wewe ndiye pia Jingalao 😄😀😀😃

Jee unataka Kwa kutumia Katiba hiyo ya CCM tuijadli hoja hiyo ya Polepole. Kama upo tayari nijulishe.
Ndio maana ya hoja hii kuja jamvini.
Mkutano mkuu unayo nguvu na mamlaka ya kuamua lolote na ndio chombo cha mwisho cha kimaamuzi.
mfano :Mkutano mkuu uliwahi kuivunja TANU na ASP na ikazaliwa CCM.
Zaidi tulijionea how transparent mkutano mkuu ulivyokuwa.
Kama kuna mjumbe aliyekuwa na hoja kwenye mkutano mkuu angeiwasilisha.
Sitegemei kuona mjumbe mmoja akatoka na kutaka maoni yake yatekelezwe vs mkutano mkuu.
 
Katika Ibara hii ndio unapata ni nini haswa nguvu na mamlaka ya Mkutano mkuu.
Tusipotoshe umma kwa kutokusoma vyema katiba ya CCM.
Alikuambia hajaielewa ama hiyo ndiyo tafsiri yako?
 
99. (1) Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utakuwa
na wajumbe wafuatao:-
(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Makamu wawili wa Mwenyekiti wa
CCM.

(c) Katibu Mkuu wa CCM.
(d) Rais na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(e) Manaibu wa Katibu Mkuu wa CCM.

Hapo kwenye (d) ndo pamenipa mashaka zaidi. Ndo maana mnapigania rais atokane na ccm daily maana siku akitokea wa chama tofauti na ccm atakuwa ni mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm wa taifa. Kama nchi tuko nyuma sana. Ahadi za wanachama namba 5, sitatumia cheo changu wala cha mwingine kwa faida yangu. Mnatumia cheo cha rais kumpa uenyekiti wa chama ili baadae atumie cheo cha urais kuongoza hadi chama chake. Hivi vitu vitengwe na tusingekuwa na marais wanaothubutu kusema sitawaletea maendeleo kwa kuwa mbunge ni chama pinzani au mgombea asiyechukua fomu kisa kashawahadaa wajumbe kupush ajenda yake.
 
Makamu wa Raisi hawezi kugombea uraisi baada ya awamu yake kuisha, na huyu makamu muda wake umeisha ameshakaa Ikulu miaka 10 asije akapazoea, na akilazimisha atafanya Madudu kuliko yaliyopo apumzike tu awaachie wengine
makamu wa rais ni Mpango Rais Samia na aliapa kama rais
 
Katika Ibara hii ndio unapata ni nini haswa nguvu na mamlaka ya Mkutano mkuu.
Tusipotoshe umma kwa kutokusoma vyema katiba ya CCM.

Kwamba wewe hapo madongori unaijua kuliko katibu mwenezi wenu? 😛 😛
 
Back
Top Bottom