PolePole alipaswa kuisoma na kuielewa Katiba ya CCM IBARA YA 99 (2 na 3)

PolePole alipaswa kuisoma na kuielewa Katiba ya CCM IBARA YA 99 (2 na 3)

Katika Ibara hii ndio unapata ni nini haswa nguvu na mamlaka ya Mkutano mkuu.
Tusipotoshe umma kwa kutokusoma vyema katiba ya CCM.
Kwa mujibu wa katiba hii uliyoshare hapa kuna ibara ningependa uzisome kwanza halafu utupatie majibu. Nadhani maelezo ya Polepole yapo hapo kuwa utaratibu uzingatiwe na siyo kuruka hatua.

Ibara ya 104 (7b) inaeleza kuwa jukumu la kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ni "Kufikiria na kutoa mapendekezo
yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM
ya Taifa juu majina ya Wanachama
wasiozidi watano wanaoomba
kugombea kiti cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
"

Pia ibara hiyo hiyo inaeleza kuhusu upande wa Zanzibar, soma 104 (7 d).

Baada ya kamati kuu kuleta majina matano kwa halmashauri kuu, nipo jukumu la halmashauri kuu tunaliona kwenye ibara ya 102 (12 b) inayosema
"Kupendekeza kwa Mkutano
Mkuu wa CCM wa Taifa majina
yasiyozidi matatu ya Wanachama
wanaogombea nafasi ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na kuyawasilisha mbele ya Mkutano
Mkuu wa CCM wa Taifa
."

Same kwa upande wa Zanzibar ni jina moja kutoka katika matatu yaliyoletwa na kamati kuu, soma 102 (12 c).

Ndipo sasa mkutano mkuu unachagua jina moja kati ya matatu yaliyopendekezwa na halmashauri kuu sawa sawa na ibara ya 100 (5 b),
"Kuchagua jina moja la Mwanachama
atakayesimama katika uchaguzi wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania."


Huu ndiyo utaratibu wa muda wote CCM. Anachosimamia Polepole ni hilo, katiba izingatiwe na pia utaratibu wa CCM waliojiwekea nao uzingatiwe. Fomu zitolewe, wagombea wachukue fomu, watafute wadhamini, warejeshe, kisha hatua stahiki zifuatwe kumpata mgombea.
 
Makamu wa Raisi hawezi kugombea uraisi baada ya awamu yake kuisha, na huyu makamu muda wake umeisha ameshakaa Ikulu miaka 10 asije akapazoea, na akilazimisha atafanya Madudu kuliko yaliyopo apumzike tu awaachie wengine
Kabisa
 
99. (1) Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa utakuwa
na wajumbe wafuatao:-
(a) Mwenyekiti wa CCM.
(b) Makamu wawili wa Mwenyekiti wa
CCM.

(c) Katibu Mkuu wa CCM.
(d) Rais na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(e) Manaibu wa Katibu Mkuu wa CCM.

Hapo kwenye (d) ndo pamenipa mashaka zaidi. Ndo maana mnapigania rais atokane na ccm daily maana siku akitokea wa chama tofauti na ccm atakuwa ni mjumbe wa mkutano mkuu wa ccm wa taifa. Kama nchi tuko nyuma sana. Ahadi za wanachama namba 5, sitatumia cheo changu wala cha mwingine kwa faida yangu. Mnatumia cheo cha rais kumpa uenyekiti wa chama ili baadae atumie cheo cha urais kuongoza hadi chama chake. Hivi vitu vitengwe na tusingekuwa na marais wanaothubutu kusema sitawaletea maendeleo kwa kuwa mbunge ni chama pinzani au mgombea asiyechukua fomu kisa kashawahadaa wajumbe kupush ajenda yake.
Mkuu mwaka huu mtatusomesha katiba za vyama vyote kwa mwendo huu --- kwamba mfano Lissu angepenya 2020 inabidi aalikwe kwenye mkutano mkuu😁 hiki chama cha nyerere watu wakiambiwa Nyerere huyu naye ni muasisi wa utapeli wote huu , wanamkinga kwa kichaka cha baba wa taifa
 
Hapa mjadala ni kutumia Katiba ya CCM. Haya mauzauza yenu pelekeni kwingine!
Hata huko kwenye mkutano mkuu wasanii huitwa kutumbuiza mkuu.

Tupo pamoja mkuu na sakata hili mpaka mwisho
 
Kwanza funaku kwa nini umetumia Katiba toleo la 2017 wakati kabla ya marekebisho ya mwaka huu kulikuwa na Toleo la 2022?

Umempotosha Danos kunukuu kifungu Cha 99 wakati kifungu hicho Kwa Sasa kimekuwa kifungu Cha 100. Hata hivyo maudhui yamebaki ni yale yale hivyo hoja yake bado ni halali.
 
Makamu wa Raisi hawezi kugombea uraisi baada ya awamu yake kuisha, na huyu makamu muda wake umeisha ameshakaa Ikulu miaka 10 asije akapazoea, na akilazimisha atafanya Madudu kuliko yaliyopo apumzike tu awaachie wengine
Kumbe alivyokuwa anataja zile rank na kutogombea kumbe lilikuwa dongo kwa huyu aliyerithishwa cheo cha juu.
 
Wewe ndio unapotosha ngoja nikueleweshe hiyo katiba inavyoeleza.
Soma Ibara ya 20. 1 ambayo inaeleza kwamba kila mwanachama atakayetaka nafasi yeyote ya uongozi sharti kwanza ni lazima AOMBE hiyo nafasi, pia ni lazima achaguliwe kwa kupigiwa kura zaidi ya nusu ya kura halali zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.
Sasa tender kwenye Ibara 99 3 uliyoeelea inasema pia kuhusu mkutano mkuu wa uchaguzi .
Sasa jiulize pale kwenye ule mkutano mkuu kulikuwa na uchaguzi? Nani aliyegombea? Alichukua fomu lini? Kura zilipigwa vipi? Kuna mtu aliyehesabu kura na kuhakikisha mshindi amepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa?
Kilichofanyika pale ni uhuni tu ulioratibiwa na kimbisa pamoja na jakaya .
Polepole yupo sahihi hata yule anayedai mwanachama mwandamizi aliyekwenda Mahakamani kupinga uhuni ule chama kikaamua kufunika kombe kwa kuamua kumfukuza uanachama yupo sahihi , kumfukuza uanachama nao ni uhuni tu.
Kimsingi inaonyesha jinsi hata vile ambavyo huielewi katiba ya ccm kiukamilifu .
Mwisho acha kupotosha Polepole yupo sahihi kusema mchakato wa kikatiba haujafuatwa.
Mkutano Mkuu pamoja na madaraka yake hauna mamlaka ya kumpitisha mtu from nowhere lazima utaratibu wa mtu kuomba kwa kuchukua fomu na kupigiwa kura uwepo
 
Ndio maana ya hoja hii kuja jamvini.
Mkutano mkuu unayo nguvu na mamlaka ya kuamua lolote na ndio chombo cha mwisho cha kimaamuzi.
mfano :Mkutano mkuu uliwahi kuivunja TANU na ASP na ikazaliwa CCM.
Zaidi tulijionea how transparent mkutano mkuu ulivyokuwa.
Kama kuna mjumbe aliyekuwa na hoja kwenye mkutano mkuu angeiwasilisha.
Sitegemei kuona mjumbe mmoja akatoka na kutaka maoni yake yatekelezwe vs mkutano mkuu.
Mbona Mkutano mkuu wa Chadema uliowapitisha Mnyika na wengine Msajili hautambui naruzuku amezuia
 
Hata huko kwenye mkutano mkuu wasanii huitwa kutumbuiza mkuu.

Tupo pamoja mkuu na sakata hili mpaka mwisho
wasanii walitumbuiza na wajumbe waliunga hoja mkono kwa maazimio yaliyotolewa.
CCM ni chama cha wafanyakazi,wakulima na makundi mengine.wasanii wanayo haki ya kuwa wanaCCM.
Donald Trump Rais wa marekani alikuwa kwenye tasnia ya sanaa(Kama ulizaliwa zamani utaijua WWE)
 
Wewe ndio unapotosha ngoja nikueleweshe hiyo katiba inavyoeleza.
Soma Ibara ya 20. 1 ambayo inaeleza kwamba kila mwanachama atakayetaka nafasi yeyote ya uongozi sharti kwanza ni lazima AOMBE hiyo nafasi, pia ni lazima achaguliwe kwa kupigiwa kura zaidi ya nusu ya kura halali zaidi ya nusu ya kura halali zilizopigwa.
Sasa tender kwenye Ibara 99 3 uliyoeelea inasema pia kuhusu mkutano mkuu wa uchaguzi .
Sasa jiulize pale kwenye ule mkutano mkuu kulikuwa na uchaguzi? Nani aliyegombea? Alichukua fomu lini? Kura zilipigwa vipi? Kuna mtu aliyehesabu kura na kuhakikisha mshindi amepata zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa?
Kilichofanyika pale ni uhuni tu ulioratibiwa na kimbisa pamoja na jakaya .
Polepole yupo sahihi hata yule anayedai mwanachama mwandamizi aliyekwenda Mahakamani kupinga uhuni ule chama kikaamua kufunika kombe kwa kuamua kumfukuza uanachama yupo sahihi , kumfukuza uanachama nao ni uhuni tu.
Kimsingi inaonyesha jinsi hata vile ambavyo huielewi katiba ya ccm kiukamilifu .
Mwisho acha kupotosha Polepole yupo sahihi kusema mchakato wa kikatiba haujafuatwa.
Mkutano Mkuu pamoja na madaraka yake hauna mamlaka ya kumpitisha mtu from nowhere lazima utaratibu wa mtu kuomba kwa kuchukua fomu na kupigiwa kura uwepo
unajua kwa nini uliitwa mkutano mkuu maalumu?
 
unajua kwa nini uliitwa mkutano mkuu maalumu?
Peleka uhuni wako uko kwenye katiba ya ccm inaeleza kuhusu mkutano mkuu wa kawaida na mkutano mkuu wa uchaguzi.
Hili la kuita mkutano mkuu maalumu nao ni uhuni ambao haupo kikatiba.
Nipatie ibara yeyote ya ccm ambayo inaelekeza kwamba katika ngazi za vikao vy mkutano mkuu kuna hicho kitu kinaitwa mkutano mkuu maalumu.
Na taratibu zote za uchaguzi ndani ya ccm zimeelezwa vizuri kwenye katiba ya ccm.
Kilichofanyika kwenye ule mkutano mkuu ni uhuni ambao haupo kwenye ibara yoyote ya ccm
 
Kwa mujibu wa katiba hii uliyoshare hapa kuna ibara ningependa uzisome kwanza halafu utupatie majibu. Nadhani maelezo ya Polepole yapo hapo kuwa utaratibu uzingatiwe na siyo kuruka hatua.

Ibara ya 104 (7b) inaeleza kuwa jukumu la kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ni "Kufikiria na kutoa mapendekezo
yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM
ya Taifa juu majina ya Wanachama
wasiozidi watano wanaoomba
kugombea kiti cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
"

Pia ibara hiyo hiyo inaeleza kuhusu upande wa Zanzibar, soma 104 (7 d).

Baada ya kamati kuu kuleta majina matano kwa halmashauri kuu, nipo jukumu la halmashauri kuu tunaliona kwenye ibara ya 102 (12 b) inayosema
"Kupendekeza kwa Mkutano
Mkuu wa CCM wa Taifa majina
yasiyozidi matatu ya Wanachama
wanaogombea nafasi ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na kuyawasilisha mbele ya Mkutano
Mkuu wa CCM wa Taifa
."

Same kwa upande wa Zanzibar ni jina moja kutoka katika matatu yaliyoletwa na kamati kuu, soma 102 (12 c).

Ndipo sasa mkutano mkuu unachagua jina moja kati ya matatu yaliyopendekezwa na halmashauri kuu sawa sawa na ibara ya 100 (5 b),
"Kuchagua jina moja la Mwanachama
atakayesimama katika uchaguzi wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania."


Huu ndiyo utaratibu wa muda wote CCM. Anachosimamia Polepole ni hilo, katiba izingatiwe na pia utaratibu wa CCM waliojiwekea nao uzingatiwe. Fomu zitolewe, wagombea wachukue fomu, watafute wadhamini, warejeshe, kisha hatua stahiki zifuatwe kumpata mgombea.
Mkutano mkuu ndio chombo cha mwisho kinachotafsiri,kubadili,kubariki na kuamua ...Kwa nini hutaki kuikubali haki hiyo ya mkutano mkuu?kwa nini hutaki kukubali ultmate na absolute power ya mkutano mkuu?
Yaani unataka maamuzi na taratibu za vikao vya chini ndio yawe makubwa kuliko yale ya mkutano mkuu?
Lazima kuwa na Chombo chenye ultmate suprimacy....
 
Sasa funaku tuendelee na mjadala. Hiyo Ibara ya 100 (Kwa toleo la 2022) ambayo wewe umeinukuu kama Ibara ya 99 (Kwa toleo la 2017) ndiyo imetaja wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM.

Pamoja na kifungu kuwa Cha 100 maudhui yake hayakubadilishwa. Wajumbe wametajwa kuanzia kifungu kidogo Cha kwanza kifungu (a) - (z).

Jee hao ndiyo wajumbe wa mkutano Mkuu?
 
Peleka uhuni wako uko kwenye katiba ya ccm inaeleza kuhusu mkutano mkuu wa kawaida na mkutano mkuu wa uchaguzi.
Hili la kuita mkutano mkuu maalumu nao ni uhuni ambao haupo kikatiba.
Nipatie ibara yeyote ya ccm ambayo inaelekeza kwamba katika ngazi za vikao vy mkutano mkuu kuna hicho kitu kinaitwa mkutano mkuu maalumu
Soma kwenye katiba vizuri ujue ni nyakati zipi au ni namna gani mkutano mkuu unaweza kuitishwa....Na Mwenyekiti aliitisha.kwa nini unataka kuipoka haki ya Mwenyekiti na wajumbe wake wa mkutano mkuu?
Haki,muundo,majukumu na ukomo wa kimaamuzi wa kila chombo vimetajwa katika katiba ya CCM ...Kwanini tunalazimisha haki na taratibu ya vyombo vya ngazi ya chini viishinde haki ya wajumbe walio wengi wa Mkutano mkuu?
 
Sasa funaku tuendelee na mjadala. Hiyo Ibara ya 100 (Kwa toleo la 2022) ambayo wewe umeinukuu kama Ibara ya 99 (Kwa toleo la 2017) ndiyo imetaja wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM.

Pamoja na kifungu kuwa Cha 100 maudhui yake hayakubadilishwa. Wajumbe wametajwa kuanzia kifungu kidogo Cha kwanza kifungu (a) - (z).

Jee hao ndiyo wajumbe wa mkutano Mkuu?

Ndio hata mimi nashangaa Rais Mstaafu Kikwete kwa mjibu wa wajumbe kikatiba alikuwaje mjumbe kwenye kile kikao
 
Back
Top Bottom