PolePole alipaswa kuisoma na kuielewa Katiba ya CCM IBARA YA 99 (2 na 3)

N.B Baraka na uhalali wa taratibu zote ndani ya ccm inatokana na Mkutano mkuu na sio zaidi au chini ya hapo.
hii ni kwa mujibu wa katiba na sio maoni ya yoyote yule
 
Katika Ibara hii ndio unapata ni nini haswa nguvu na mamlaka ya Mkutano mkuu.
Tusipotoshe umma kwa kutokusoma vyema katiba ya CCM.
Sawa kumfunga mtu mikono kabla ya kumuua ipo kwenye ibara ngapi ya CCM.
 
Ni hivyo kwa vyovyote vile Mkutano Mkuu hauwezi kupoka haki za kikatiba za uchaguzi kama zinavyoelekezwa kikatiba.
Katiba ya ccm ibara ya 20 1 inaelekeza taratibu za uchaguzi ambazo mkutano mkuu lazima uziheshimu.
Ukweli ni kwamba kwa mtu yeyote mwenye akili timamu na muelewa lazima ajue kwamba kilichofanyika kwenye ule mkutano mkuu ni uhuni na uvunjaji mkubwa wa katiba ya ccm
 
Usichotaka kuelewa ni kipi?
Mkutano mkuu unao uwezo hata wa kuammend katiba.mkutano mkuu una mamlaka ya mwisho
 
tatizo nimekuwekea katiba lakini huisomi
Ningekuwa sikuisoma ningejuaje kuwa umetumia toleo la 2017 badala ya toleo la 2022?

Swali langu Kikwete aliingilia ule mkutano kama nani? Maana yeye hakuwa mjumbe wa mkutano ule.
 
Usichotaka kuelewa ni kipi?
Mkutano mkuu unao uwezo hata wa kuammend katiba.mkutano mkuu una mamlaka ya mwisho
Wangetakiwa kubadili basi hivo vifungu vya uchaguzi ili viruhusu ule uhuni waliofanya .
Kwa hiyo wangetakiwa kubadili kifungu cha uchaguzi kinachoeleza kwamba kila nafasi lazima mtu agombee kwa kuchukua fomu.
Wangeweka kifungu kwamba mkutano mkuu wa taifa unaweza kumpendekeza na kumpitisha mtu yeyote kuwa mgombea bila ya mtu huyo kuchukua fomu .
Wangetakiwa kufanya hivyo kabla ili kuondoa huu utata uliofanyika
 
unajua kwa nini uliitwa mkutano mkuu maalumu?
Ulikuwa maalumu kwa ajili ya kumteua makamu mwenyekiti wa chama na siyo mkutano mkuu wa uchaguzi. Utaratibu ulipaswa kufuatwa kumpata mgombea urais. Katiba ilivunjwa huo ndiyo ukweli.
 
Ulikuwa maalumu kwa ajili ya kumteua makamu mwenyekiti wa chama na siyo mkutano mkuu wa uchaguzi. Utaratibu ulipaswa kufuatwa kumpata mgombea urais. Katiba ilivunjwa huo ndiyo ukweli.
kwa hiyo umekubali..kwamba ni mkutano halali.
kwa nini hutaki kuzikubali agenda zake zote zikizofanyiwa maamuzi?
 
Naomba unisaidie kufahamu kama mkutano mkuu unaweza kufanya hata kazi ambazo hazijaainishwa na katiba kuhusu majukumu yake. Soma katiba ya mwaka 2022 ibara ya 101 halafu ufafanue ni wapi hayo uliyoyaeleza yanasimama.
 
Katika Ibara hii ndio unapata ni nini haswa nguvu na mamlaka ya Mkutano mkuu.
Tusipotoshe umma kwa kutokusoma vyema katiba ya CCM.
Mnahangaika sana
Wewe unajifanya unajua katiba desturi za CCM kuliko Polepole, jiulize wapi imeandikwa mtawala asipingwe kabla ya vipindi viwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…