Duh ! mzee we noma ndio nini sasa iki?
Hili ni shairi maarufu sana la mshairi wa Ki Irish W.B Yeats.
Liliandikwa mwaka 1919 lakini ni kama lilitabiri mengi yaliyofuatia. W. B Yeats aliona dunia ikibadilika sana baada ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia kuisha na influenza pandemic of 1918 -1919.
Kama umesoma au kusikia kuhusu kitabu maarufu cha Cjinua Achebe "Things Fall Apart", Chinua Achebe hapa ndipo alipopata jina la kitabu chake. Siku hi,i ukitaja "Things Fall Apart" watu wengi wanajua kitabu cha Achebe kuliko hili shairi la W.B Yeats.
Shairi linaelezea dunia ya mabadiliko sana.
Turning and turning in the widening gyre.
Tunazunguka sana katika dhoruba inayozidi kuwa kubwa na kukua kila siku.
Watanzania wanaweza kulinganusha matatizo yasiyoisha na uongozi mbovu ambao kila siku inayofuata ni afadhali jana yake.
The falcon cannot hear the falconer. Ndege kipanga hamsikii mwenye ndege.
Ndege kipanga ana kipaji cha kuweza kuchukua maagizo kutoka kwa mwenye ndege na kuyafanyia kazi vizuri sana. Lakini hapa tunaona ndege kipanga hamsikilizi tena mwenye ndege.
Balozi hamsikilizi aliyemteua. Rais hawasikilizi wananchi waliompa dhamana. Kimsingi ni wakati wa vurugu ambao hauna kusikilizana.
Things fall apart; the centre cannot hold;
Mambo yanaparaganyika, muhimili wa kati hauwezi kusimama na kuzuia mparaganyiko.
Tulikuwa na uongozi uliofanyia kazi mambo kama umoja wa kitaifa, watu pamoja na umasikini wakajiona wana nchi inayowajali. Leo hii ni kama nchi imeshawashinda viongozi na hawawezi kuimudu.
Mere anarchy is loosed upon the world.
Fujo tupu zinatawala dunia.
The blood-dimmed tide is looswd, and everywhere.
Damu inamwagika kirahisi kila pahali.
Watu wanatekwa, wanapotezwa. Rais anasema "kifo ni kifo tu".
The ceremony of innocence is drowned.
Watu wasio na hatia na waadilifu hawasifiki tena. Waovu ndjo wamechukua nchi.
The best lack all conviction, whike the worst are full of passionate intensity.
Watu wazuri kabjsa hawajiamini kabisa. Wanaogopa hata kuchujua nafasi za uongozi. Wakati watu wabaya kabisa, wasio na sifa, ndio wamejaa maneno mengi makali kunionesha wana miranga cha kuongoza.
Surely some revelation is at hand
Watu wengine wanasema yumkini tutafungukiwa njia karibuni tu.
Surely the Second Coming is at hand
Watu wengine wanasema yumkini kizazi kipya kitatuokoa karibuni
When a vast image out of Spiritus Mundi
Troubles my sight: somewhere in sands of the desert
Picha kubwa la linyama la dunia linapokuja kutisha maono yangu, kule kunapo michanga ya jangwani.
Tulikuwa tunategemea mtu fulani aje kurekebisha matatizo ya awamu ike lakini tunaona picha baya sana
A shape with lion bodh and the head od a man.
Uongozi wa hadaa ambao unatuonesha kichwa cha ubinadamu lakini kiukweli una mwili wa kinyama.
A gaze blank and pitiless as the sun
Unatutazama kwa macho yasiyo na hisia na bila huruma kama jua.
Is moving its slow thighs, while all about it
Reel shadows of the indignant desert birds
Unazembea na kutembeza mapaja yake Polepole ukizungukwa na kivuli cha ndege wa jangwani wenye hasira (kivuli cha DP World).
The darkness drops again; but now I know
Tulikuwa na matumaini kuwa enzi za giza za Magufuli zimeisha, lakini giza limerudi tena, sasa tunajua.
That twenty centuries of stony sleep
Kwamba karne ishirini za usingizi mzito.
Were vexed to nightmare by a rocking cradle.
Zimechafuliwa kuwa ndoto za jinamizi kwa kutikisa kitanda chetu cha utoto.
Tunavyozidi kujielewa na kujua ndivyo tunagundua hali ilivyo mbaya.
And what rough beast, its hour come round at last
Na hili dudubaya gani tumelifikia sasa.
Slouches towards Bethlehem to be born
Linaelekea Bethlehem, sehemu ambayo tulifikiri tutapata uhuru na ukombozi, kuzaliwa huko?
Uhuru wetu tuliofikiri kuwa utatukomboa na kutupa fanaka unatuzalishia dubwana gani hili katika uongozi wetu wa sasa? Uongozi huu utazaa lidubwana gani?