Polepole ashitakiwe kwa uhalifu huu, kama anachosema ni kweli

Watu watakwambia ameomba msamaha na amesamehewa, Kwa hiyo wahalifu wakiomba samahani basi wasamehewe tu.

Kesho JK maslahi yake yakiguswa akaanza kupambana na CCM naye tumsamehe.

HP ni mhalifu kama wahalifu wenzie ndani ya CCM, kinachofanyika ni vita ya maslahi ndani ya mfumo ambayo inaweza kuwa compromise mambo yao ya uhalifu yanaendelea.

Mexico kuna ugomvi kati ya Sinaloa Cartel Vs CJNG Cartel lakini wote ni wauza unga, kidnapers, money laundering , human traffickers na uchafu wote.

Safarini Khartoum Sudan.
 
Ni lazima Polepole aje athibitishe kwanza kauli yake au uchunguzi ufanywe kuthibitisha hayo. Njia rahisi nini yeye kuthibitisha kauli yake, inawezekana anaropoka tu katika kipindi hiki cha uropokaji na waropokaji. Kuna wakati tuliwahi kuonyeshwa picha za majenerali huko Iran ambao ni ndugu zake Salim Ahmed Salim eti kama akiwa Rais hapa majenerali hao wataiteka nchi
Kwa hali ya siasa za nchi hii unafikiri akikanyaga ardhi hii hata maiti yake itaonekana?
 
Kumuamini Polepole aliyechanganyikiwa ni kuchanganyikiwa kuliko Polepole mwenyewe. Polepole ana afya ya akili.
images.jpeg
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.
Unashitakiwa vipi kwanza kulingana na mada ya andiko lako hapo , hivi nyie ccm mna akili kweli? mnajifanya mifumo yote mmeiweka mfukoni sio ,sio mda mtajua hamjui ,ilo likebo lenu, hilo linaenda kuzaa makubwa .

Angalia kichwa cha habari cha mada yako hapa nakuwekea chini ndo ujue ccm akili hamna.

(Polepole ashitakiwe kwa uhalifu huu, kama anachosema ni kweli)
 
Uchaguzi wa 2025 haujatumia mifumo hiyo bado, labda kama bado ipo na wanatarajia kuitumia pia.
TAL anashtakiwa uhaini kwamba alikuwa na NIA ya kutenda kosa.

Unadhani kwa kigezo hicho hicho CCM itasalimlika kwenye hili bomu zito la Polepole?
 
Unashitakiwa vipi kwanza kulingana na mada ya andiko lako hapo , hivi nyie ccm mna akili kweli? mnajifanya mifumo yote mmeiweka mfukoni sio ,sio mda mtajua hamjui ,ilo likebo lenu, hilo linaenda kuzaa makubwa .

Angalia kichwa cha habari cha mada yako hapa nakuwekea chini ndo ujue ccm akili hamna.

(Polepole ashitakiwe kwa uhalifu huu, kama anachosema ni kweli)
Mkuu ndiyo maana nikamwambia hapo juu kwamba hata hao anaodhani kuwatetea wakisikia haya asemayo jamaa, watasonya kwa hasira.

Hiyo ni self-incrimination (kujituhumu).

Halafu huyu wala siyo CCM. Hawa ni mahaba niue wasiotumia akili zao.
 
Ni lazima Polepole aje athibitishe kwanza kauli yake au uchunguzi ufanywe kuthibitisha hayo. Njia rahisi nini yeye kuthibitisha kauli yake, inawezekana anaropoka tu katika kipindi hiki cha uropokaji na waropokaji. Kuna wakati tuliwahi kuonyeshwa picha za majenerali huko Iran ambao ni ndugu zake Salim Ahmed Salim eti kama akiwa Rais hapa majenerali hao wataiteka nchi
Badala ya kumbana Polepole aliyefichua siri hii nzito, kwa nini taasisi zote husika na wahusika wote wasishurutishwe kutoa majibu ya kina kuhusu hii sintofahamu?

Kama wako safi, kuna nini cha kuficha?

Ni muda mwafaka wauthibitishie umma wa Watanzania kwamba Polepole ni tapeli.
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.
Acha ujingaujinga wewe mtu mzima.Polepole ni kama Sila/Paulo mtume.Ameomba radhi na mahakama ya wananchi imemsamehe kasoro wewe na vimbwenerehi wachache mlioko CCM.
 
Hajui kwamba kisheria mhalifu anaweza kusamehewa makosa yake kwa vile amejiweka rehani kuuanika mfumo mbovu.

Kitendo tu cha kujianika kiasi hicho ni hukumu tosha dhidi yake.

Ni dhahiri yuko exposed kwa maadui wa ndani na nje.
 
TAL anashtakiwa uhaini kwamba alikuwa na NIA ya kutenda kosa.

Unadhani kwa kigezo hicho hicho CCM itasalimlika kwenye hili bomu zito la Polepole?
Ccm kama chama kwa mjibu wa polepole ni wahini no moja , wamefanyia uhaini watz .

Naomba wanasheria kutafakari hoja ya polepole ,na nini kinatakiwa kufanyika ndani ya mahakama tz na mahakama za nje , kama kweli likebo lipo , inamanisha tumeongozwa na viongozi hewa .

Wanadoria wa mtandaoni mwaka huu mtawafunga wengi kisa kuwa vibaraka , ila sio mda mtatikiwa kuijua Dunia asema Bwana.

Sasa rasmi

Warudisheni wapendwa wetu waliopotea maana sasa tunajua kumbe wanadoria ndo mmesababisha ndugu zetu kutoweka.

Anzia leo plate no za gari zinazolalamikiwa hazitakiwi barabarani ,jeshi la police mpo , kama mtu yupo na mapenzi na SSH badika stiker kwenye ubavu wa gari yako period na sio plate no
 
Hapana yule mhuni sio nguruwe ni digidigi wa Tarangire, ukiweza kumuona lazima uwe mwenye bahati sana na utapiga hela ndefu na mvua kubwa itanyesha
Polepole kwasasa ni kama nguruwe ndani ya tope, ukitaka kumtoa basi ukubali kuchafuka. Swali, nani atakubali kuchafuka dakika hizi za jioni, October sio mbali mjomba.
 
Mkuu ndiyo maana nikamwambia hapo juu kwamba hata hao anaodhani kuwatetea wakisikia haya asemayo jamaa, watasonya kwa hasira.

Hiyo ni self-incrimination (kujituhumu).

Halafu huyu wala siyo CCM. Hawa ni mahaba niue wasiotumia akili zao.
Hupo sahii mkuu, ccm imejaza vilaza ,yani eti mtu ashitakiwe kisa alichosema ni ukweli, so mahakama inafanyaje hapa wakati mtu alichosema ni ukweli.

Na jitu kama hili unalikuta lipo na familia kqbisa
 
Kwa hali ya siasa za nchi hii unafikiri akikanyaga ardhi hii hata maiti yake itaonekana?
Anachokifanya sio kigeni sana, kwenye chama na Tanzania polepole ni mtu mdogo sana kuliko Oscar Kambona, Ibrahim Babu, Maalim Sharif, Lowasa, kingunge au Membe. Wote Hawa walishindwa kuifuta CCM kwenye ramani. Wanachofanya CCM ni kilekile wanachofanya China, Urusi, North Korea, Cuba na Ulaya mashariki yote. Hata Polepole analijua hilo na anafahamu adhabu ya kupingana nalo. CCM ni zaidi ya chama cha siasa. Hata hivi vyama vingi vilikuja tu kwa busara za Nyerere na vikwazo vya Magharibi.
 
Hajui kwamba kisheria mhalifu anaweza kusamehewa makosa yake kwa vile amejiweka rehani kuuanika mfumo mbovu.

Kitendo tu cha kujianika kiasi hicho ni hukumu tosha dhidi yake.

Ni dhahiri yuko exposed kwa maadui wa ndani na nje.
Duuuuh!! Yaani mtu akizaa na mkeo halafu baada ya miaka 4 anakuja anakwambia nilizaa na mkeo yule mtoto wako wa tatu ninamtaka mwangu samahani sana unisamehe, wewe utamwambia sawa tu chukua mwanao aloo.
 
Ninyi Wanasheria wasomi wa nchi hii hamuwezi kufungua kesi kuishtaki Ccm?
 
Kwa hali ya siasa za nchi hii unafikiri akikanyaga ardhi hii hata maiti yake itaonekana?
Hakuna la kuhoni Wala kukasirika hapa mpaka Polepole aje atuonyeshe mifumo walioweka Iko kwenye chumba kipi na ilikuwa kwa kazi Gani na itatumika namna gani kuiba kura. Aliisanifu yeye na nani. Ni maagizo yake mwenyewe au maagizo ya nani ambae yuko hai au alishakufa. Ndipo sisi tuangalie kama mifumo bado ipo au waliiharibu baada ya JPM kuapishwa.
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.
The Whistleblower Protection Act (WPA) inatutaka tumlinde Kwa wivu mkubwa.
 
Back
Top Bottom