Polepole ashitakiwe kwa uhalifu huu, kama anachosema ni kweli

Polepole ashitakiwe kwa uhalifu huu, kama anachosema ni kweli

Hakuna la kuhoni Wala kukasirika hapa mpaka Polepole aje atuonyeshe mifumo walioweka Iko kwenye chumba kipi na ilikuwa kwa kazi Gani na itatumika namna gani kuiba kura. Aliisanifu yeye na nani. Ni maagizo yake mwenyewe au maagizo ya nani ambae yuko hai au alishakufa. Ndipo sisi tuangalie kama mifumo bado ipo au waliiharibu baada ya JPM kuapishwa.
Acha kujitoa akili kama kweli unazo. Wizi wa Kura Kwa CCM ni kitu kiko Wazi chaguzi zote.
 

Attachments

  • 20250822_161822.jpg
    20250822_161822.jpg
    371.1 KB · Views: 11
The Whistleblower Protection Act (WPA) inatutaka tumlinde Kwa wivu mkubwa.
Huyu sio whistleblower, ni mhalifu kama wahalifu wengine kwakuwa alitengeneza mfumo yeye mwenyewe uliomsaidia JPM tu basi na JPM amekufa na yeye hayuko na nafasi ile iliyomwezesha kutengeneza mfumo ule. Anatakiwa kukamatwa yeye mwenezi, Katibu wa CCM Bashiru Kakulwa, mwenyekiti wa CCM, mkurugenzi wa NIDA na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa mwaka 2020 ili watuongoze kwenye hili.
 
Hakuna la kuhoni Wala kukasirika hapa mpaka Polepole aje atuonyeshe mifumo walioweka Iko kwenye chumba kipi na ilikuwa kwa kazi Gani na itatumika namna gani kuiba kura. Aliisanifu yeye na nani. Ni maagizo yake mwenyewe au maagizo ya nani ambae yuko hai au alishakufa. Ndipo sisi tuangalie kama mifumo bado ipo au waliiharibu baada ya JPM kuapishwa.
Tulizeni mzuka yote yatawekwa wazi mnasingizia Lissu ni mhaini huu sasa ndiyo uhaini wenyewe wa kupindua matakwa ya wapiga kura .
 
Kabla hamjampa Polepole mashtaka tuanzie hapa

Toa maelezo kuhusu video hizi mbili za Nape na ex DC waliosema jinsi CCM inavyoiba kura walichukuliwa hatua gani kisheria .?

Itakuwa na mantiki kama hawa maharamia wawili wa demokrasia wakianza kuchukuliwa hatua kwanza kwani wao ndio walisema mbinu hizi chafu kabla ya Polepole.


View: https://youtu.be/bsMYAk6cWaE?si=3Wt0tkdgTwCRHFeM


View: https://youtu.be/dTvdkX19XOs?si=G57KoUskQ_OX49tF

Hawa akina nape kwanza walikuja kukanusha kwamba ulikuwa utani tu, pamoja na hayo walipoteza uongozi wao hadi Leo. Na Polepole aje aseme kama ni kweli au anatania tu kwaajili ya uchaguzi. Vinginevyo wananchi wampuuze kama walivyowapuuza akina nape.
 
Hawa akina nape kwanza walikuja kukanusha kwamba ulikuwa utani tu,
Weka video ya Nape kukanusha na kusema ni utani , pia thibitisha huo utani ulikuwa unawalenga watu gani.
pamoja na hayo walipoteza uongozi wao hadi Leo.
Well well...ukiwa muongo uwe mwepesi kukumbuka Nape amegombea ubunge alitolewa uwaziri bila kutolewa sababu hivyo hajapoteza uongozi maana kama angepoteza uongozi basi angekuwa ni raia tu wa kawaida

Huyo DC alitenguliwa kweli ila bado serikali haikutoa sababu za utenguzi wake na haikukanusha wala yeye hajawahi kukanusha popote alichokisema , alitenguliwa uDC ila uafisa kipenyo wake alibaki nao pengine kurudia ule mchezo wa maporini katika uchaguzi bandia wa 2025.
Na Polepole aje aseme kama ni kweli au anatania tu kwaajili ya uchaguzi. Vinginevyo wananchi wampuuze kama walivyowapuuza akina nape.
Polepole amejiuzulu kabla ya kuanza kusema hayo na ni mara ya kwanza baada ya miaka 17 kiongozi kujiuzulu nafasi yake ya uteuzi hivyo usimuweke kundi moja na hao watu wengine ambao hawajajiuzulu na wako na nafasi kwenye serikali dhalimu ya bi Mwenda.

Hadi hapo hujanishawishi kusema nimpuuze Polepole labda nikupuuze wewe maana inaonekana unaweza ukawa ni miongoni mwa majizi ya taasisi zilizotajwa sasa unajiandaa tena kwa hadaa nyingine mnayoiita uchaguzi 2025.
 
Weka video ya Nape kukanusha na kusema ni utani , pia thibitisha huo utani ulikuwa unawalenga watu gani.

Well well...ukiwa muongo uwe mwepesi kukumbuka Nape amegombea ubunge alitolewa uwaziri bila kutolewa sababu hivyo hajapoteza uongozi maana kama angepoteza uongozi basi angekuwa ni raia tu wa kawaida

Huyo DC alitenguliwa kweli ila bado serikali haikutoa sababu za utenguzi wake na haikukanusha wala yeye hajawahi kukanusha popote alichokisema , alitenguliwa uDC ila uafisa kipenyo wake alibaki nao pengine kurudia ule mchezo wa maporini katika uchaguzi bandia wa 2025.

Polepole amejiuzulu kabla ya kuanza kusema hayo na ni mara ya kwanza baada ya miaka 17 kiongozi kujiuzulu nafasi yake ya uteuzi hivyo usimuweke kundi moja na hao watu wengine ambao hawajajiuzulu na wako na nafasi kwenye serikali dhalimu ya bi Mwenda.

Hadi hapo hujanishawishi kusema nimpuuze Polepole labda nikupuuze wewe maana inaonekana unaweza ukawa ni miongoni mwa majizi ya taasisi zilizotajwa sasa unajiandaa tena kwa hadaa nyingine mnayoiita uchaguzi 2025.
Tatizo letu kubwa kupita yote Tanzania hakuna vyama vya upinzani strong vya kuweza kushika dola. Ni vyama vya kiharakati na matukio tu, vyenye viongozi ambao nusu ni CCM na nusu upinzani. Akikosana na huku anarudi huku na kutoa Siri zote za kule atokako. Mpina katika huku Leo anakwenda kule siku hiyohiyo kugombea urais
 
Huyu mtu itakuwa ni miongoni mwa majizi yanayofisadi demokrasia hapo NIDA au tume ya mama.
Kabisa maana naona anatokwa na povu utafikiri amesukutua omo, na hapa bado yatasemwa mengi hadi Samia achanganyikiwe kama alivyochanganyikiwa Richard Nixon kwenye kashfa ya Watergate hadi akatema bungo.
 
Tatizo letu kubwa kupita yote Tanzania hakuna vyama vya upinzani strong vya kuweza kushika dola. Ni vyama vya kiharakati na matukio tu
Mbona hujajibu maswali yangu badala yake umejitengenezea mada nyingine?

Anzisha uzi wa mada hii nyingine nitakuja kuchangia.
, vyenye viongozi ambao nusu ni CCM na nusu upinzani. Akikosana na huku anarudi huku na kutoa Siri zote za kule atokako.
Hii ina uhusiano gani na wizi wa kura aliousema Nape au huyo ex-DC?

Unaweza kukanusha sio kweli CCM huwa haiibi kura kwa njia zinazoonekana kwa macho na za nyuma ya pazia na kwa njia mojawapo nina uthibitisho wa video za uchaguzi wa 2020
Mpina katika huku Leo anakwenda kule siku hiyohiyo kugombea urais
ACT na CHAUMMA mtu makini anajua hivyo ni matawi ya CCM.

Nakuuliza tena bado hujatoa hoja za kupinga hizo video mbili na yaliyofanyika je na wewe ni miongoni mwa majizi kutoka taasisi tajwa ?
 
Kabisa maana naona anatokwa na povu utafikiri amesukutua omo, na hapa bado yatasemwa mengi hadi Samia achanganyikiwe kama alivyochanganyikiwa Richard Nixon kwenye kashfa ya Watergate hadi akatema bungo.
Samia hachanganyikiwi ng"o, amesema yeye chura kiziwi hasikii kelele za kutishwa na wakatisha tamaa.

Tatizo letu Kuna watu wanadhani Ulaya ndiye wanaotakiwa kutuadhibu kama tukikoseana. Wako bize kusema na kufanya mbele ya camera za Magharibi ili waone na kusikia kwa matarajio kuwa watatoa adhabu kwa watawala, Hizi ni fikra za hovyo kwakuwa nchi za Magharibi wana njia nyingine za uhakika za kuoana na kusikia mambo. Nchi za Magharibi wana habari zote kuhusu wakimbizi walioko Tanzania, demokrasia ,amani na maendeleo yanayofanywa Tanzania kwenye barabara, elimu, kilimo, uchimaji, umeme, maji, chanjo, afya ya mama na mtoto nk. Hawasubiri taarifa za wahuni kama Polepole, Gwajima, dk. Slaa nk.

Mabalozi wao wanatoa taarifa Kila siku kuhusu Tanzania.
 
Polepole amesema mwenyewe kuwa yeye na wenzake aliowataja walitengeneza mfumo pale CCM na tume ya uchaguzi unaounganisha tume, CCM na NIDA ili kumsadia Magufuli kushinda uchaguzi 2020 kwa njia nyepesi, na mfumo huo ungetumika pia kama mgombea wake ndiye angeteuliwa kuwania Urais.

Kama kweli hili ni kweli Polepole lazima ashitakiwe kwa uhalifu huu mkubwa kiasi hiki.
Ashtakiwe
 
Back
Top Bottom