Balozi Humphrey Polepole aliyetangaza kujiuzulu nafasi ya Ubalozi nchini Cuba hivi karibuni kutokana na madai mbalimbali ikiwemo kutofurahishwa na mwenendo wa serikali na Chama Cha Mapinduzi hasa katika usimamizi wa haki na maadili ya uongozi, ametangaza kuahirisha mkutano wake na wanahabari aliokuwa amepanga awali kufanya Kesho Alhamisi Julai 17, 2025 na badala yake amebainisha kuwa Mkutano huo ataufanya siku ya Ijumaa Julai 18, 2025 saa tano asubuhi.
Katika taarifa yake usiku huu Julai 16, 2025, Polepole amebainisha kuwa sababu ya ahirisho hilo ni kupisha zoezi la Uzinduzi wa Dira ys Taifa ya Maendeleo, Dira ambayo itazinduliwa Alhamisi Julai 17, 2025 Mjini Dodoma na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Niseme kwa moyo mkubwa, kwa unyenyekevu na kwa hofu ya Mungu, tukutane Tarehe 18 Julai, 2025 saa tano asubuhi, Utaratibu wa ushiriki kwa waandishi wa habari nitautoa Kesho jioni Alhamisi Julai 17, 2025" amesema
Source JAMBO TV